SHUHUDA.
1. Tumsifu Yesu Kristo pole na majukumu Mtumishi namshukuru Mungu kupitia yale maombi unayoweka kwenye mtandao yamefungua vitu vitu vingi kwenye familia yetu na ukoo pia vifungo vya kichawi vimemtesa sana mzee baada ya kuomba yale maombi ya kuvunja mafundo ya uchawi yule mchawi aliyemfunga baba yangu akajitokeza.
Mungu akubariki sana pia naomba uniombee nipate ajira serikalini

2. Mtumishi shaloom, Bwana YESU! Asifiwe sana! Nimeoa mwaka 2017
ila mpaka sasa nakaribia kujuta kuoa! Mama mkwe hanipi kukaa na mke wangu leo nina siku 97 toka mama mkwe aje kumchukua mke wangu na nikitaka kwenda kumfuata wanapanga kunipiga,nikituma wazee wana wachenga mpaka wazee wanarudi! Naomba msaada waKIMUNGU wa maombi!
Mimi nilioa kwa taratibu zote za kikanisa. Toka mwezi wa 8 wakwe zangu na mke wangu wote wameacha kanisa wamekuwa wapagani.
Hata mke wangu amejifungua siku ya Christmas nikitaka kwenda niwaone sisemeshwi.
Nahitaji maombi yako Mtumishi.
*Baada ya maombezi, siku chache baadae akanitumia ujumbe huu.*
Shaloom Mtumishi, Bwana YESU Asifiwe daima!
MUNGU ni mwema zaidi,hakika naona mwelekeo, jumatatu tumekubaliwa tukazungumze huko kwa wakwe ili niweze kuungana na familia yangu tena! Akhsante kwa maombi,naomba tena uzidishe ili tushinde na zaidi yakushinda na jina la Bwana lihimidiwe!
*Maombi yakaendelea, na siku chache baadae akaniandikia ujumbe huu*
Shaloom mtumishi, Bwana YESU asifiwe!
MUNGU ni mwema! Pamoja na mazungumzo kufanyika kimila jumatatu! Na kuonekana bado sina makosa,nilipigwa faini 250 elfu na nilikubali;ilihitajika jumatano ili nipewe mke wangu,lakini baada ya kuondoka wazee waliongea na wakwe zangu nakuwaambia msile dhuluma maana kijana hajawakosea chochote,jumanne nikapigiwa simu kuwa jumatano uje uwachukue familia yako na usilete chochote.
Hivyo jumatano jioni nilipewa mke wangu na sasahivi nipo nae na kila hila za mamamkwe zilikemewa kabisa!
Hivyo basi MUNGU akulipe wewe pamoja na wale wote waliofunga,wakakesha,kwa kusali na kuomba na kushukuru.
Na ahimidiwe MUNGU ajibubuye maombi milele! Amina
3. *Baada ya Leo kufundisha somo lisemalo WASAIDIE WATU KUTOKANA NA ULICHOFUNULIWA NA MUNGU JUU YAO rafiki yangu mmoja akaniandikia hivi*
Mtumishi mwaka 2017 mwezi wa Sita Dada yangu aliota katika ndoto kuwa mdogo wangu WA kiume amezungukwa na vijana watatu wakamchoma kisu na kufa aliwaambia Dada na Kaka zangu Habari za ndoto hiyo lakini walimpuuza na kumwambia kuwa ndoto za ajabu ajabu wao hawataki.
Aliota ndoto hiyo siku tatu uku akilia maana ilikuwa ndoto yenye kusikitisha.
Atimaye mwezi wa tisa 2017 mdogo wangu aitwae Julius majira ya saa nne usiku maeneo ya kigamboni alivamiwa na vibaka alipigana nao baada ya kuzidiwa nguvu walimchoma kisu cha Kifuani karibu na moyo usiku huo huo alifariki.
Ni story yenye kuumiza sana kwangu Nina weza kuandika adi kitabu.
Nikamjibu hivi
*Pole sana, baadhi ya ndoto ni taarifa ya rohoni inayotakiwa kufanyiwa kazi na sio kupuuzwa."

