USHUHUDA WANGU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Kipekee namshukuru sana MUNGU Baba wa mbinguni kwa kunipa neema hii ya kuishi na kumtumikia katika KRISTO YESU Mwokozi.
Ushuhuda wangu wa leo ni kuhusu neema ambayo MUNGU amenipa hata baadhi ya masomo yangu kuwekwa magazetini na kusomwa na watu wengi.
Kuna kipindi kuna gazeti Moja la KRISTO lilikuwa linaweka gazetini mfululizo masomo yangu kwa zaidi ya miezi 3, kwangu huo ni ushuhuda wa mbinguni.
Baadae kuna gazeti lingine nalo likaongezeka na kuwa linaweka gazetini masomo yangu kila wiki kwa muda mrefu(hata picha za post hii ni kutoka gazeti hilo), kwangu huo ni ushuhuda wa mbinguni.
Tena huduma hiyo inaendelea, kwangu huo ni ushuhuda wa mbinguni.
Baadae tena kuna gazeti tena hili wala haliandikwi mambo ya dini bali huandikwa tu masuala ya siasa na michezo lakini kwa neema ya ajabu sana wakanipigia simu wenyewe na kuniomba somo langu moja liwekwe gazetini kwao katika siku ambazo wana vipengele vya dini, kwangu huo ni muujiza wa mbinguni.
Magazeti haya sio magazeti ya mitandaoni bali ni magazeti ambayo mtu popote Tanzania anaenda kwenye mabanda ya kuuzia magazeti na ananunua gazeti la siku hiyo, kwa somo langu kuwapo katika moja ya magazeti, kwangu huo ni muujiza wa mbinguni.
Mimi nimrudishie nini MUNGU Baba kwa wema na fadhili zake alizonitendea?
Zaburi 23:6 "Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele."
Kwanini nasema "Huu ni muujiza wa mbinguni?"
Ni kwa sababu mimi ni nani hata nipate nafasi hiyo gazetini?
Magazeti huuzwa nchi nzima na kuweka ujumbe wako hapo sio Kazi rahisi ni gharama kubwa na kibali, ndio maana nikasema kwangu huu ni muujiza wa mbinguni.
Kuna Baba zangu Maaskofu wangapi hata nipate neema Mimi?
Kuna Baba zangu Wachungaji wangapi Tanzania hata nipate neema mimi?
Maaskofu na Watumishi wengine wanaoifanya kazi kubwa ya Injili na Wachungaji walio Watumishi halisi wa Bwana YESU KRISTO mimi huwa nawaita Baba zangu.
Kuna watumishi hai wa Bwana YESU wangapi wenye vibali, wenye Neno safi la KRISTO, wenye huduma kubwa hata neema hii iwe kwangu?
Sijatumia hata Tsh 100 kuchapishwa somo langu gazetini bali neema ya MUNGU tu.
Yaani mtu mkuu mwenye hadhi yake akupigie simu akikuomba uruhusu gazeti lao pendwa lichapishe somo lako, huu ni muujiza wa mbinguni tu.
Miaka kama mitatu nyuma niliona tangazo kwenye gazeti moja likionyesha kinafasi kidogo ambacho kiko wazi kwa yeyote kwa matangazo au Neno kwa ufupi, nilipoulizia niliambiwa bei ni Tsh laki 2 kila wiki, nikajisemea moyoni kwamba kazi hii niwaachie watumishi wa MUNGU ambao MUNGU awewainua kwa wakati huu.
Nini matokeo ya huduma hii ya masomo yangu kuwekwa magazetini?
Nimepigiwa simu nyingi na Watu wengi kutoka maeneo ambayo hata sikutarajia wakisema wamesoma masomo yangu gazetini.
Nimepata mialiko ya kwenda kuhubiri hadi nikashangaa.
Mchungaji mmoja akaniambia niende mkoani kwake nikawe mgeni rasmi na mhubiri nikizindua tawi jipya la Kanisa lao.
