![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
✓✓Uzinzi na uasherati huwapeleka watu jehanamu.
✓✓Ni kuamua tu kuacha uzinzi na uasherati kama kweli unaitaka mbingu.
Yakobo 4:4 "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU."
◼️Uzinzi na uasherati wala hauhitaji maombi hata mtu aombewe kuacha uzinzi bali kuacha uzinzi ni maamuzi tu ya kuikataa jehanamu ili uipate mbingu ukiwa na KRISTO YESU.
◼️Nakushauri Ndugu Amua kuacha uzinzi na utaweza, vunja urafiki na uliwahi kufanya nao uzinzi wenye ukaribu na wewe.
◼️Futa hata namba zao uliowahi kuzini nao ili wasikuangushe tena dhambini.
◼️Tumia muda wako kwa mambo ya MUNGU Na sio kuwaza uzinzi na uasherati
Kumbuka kuna jehanamu kwa wazinzi na waasherati.
Ufunuo 21:8 "Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."
Hivyo wewe Mkristo unapofanya uzinzi au uasherati ujue jina lako wala haliko katika kitabu cha uzima bali unapofanya uzinzi au uasherati ujue jina lako liko katika majina ya waenda jehanamu.
✓✓✓Toba na kuacha dhambi ya uzinzi ndio itarudishs Jina lako katika kitabu Cha Uzima.
Ndugu, nakuomba tubu haraka sana na acha uzinzi na uasherati.
Omba maombi ya toba na acha kuanzia leo huo uzinzi na uasherati.
✓✓Okoka kwa kumaanisha na sio kuigiza.
◼️YESU KRISTO hahitaji waigizaji katika Wokovu wake bali anahitaji Watu walioamua kweli kweli kaokoka.
Ndugu, unayehusika na dhambi hii ya uzinzi na uasherati nakuomba fanyia kazi Neno hili maana ni la MUNGU.
Inawezekana unajiuliza Uzinzi ni nini?
◼️Maana ya UZINZI ni kufanya mapenzi/Ngono na mtu yeyote ambaye sio Mke wako wa ndoa au sio Mume wako wa ndoa.
◼️Uzinzi ni kukutana kimwili na Mtu yeyote ambaye hujafunga naye Ndoa ya Mke mmoja tu kwa Mume mmoja tu.
Ndugu, kama unahusika na uzinzi acha kuanzia leo.
1 Wakorintho 6:9-10 " Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."
Kama huhusiki na uzinzi MUNGU akubariki sana ila wajulishe wazinzi na waasherati kwamba waache uzinzi.
Yeremia 23:10 "Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki."
✓✓Mwambie kila mtu kwamba "Wazinzi ni wengi sana ila naomba usiwe wewe maana watakaoingia Katika ziwa la moto ni pamoja na wazinzi "
Ufunuo 21:8 "Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."
Ndugu, kama unahusika na dhambi hii nakuomba tubu katika KRISTO YESU, okoka na jina lako litaandikwa katika Kitabu cha uzima mbinguni.
Usipotubu ujue ghadhabu ya MUNGU inakukalia.
Na kumbuka toba ya kweli ni kutubu na kuacha dhambi hiyo iliyokufanya utubu.
Hivyo tubia uzinzi na usiufanye tena.
Pia zingatia na hii Ndugu yangu, Kumbuka na hii unaweza kutenda mema yote unayoyafahamu lakini bila kumpa Bwana YESU maisha yako hakika huwezi kuingia katika ufalme wa MUNGU.
Matendo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
Wokovu ni Katika KRISTO YESU pekee.
NDUGU KUOKOKA NI LAZIMA KAMA UNATAKA KWENDA UZIMA WA MILELE.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, kuandika meseji na hadi whatsapp).
Ubarikiwe

Comments