SHUHUDA MBALIMBALI.

SHUHUDA MBALIMBALI.
Bwana Yesu Kristo atukuzwe ndugu zangu wote.
Leo nakuletea baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya marafiki zangu waliniandikia baada ya maombi na wengine baada ya kujifunza Neno la MUNGU ambalo MUNGU Baba alinipa neema ya kuandika na kupost.
Nakuletea shuhuda Kama zilivyo lakini sifa, Heshima na utukufu wote kama ulivyo ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
1. Shalom mtumishi wa Bwana Yesu, nashukuru kwa maombi yako kipindi nikiwa mjamzito nashukuru yalifanyika ukuta kwangu nilijifungua salama Ubarikiwe na Bwana.
2. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Najua ulikuwa unaniombea ndio maana naendelea vizur hata kama hukutaja kwa jina lakini naimani uliniombea maana nilikushirikisha uniombee, ndio maana naendelea vizuri ,Leo nimeona nikupe ushuhuda kwa Yale tuliyomuomba Mungu katenda.
Ilikuwa pia nikupigie simu ili pia nikusimulie ndoto ambazo zilikuwa zinanitesa kwa kipindi kirefu na huku nimeokoka nilikuwa najihoji sana kaka yangu,ni nyingi na mazingira ya kuota yanakuwa tofauti mwisho wa siku Mungu kaniponya na jaribu hili namtukuza yeye na kumuinua ,kwa ushindi huu, nafasi yangu inamfurahia Mungu.
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Nashukuru kwa maombi maana baada ya maombi nimedhihirishiwa kwa macho ya nyama ni nani mchawi anayetusumbua.
Nimeona live vituko vya muovu huyu ambaye humtumia mama mwenye Nyumba wangu , kumbe ni mchawi ,naendelea kumuomba Mungu ili mwisho nije kukupigia simu kwa ajili ya ushuhuda mzima.
Ahsante kwa kuomba nami, naomba Mungu akuzidishie Hekima na maarifa zaidi ya ki ungu ili uzidi kutumika katika Ufalme wake namtukuza Mungu kwa ajili ya huduma unayosaidia watu Ubarikiwe na Mungu
4. Asante mtumishi kwa maombi yako maana Mungu ametenda kwangu tangu nimeanza kuuza mitumba mnadani sijawahi kuuza hata elfu kumi na tano lakini kwa maombi yako Mungu kanitendea hata niliuza sh 21000 elfu ishilini na moja namshukuru sana Mungu maana najua Mungu hupendezwa na moyo wa shukrani naomba Mungu azidi kuniinua katika viwango vya juu zaidi.
5. Bwana Yesu asifiwe
Mungu akulinde na akubariki mpaka sasa naishi vizuri mwenye afya na magonjwa yamekata, asante sana kwa maombi yako.
Kwa sasa nasinzia hadi kunakucha ,nyumba vituko vya ndani vimeisha ,maneno mitaani yamepungua kabisa.
Nakushukuru ,na nitazidi kukuombea kazi hii unayoifanya Mungu azidi kukubariki
Asante Peter kwa hali hii niliyo nayo,nasema asante Yesu.
Nakutakia jumapili njema
6. BWANA YESU ASIFIWE, MTUMISHI. namshukuru Mungu aliyemponya mke wangu kupitia maombi yako! mtumishi naomba uniombee nipate kazi/ajira kwani tangu nilipomaliza chuo cha ualimu mwaka 2015. sijapata kazi yeyote na nimehangaika sana kutafuta shule binafsi lakini nimekosa. tafadhari naomba unisaidie kwani nina hali ngumu sana hadi watu wananicheka. hata sijui tatizo ni nini? .
7. Shalom mtumishi.
MUNGU ni mwemwa sana. nafurahia masomo mazur sana unayofundisha kwa kweli. hasa masomo yanayohusu maombi kwa kweli niljaribu kuomba sawasawa na neno, yaani niliona mpenyo wa ajabu ambao unaambatana na ushindi mkuu. YESU KRISTO AMBAYE NI MUNGU mwenye nguvu sawasawa na ISAYA 9:6 huyu YESU azidi kukuinua sana ili tupate kuelewa na maandiko. barkiwa sana mtumishi.
8. Mtumishi Mabula namshukuru Mungu kwa maomb yako mtumish,mume wangu amerud usiku wa jumamosi usiku baada ya kutelekeza familia kwa miezi mingi.
9. Mtumishi ni Mimi Uliniombea Wiki Iliyopita sikumbuki Ilikua Juma ngapi Na Uliomba Juu Ya Ndoa yangu Maana ilikuwa imefikia Hatua nikarudi nyumbani Na Watoto, Nina miezi Minne Sasa Mawasiliano Na mme wangu Hayakuwa vizuri lakini Leo Namshukuru Mungu Kwasababu Jana Alinitumia Kifurushi Cha Sms Na Leo Mchana Huu Katuma meseji Anajiandaa Kuja Siku Yoyote Yupo Kahama Mi Niko Magu akasema "Nataka Nije nyumbani" Hajawahi Kusema Anakuja zaidi alikuwa Anasalimia Watoto Wake Tu basi Namshukuru Sana Mungu Kwa Sababu Ametenda Muujiza Na Naomba mtumishi Uzidi Kuniombea Hiyo Satfar Yake Ya Kuja Kutufuata Huku Isiwe Na Vizuizi Vya shetani
10. Mtumish Bwana YESU Asifiwe nimatumaini yangu kwamba umzima unaendelea kuelimisha jamii, MUNGU akutie nguvu. hali ya mwanangu imekuwa nzuri na sasa ni mzima mwili wake hauweki tena vifunza, na mjukuu wangu anaendelea vizuri mtumishi, kinachonisumbua kwa sasa ni mume wangu ambaye bado hajamkiri YESU ni mwislam naomba unisaidie hiyo roho iyeyuke kwa maana nampenda sana sitaki abaki kwenye uislamu.
Ahsante mtumish barikiwa sana.

Comments