SHUHUDA MBALIMBALI.
Hizi ni baadhi ya shuhuda walizonitumia baadhi ya marafiki ambao ninaomba nao kwa simu, nakuletea shuhuda hizi kama walivyonitumia.
1. Bwana Yesu Apewe Sifa Mtumishi,Namshukru Mungu kupitia maombi yako nauona Utukufu Wake juu ya Mguu na Mkono wa kulia hali iliyokuwepo haipo tena. Nakushukru Sana na naomba uzidi niombea nizidi kuishi maisha Matakatifu ya Kumpendeza Mungu. Huwa naona kusudi kubwa juu ya kukutana nawe katika facebook.
Naomba uzidi niombea juu maisha yangu mwaka huu ,Juu ya kuinuka Kiroho, Mungu kubadilisha maisha yangu kiuchumi uinuke na nimpate mke ambaye Mungu amekusudia awe mke wangu.
Ubarikiwe sana.
2. BWANA YESU ASIFIWE MTUMISHI WA MUNGU.
MTUMISHI YULE MCHAWI WA KULE KIJIJINI ALIYENENA MANENO YA MIMI KWAMBA SITAOLEWA ANAUMWA SANA BAADA YA YALE MAOMBI,PIA SHANGAZI YANGU YULE AMBAE NILIKUAMBIA KUWA NA YEYE ANA ROHO YA USHIRIKINA, NA YEYE ALIUMWA AKAWA ANAMWAMBIA MAMA YANGU KWAMBA MIMI SIJAWAHI KUMNENEA MTOTO YEYOTE WA MTU MABAYA, MIMI NIKAMWAMBIA WEWE MWACHE ATASEMA YOTE, MAANA MUNGU NI MUNGU NA ATABAKI KUWA MUNGU MILELE YOTE, HATA WANGEKUSANYIKA WAGANGA WOTE WA DUNIA HII HAWATAWEZA MAANA WAKATI WA MUNGU UKIFIKA WATASARENDA WOTE, MAANA BWANA WA MAJESHI,MFALME WA WA FALME, AMIRIJESHI MKUU AMETAMALAKI.
UBARIKIWE SANA MTUMISHI.
3. Bwana Yesu asifiwe,
Mimi naendelea vizuri,
Niko na kundi moja tusoma Biblia nimefika Timotheo, sasa kila ninavyozidi kusoma Biblia nafunguliwa mambo mengi sana mpaka kuonyeshwa na kuambiwa pia ,
Namshukuru Mungu kwa haya yanayoendelea kuonekana kwangu
Kweli jina la Yesu na damu yake ndiyo ndiyo suluhisho kwa maisha yangu,
Naona kwa macho yangu matendo makuu ya Mungu kwangu,sasa watu wao wananiogopa hadi wanasema siku hizi mwl aachani na Biblia anaona kila mchawi ,wakitoka kwenye vikao vyao wajitoa wengine wanakuja kusema,nami nawajibu mwache Mungu aitwe Mungu fanyeni mwezavyo ipo siku nanyi mtajua kuwa mmepotea mtarudi upande wangu nilipo mtatembea na Biblia kama Mimi,yaani wanashangaa wanasema ungelikufa ili watese mtoto wako,nawauliza yote haya mnafaida gani,wanacheka wanasema shukuru huyo Mungu wako endelea kumshikilia,kama ni mganga huyu umemtoa mbali tusaidie nasisi na wauliza mbona amsemi niwasaidie huyu Mungu kwangu,wanasema nawadanganya,
Kwa kweli ninafurahia hali hii ya kutembea na Yesu katika maisha yangu.
Nilifurahi nikaona ni vema nikueleze na wewe pia furaha niliyo nayo maana huwa unaniombea.
Mungu akubariki sana endelea kutufundisha neno la Mungu na endelea kuniombea.
Peter ungelikuwa karibu nina mengi ningelikuhadithia umenitoa mbali nilikuwa wa kulia kila iitwapo Leo sina raha hata amani,
Asante Yesu
Asante Peter kwa kunionyesha njia.
Nami Leo naongea mbele za watu nacheka ,natafutwa naulizwa,Mungu ni Mkuu hakika.
4. SHALOM PASTOR
Ninalo jambo la kumshukuru Mungu kwakuwa nimepata neema ya kuufikia mwezi mpya pili.
Mwezi wa kwanza ulikua mwezi wa baraka sana kwangu.
Nimemuona Mungu akinivusha katika magumu na kuninawirisha.
Mengi niliyokua najiuliza nitapitaje katika hili niliyafanikisha kwa njia rahisi sana.
Ni kiu yangu kuona February inakua ya mafanikio zaidi, Ninatamani kumuona Mungu akinifanyia mambo makubwa zaidi ya niliyowahi kuyashuhudia.
Ninamshukuru sana Mungu, kwa sala na maombi yenu nimepita Januari bila vikwazo.
Ninakushukuru sana Mchungaji kwa jinsi unavyojitoa kwangu na kwa wengine Mungu akubariki sana wewe na familia yako, ndani ya mwezi huu na kuendelea ukastawi na kuongezeka zaidi na zaidi katika huduma na maisha yako ya kila siku.
BARIKIWA SANA MTUMISHI WA MUNGU.

Comments