Nilipata mshangao mkubwa na nikakosa hata majibu sahihi ya kumweleza Mtumishi huyo wa MUNGU.
Kuna hadi dada mmoja yuko Katavi aliniambia atanitumia Tsh 6,000 ili niongezee nichapishe kitabu kabisa kutoka katika masomo yangu aliyoyaona na kuyasoma, huu ni muujiza wa mbinguni.
Nimemshagaa MUNGU kwa miujiza hii kwangu. Sifa, heshima, adhama na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba juu mbinguni.
Nimejikuta nakumbuka andiko moja ambalo MUNGU alisema nami mara nyingi sana zaidi ya miaka 9 iliyopita.
Andiko hilo ni hili.
Yeremia 31:16 "BWANA asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo BWANA."
Kwa andiko hili nilisemeshwa zaidi hata ya mara 10 hadi kwenye Biblia yangu nikaweka alama, sikuelewa neno hili lina maana gani kwangu hadi nilikuja kuelewa baada ya kuona matokeo.
Mfano hao ni huu, katika utumishi wangu mtandaoni nimeongoza sala ya toba watu wengi, baadhi yao ni ambao wako katika nchi ambazo Ukristo hauko au hauruhusiwi.
Watu hawa baada ya kufunguliwa kupitia masomo yangu hadi wakaamua kufanyika Wakristo wa siri, yaani ingawa nchi zao ni marufuku kuwa mkristo, ni marufuku kuwa na Biblia lakini wao wamemchagua YESU KRISTO kwa ajili ya uzima wa milele. Hivyo wanajifunza Neno la MUNGU mtandaoni na wanafuata mafundisho ya KRISTO mtandaoni. Nakubaliana na mhubiri mmoja wa Marekani ambaye siku moja alisema kwamba kwa utafiti wamegundua kuwa kuna Wakristo wa siri zaidi milioni 120 katika nchi ambazo Ukristo unakatazwa, hata mimi nimeongoza sala ya toba watu zaidi ya 10 kutoka katika kundi hilo.
Haya ni sehemu ya majibu ya kile ambacho nilisemeshwa mara nyingi bila kuelewa, lakini kitendo cha watu wa magazeti labda kukaa vikao na kupitisha masomo yangu kuwekwa bure kwenye magazeti yao ni neema ya MUNGU tu na ni muujiza wa mbinguni huu.
Kama yuko mhusika wa magazeti hayo anayesoma ujumbe wangu huu napenda kumwambia hivi ;
"Ninyi ni watumishi wa MUNGU, matokeo mazuri yanayotokana na Neno la MUNGU, matokeo hayo mkutane nayo katika maisha yenu. Bwana YESU awakumbuke na kuwalinda na kuwabariki.
MUNGU awape miaka mingi ya kuishi duniani.
MUNGU awape neema ya Wokovu wa KRISTO YESU ili mkutane na thawabu ya MUNGU kutokana na kazi yenu ya kuisambaza injili ya KRISTO hata watu wakafunguliwa na Kuokoka"
Mimi binafsi namtukuza sana Bwana YESU maana ni kwa neema yake tu na upendo wa MUNGU Baba na ushirika wa ROHO MTAKATIFU ndio maana imekuwa hivi.
Ninachoweza kusema cha mwisho ni hiki.
Mbingu zinavyoonekana tu zinahubiri utukufu wa MUNGU, Anga linavyoonekana tu linatangaza kazi za mikono ya MUNGU.
Ninakushukuru sana MUNGU Baba kwa upendo wako mkuu kwangu na kwa wanadamu wote.
Ninakushukuru sana Bwana YESU kwa neema yako ya ajabu sana kwangu na kwa ndugu zangu, jina lako lina ushindi wa ajabu kwa kila aaminiye.
Asante ROHO MTAKATIFU kwa wewe kuwa Mwalimu na kiongozi wangu.
Hakika hii ni AMAZING GRACE.
MUNGU awabariki sana wote.
By Peter Michael Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Comments