VITU TISA(9) VITAKAVYOSABABISHA KUSUDI LA MUNGU LIFANYE KAZI KWAKO.

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu. 

Najua unatamani kusudi jema la MUNGU lifanye kazi  kwako. 

Najua unatamani akutumie katika kazi yake,  akubariki  na akutendee mema ya kila namna. 

Matendo y 20:27 "Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la MUNGU."

Kama kweli unatamani kusudi la MUNGU litimie kwako au lifanye kazi kwako basi  haya mambo 9 hakikisha uko nayo yote. 

1. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako  MPENDE MUNGU NA MTAFUTE  KWA BIDII. 

Mithali 8:17 "Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona."

Kumtafuta MUNGU kwa bidii ni kufanya jitihada katika kufanya mambo ya kiroho yatakayomfanya MUNGU aonekane kwa kutenda miujiza, kukutumia katika kazi yake,  kukubariki na kukupa haja ya moyo wako. 

Ayubu 8:5-7 " Wewe ukimtafuta MUNGU kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi;  Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana."

2. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako KAA KATIKA KUSUDI LA MUNGU. 

Wafilipi 2:13 "Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema."

Kukaa katika kusudi la MUNGU ni kuliishi kusudi la MUNGU kupitia Neno la MUNGU linalofunua kusudi hilo la MUNGU au kufuata maelekezo ya Neno la MUNGU yanayozungumzia kusudi hilo la MUNGU. Hayo pia ndio Mambo ambayo Mimi Peter Mabula nimejifunza na ndio Maana napata ujasiri wa kukufundisha rafiki yangu unayefuatilia masomo yangu.

3. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi  kwako  KAA NDANI YA YESU KRISTO. 

Bwana YESU mwenyewe anasema  "Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.-Yohana 15:4"

Kukaa ndani ya YESU ni kuokolewa na YESU KRISTO kisha, kuishi ndani ya Wokovu wake na   kulizingatia neno lake.

1 Yohana 2:28 "Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake."

4. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi  kwako  ISHI MAISHA MATAKATIFU YA WOKOVU WA KRISTO. 

1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"

5. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako TEMBEA KWENYE KANUNI ZA MUNGU .

Kumbu  28:-2 " Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako."

Kanuni za MUNGU ziko nyingi sana. 

Kila jambo la ki MUNGU unalolihitaji lina kanuni zake,  hizo kanuni ndio maagizo yake kama maandiko hapo juu yanavyosema.

Sauti ya MUNGU ni Neno lake la ufunuo katika ROHO MTAKATIFU na maagizo yake ni kanuni zilizo ndani ya Neno la MUNGU.

Mfano baadhi ya Kanuni za MUNGU za kuzifuata sana ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako ni maombi,  sadaka na zaka,  kumtumikia MUNGU n.k

Ili kusudi la MUNGU Lifanye kazi kwako hakikisha unajifunza Neno la MUNGU juu ya kanuni mbalimbali za MUNGU  na zizingatie sana kanuni hizo za kibiblia. 

6. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi  kwako  uwe MWAMINIFU MBELE ZA MUNGU. 

1 Wakorintho 4:1-2 " Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU.  Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu."

Mfano ni Musa ambaye alikuwa mwaminifu kwa MUNGU ndio maana kusudi la MUNGU lilifanya kazi kwa kiwango kikubwa sana Kwa Musa. 

 Hesabu 12:7-8 " Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?"

Uaminifu Kwa MUNGU hulifanya kusudi la MUNGU kufanya kazi,  ndugu ishi maisha ya uaminifu kwa MUNGU katika KRISTO YESU ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako. 

MUNGU anafanya kazi na watumishi wake walio waaminifu tu. 

1 Samweli 2:35 "Nami nit

ajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa na mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yangu; nami nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele."

Ukikosa uaminifu mbele za MUNGU kunaweza kukizuia kusudi la MUNGU kufanya kazi kwako,  hivyo hakikisha unakuwa mwaminifu kwa MUNGU katika mambo yote ndipo kusudi la  MUNGU litafanya kazi kwako. 

7. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi  kwako  MSIKILIZE ROHO MTAKATIFU NA FUATA DAIMA USHAURI WAKE KWAKO. 

 Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."

Kumsikiliza ROHO MTAKATIFU na kufuata maelekezo yake ndio kuongozwa na ROHO MTAKATIFU,  hivyo siku zote hakikisha unamsikiliza na kumfuata ROHO MTAKATIFU ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako. 

Yeye ROHO MTAKATIFU yuko tayari siku zote kukusaidia ili kusudi la MUNGU lifanye kazi kwako. 

Zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."

8.Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi  kwako   JITENGE MBALI NA DHAMBI NA JIEPUSHE NA KILA UOVU. 

1 Wathesalonike 5:22 "jitengeni na ubaya wa kila namna."

9. Ili kusudi la MUNGU lifanye kazi  kwako FANYA KAZI YA MUNGU  KWA BIDII. 

Warumi 8:28 "Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote MUNGU hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake."

Fanya kazi ya MUNGU ndipo kusudi la MUNGU la ajabu litafanya kazi kubwa sana. 

1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."

MUNGU akukumbuke na kukubariki ukizingatia Neno lake hili katika KRISTO YESU Mwokozi.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Ni namba hii  kupiga,  kuandika meseji na hadi whatsapp).

Comments