SHUHUDA MBALIMBALI.


SHUHUDA MBALIMBALI.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Hapa chini ni baadhi ya shuhuda mbalimbali ambazo baadhi ya marafiki zangu walinitumia.
Shuhuda hizi baadhi ni kutokana na Maombi na baadhi zinatokana na Mafundisho ya Neno la MUNGU.
Sifa, heshima na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni.
1. Bwana YESU asifiwe Mchungaji, Ninaungana na wezangu nashukuru kwa lile somo ulilofundisha la SILAHA ZA KIROHO ZA KIMAOMBI ZA VITA YA KIROHO hasa juu kutumia upanga wa YESU kweli nimemuona MUNGU akitenda kazi kwangu nashukuru Sana mtumishi nafurahi sana sana, kwa kweli somo hili nimelisoma na nimeelewa mno. Tena siku hizi nikiwa nasoma mafundisho kuna mabadiliko makubwa nayapata hata siwezi kuelezea Mchungaji,najikuta muda mwingi nataka niendelee na maombi tu. Nashukuru mno Mchungaji Kwa kweli MUNGU amenifanyia maajabu sana, Nina amani mno na mambo madogo madogo hayaniumizi Tena Kama kipindi kilchopita.
Ninashukuru sana. MUNGU akubariki Mtumishi.
2. Mtumishi Ubarikiwe sana.
Mimi binafsi ni derava wa malori , kwa sasa niko Congo, mafundisho mengi nayapata kwako nikiwa katika safari najiona kama wengine ambao huhudhuria ibada.
Mungu akubariki sana kwa Mafundisho mbalimbali.
3. Bwana Yesu asifiwe Mtumishi Wa Mungu! Mimi na familia yangu tunamshukuru Mungu kwa kupata masomo ya kweli ya neno la Mungu kwenye kurasa zako za Facebook. Tunamshukuru Mungu kwa kukufunulia kweli yake na kukuwezesha kutufundisha kwa uwezo Wa Roho Mtakatifu. Hakika tumebarikiwa na kukua kiroho.
Mungu akubariki, akulinde na akutetee. Aipe kibali huduma aliyoiweka ndani mwako, akuinue utukufu hadi utukufu. Amina!
4. Bwana apewe sifa Mtumishi, somo hili AINA TATU ZA MAJARIBU limenigusa Sana, nimeelewa Sana aina tatu za majaribu. Hii aina ya tatu jaribu Kama kipimo Cha Mungu nimelishuhudia Jana tarehe 24/10/2019. Nilikuwa na katafrija kadogo ka zawadi kwa mdogo wangu ambae anafunga ndoa siku inayofuata. siku hii ilikuwa na mvua kubwa mno kiasi kwamba ilikuwa shida Sana kwa wapishi ila Mungu alibariki wapishi walikuwa bega kwa bega,na baadae mvua ilikata kabisa na kwa kweli katafrija kalikuwa kazuri mno. Kitu kilichonishangaza Ni jinsi mvua ilivyokuwa inanyesha maji yalivyokuwa yanapita lakini Moto uliendelea kuwaka na tukapika na mvua. Kwa kweli Mtumishi nimeuona utukufu wa Mungu. Ninashkuru Sana na huwa ukitoa somo Mchungaji linaendana na Mimi kwa wakati huo na pale ndipo imani inaongezeka kwa Sana. Nashukuru sana Mchungaji.
5. Bwana Yesu asifiwe, apewe sifa, nakushukuru sana kuhusu somo la maombi kwa kutumia upanga kuna kitu kilikuwa kinanitatiza sana, yaani nikiota ndoto nikiamka asubuh siikumbuki, halafu nikiwa nasali ufahamu wangu unatoka najikuta naongea vitu vingine kabisa, nikaamua nichapishe maombi na niyatumie kwenye maombi, bado naomba, nasoma ufahamu wangu unaondoka nakuta nasoma mambo mengine kabsa hayahusiani, nikaingia semina siku 40 kufunga na maombi hadi 18/10 wapi hali inaondoka inarudi ila juzi ndo nikaona maombi kutumia upanga.
