SHUHUDA SABA(7) MBALIMBALI.

SHUHUDA SABA(7) MBALIMBALI.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu wote.
Hapa chini ni baadhi ya shuhuda ambazo baadhi ya rafiki zangu wamenitumia.
Namshukuru MUNGU Baba wa mbinguni Kwa miujiza hii.
Shuhuda hizi zinatokana na maombi na zingine zinatokana na masomo ya Neno la MUNGU.
Sifa na utukufu wote ni kwa Bwana YESU KRISTO Mtenda miujiza maana ndiye aliyetenda.

1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi. namshkuru Mungu amenitetea nimejifungua salama kawaida na nmepata Mtoto wa kike. Nilikuwa na wasiwasi mno, nakushukuru Kwa maombi yako yalinitia Nguvu.
Endelea kuniweka kwenye maombi shetani anyamaze kimya wakati huu ambao niko kwenye uzazi na siku zote. Jina la Bwana wetu Yesu kristo lihimidiwe milele na milele.
2. Tunakuombea Safari njema Mchungaji, tunashukuru Sana kwa maombi.
Binafsi mambo mengi uliyoniombea namshukuru Sana Mungu yanakwenda vizuri, Sasa hivi Nina amani Mchungaji nashukuru Sana, ukirudi nitaomba tufanye maombi zaidi ya kuvunja nguvu.Nakutakia Safari njema Mchungaji,tuko pamoja.
3. Bwana YESU KRISTO asifiwe mtumishi wa MUNGU nashukuru sana kwa somo hili (MAOMBI YA KUMILIKI MILANGO YA BARAKA AMBAYO ALIKIWA AMEISHIKILIA ADUI.)
Kwa kuwa nimeona maajabu ya MUNGU na kufunguliwa jana nilikuwa nimelala usiku sana nane nikajisikia msukumo flani ukiniambia niamuke nisome hili somo kweli niliamuka na kulisoma kwa makini kabisa nilipofika kwenye maombi nilijipata nalia nikaamuka kitandani nikapiga magoti na nikaendelea kuomba huku bado nalia kumaliza Amen nilisikia kama vitu vinafunguliwa kwa Tumbo nilijipata nasema tu asante YESU kwa muda mrefu na kisha nikajipata nimeacha kulia.
4. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI. KWEL MUNGU NI MKUU HATIMAYE MZEE WETU PHILLMON ANANAFU AMETOLEWA MASHINE AMBAYO ILIKUWA INAMSAIDIA KUPUMUA, IMEONDOLEWA NA AMEKUNYWA KIKOMBE CHA UJI ASUBUHI YA LEO. NASHUKURU SANA KWA MAOMBI YENU.
MUNGU WA MBINGUN NA AZIDI KUWATUMIA AMINA BARIKIWA SANA.
5. Nashukuru sana mtumishi wa BWANA maana umeniombea nimeshinda ile vita maana ni vita vya kiroho ilikuwa kubwa sana.
Ila namshukuru sana KRISTO YESU kwa ajili yako, wewe ni mtu wa maana sana kwangu! Uzidi kubarikiwa na kuinuliwa ndugu yangu
6. Bwana Yesu asifiwe.
Mungu akubariki mtumishi masomo unayotoa hakika yamenipigisha hatua kiroho hakika anaesema si wewe bali ni Mungu mwenyewe kupitia wewe Mtenda kazi wake. ubarikiwe, Mungu akupe mafunuo zaidi juu ya silaha za kutumia katika vita kiroho,nangoja kwa hamu muendelezo wa somo,barikiwa, mimi nimeokoka namtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji pia ni mwinjilisti niko Bukoba Kagera.
Mungu ni mwema, ubarikiwe.
7. Halleluya mtumishi wa MUNGU.
naitwa Danieli natokea Morogoro hii sio Mara ya kwanza ya mimj kuomba msaada wa maombi kwako,
Nimekuwa nikiona msaada mkubwa sana kwa BWANA kwa ajili ya maombi yako unayoniombea.
Namshukuru sana MUNGU kwa kuniungsnisha na wewe.
MUNGU akubariki sana ndugu.

Comments