TIMIZA WITO WAKO KWA KRISTO.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU la uzima.

◼️Kama wewe umeokolewa na Bwana YESU KRISTO na unaishi maisha matakatifu basi inakupsa kutimiza wito wako katika MUNGU.

Wito ni nini?

✔️✔️Wito ni tendo la kumsikia MUNGU au kumuona YESU KRISTO akitoa majukumu ya utumishi fulani kwako.

Kutoka 3:10 "Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri."

✓✓Musa alipokea wito kwa kuisikia sauti ya MUNGU ikimtaka aende Misri kuwatoa Waisraeli kutoka utumwani.

Je wito wako ni nini katika kazi ya MUNGU?

✔️✔️ Wito ni hali ya kuitwa na MUNGU ili umtumikie katika KRISTO YESU.

Mathayo 4:18-19 " Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu."

✓✓✓Akina Petro waliitwa na YESU KRISTO ili wamtumikie.

Je mbona wewe umeitwa na KRISTO lakini kazi yako ni kua kazi ya MUNGU na sio kuiendeleza?

Je unaujua wito wako kwa KRISTO?

✔️✔️ Wito ni taarifa ya rohoni unayoipata ikikutaka au kukujulisha umtumikie MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi au taarifa ikikupa maelekezo ya kiroho.

Yeremia 1:4-5 " Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa."

✔️✔️Wito ni mwaliko wa kiroho unaopewa na MUNGU kwa njia ya ROHO MTAKATIFU ili ujitambue na utambue unatakiwa ufanye nini katika kazi ya injili ya KRISTO.

1 Wafalme 17:2-3 "Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani."

Mambo ya kujua kuhusu Wito ulioitiwa.

1. Wito wa MUNGU ni katika KRISTO YESU pekee.

Wafilipi 3:14 "nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa MUNGU katika KRISTO YESU."

✓✓Wito sahihi ni katika kweli ya MUNGU tu ambayo ni MUNGU Baba, YESU KRISTO na ROHO MTAKATIFU.

Pia wito ni katika imani ya Wokovu wa KRISTO tu.

Waefeso 4:4-5 "Mwili mmoja, na ROHO mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana(YESU) mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. MUNGU mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote."

2. MUNGU anaweza kukujulisha wito aliokuitia kwa njia nyingi, baadhi ya njia ni hizi.

A. Kwa njia ya Malaika(Kutoka 3:16)

B. Kwa njia ya ndoto(Mathayo 2:13)

C. Kwa njia ya maono(Matendo 10:17)

D. Kwa njia ya watumishi wengine kukujulisha.

E. Kwa njia ya ufunuo wa ROHO MTAKATIFU wa moja kwa moja kupitia utu wa ndani na macho ya rohoni.

1 Wakorintho 2:10-11 " Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya MUNGU hakuna ayafahamuye ila ROHO wa MUNGU."

3. Wito wa MUNGU hauangalii hali yako kiuchumi, wito hauangalii elimu yako wala wito wa MUNGU hauangalii hadhi yako katika jamii.

Amosi 7:14-15 "Ndipo Amosii akajibu akamwambia Amazia, Mimi sikuwa nabii, wala sikuwa mwana wa nabii; bali nalikuwa mchungaji, na mtunza mikuyu; naye BWANA akanitwaa, katika kufuatana na kundi; BWANA akaniambia, Enenda uwatabirie watu wangu Israeli."

1 Wakorintho 1:26 "Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;"

4. Wito wako unahitaji sana uendelee kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.

Wagalatia 5:16 "Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na  whatsapp).
Ubarikiwe sana.

Comments