Nikajiandaa kwa maombi vizuri tu nikasoma neno lile nikasema "sasa naushika upanga wa Mungu ukatao kuwili nafyeka maroho machafu yote yanayoshikilia ufahamu wangu, yanayoshikilia malango yangu ya ndoto, uchumi wangu, ndoa yangu, kazi yangu, uzao wangu, nyumba yangu kila cha kwangu" nikataja nikafyeka kwa hasira kama wapo mbele yangu nikafyeka, fyeka, fyeka, katakata, maroho machafu kama ni ya uchawi, uganga, nguvu za miungu, mizimu kila kitu nikataja mpaka nikajiona hooi, FYEKELEA MBALI KWA UPANGA, KISHA NIKASEMA "NAWEKA UPANGA KAZINI, DUKANI, NYUMBA UZUNGUUKE PANDE ZOTE CHA KUZIMU CHOCHOTE KIKIJA KIFYEKWE"
Yaani Mtumishi wangu huwezi kuamini nimelala nimeota ndoto kama zote na zote nazikumbuka na ufahamu wango upo vizuri tangia jana hadi leo niko poa.
Kuna kampuni moja niliwahi kufanya kazi kuna dada alikuja nikamfundisha kazi miaka kama 20 imepita sasa baada ya miaka michache akapanda mshahara mara 3 Zaidi yangu na akapanda na cheo na elimu yake ilikuwa ndogo, sikuelewa ila jana ndo nimeota nimeenda pale ofisini yeye bado yupo hapo hapo hadi leo nimeenda kuchukua viatu vyangu, na nakumbuka kuna viatu vyangu alikuwa anavipenda akaniomba nimpe nikampa ndo Napata ufunuo kuwa alichukua hatua zangu, ashukuriwe Bwana Yesu nimekombolewa kwenye gereza la mganga wa huyo dada.
Mtumishi asante sana Mungu azidi kukubariki, Mungu azidi kukufunulia maombi mbali mbali, Mungu akupiganie pamoja na familia yako, kusiwepo na atakaye simama mbele ya huduma yako akutane na upanga ukatao kuwili.
6. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Nashukuru sana kwa maombi yako mke wangu sasa hivi amepona kabisa anaendelea nashughuli zake kama kawaida,jina la Bwana libarikiwe sana
7. Pastor Mabula ninajua mambo mengi Mungu hakufichi.
Mtoto wangu alipotea muda mrefu nikawa na hofu kuu na simu haikupatikana, niliwaza siku nyingi amefichwa wapi? Nikaamua kukushirikisha, yaani Pastor Mtoto wangu John Adego amepatikana akiwa hai. Asante kwa kusimama nami katika maombi.
Anasema waajiri wake walimtesa kwa kumnyima mshahara.
Akachanganyikiwa nakuanza kuota ndoto mbaya. Mungu amenipa wimbo mpya wa furaha. Jane Koimburi wa Kenya.
8. Jambo baba!
Nakujulisha kwa furaha kubwa ya kwamba mchumba Wangu alifika Kuleta Mali kwa wazazi jana jioni, ilikuwa furaha kubwa! Ninakushukuru kwa maombi yako, namshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi zake kwetu. Ndoa Inapangwa mwezi wa kumi na mbili. Asante sana tena sana kwa kunisaidia kwa njia ya maombi baba yetu.
9. Bwana Yesu atukunzwe! Namshukuru Mungu wa mbinguni kwa kujibu ombi langu la kupata mtoto katika ndoa yangu nakumbuka kuna siku uliniambia Mungu atakushindia na utakuwa na uzao bora sana nimekuwa nikifunga na kuomba
Mara kwa Mara na wewe ukiniombea nilitaka kusubiri mpaka mtoto azaliwe ndo nishuhudie lakini moyoni napata msukumo wa kushuhudia maana mpaka sasa Mke wangu ni mjamzito wa takribani miez mitatu sasa.
Sifa, Heshima na Utukufu namrudishia Mungu Baba naamini atatufunika na kutulinda kwa damu ya Yesu Kristo.
10. Mtumishi Mabula, Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!
Ninajua kwamba utawaombea kidato cha nne katika mtihani wa Taifa. Naomba pia mtaje binti yangu afaulu mitihani hiyo pia. Nashukuru kwa kumwombea aondokane na woga hofu na kweli imeondoka. Mtumishi namshukuru sana Mungu kwa ajili yako na kwa mafundisho ya injili unayotoa kwenye Facebook yananisaidia sana. Pia katika sala zangu nakuombea pia ili Injili zienee zaidi hadi iwafikie hasa kwa wale bado kufikiwa na Injili.
Ubarikiwe sana mtumishi.
11. Shalom Mtumishi wa MUNGU.
Mtumishi Mungu akubariki sana kwa maombi yako, nimejifungua niko salama na mtoto yuko salama.
Ni mimi Rahabu.

Comments