![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Hili ni Neno la MUNGU la kukupa maarifa ya kuomba na kushinda dhidi ya nguvu za giza.
Nguvu za giza na kila watendakazi wa shetani ndio maadui zetu.
Maadui hawa siku zote huhakikisha huna amani, huna furaha, hufanikiwi, hupati baraka zako, huendelei, hupati uzima wa milele, huponi n.k
Kuna namna nyingi za maombi ili kushinda nguvu za giza na kila watenda kazi wa shetani.
Leo omba maombi ya vita ukiamuru haya yaliyo katika Zaburi 6:10 yanawapata adui zako wote kutoka ulimwengu wa roho wa giza.
Zaburi 6:10 Biblia inasema "Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika."
Nini ufanye katika Maombi haya?
1. Omba Maombi kwamba adui zako waaibike na kuachana na wewe.
Zaburi 25:3 "Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu."
Kataa kuaibishwa na nguvu za giza.
Katika jina la YESU KRISTO futa kila mipango ya nguvu za giza ya kukuabisha.
✓✓Wanaweza kukufunga ili usiolewa/usioe au usipone ugonjwa, huko ni kuaibishwa, hivyo katika jina la YESU KRISTO kataa kuabishwa kipepo.
✓✓Wanaweza kuivuruga ndoa yako ili uabike, leo kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO futa kila aibu iliyopangwa kichawi ili ikupate.
✓✓Wanaweza kuwakamata kiroho watoto wako ili uabike, futa hiyo roho ya kuabishwa kipepo.
Wanaweza kufunga uchumi au kukufanyia baya lolote ili tu uabike.
Leo kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO kataa kuaibishwa na nguvu za giza, futa kuaibishwa na wakuu wa giza.
Baada ya kuomba hivyo omba ukiamuru wao ndio waabike.
Taja eneo ambalo walikuwa wamekufunga kisha amuru waabike sawasawa na Neno la MUNGU.
Neno la MUNGU hapo juu liko wazi sana kwamba
"Wataaibika watendao uhaini bila sababu."
Hivyo amuru kila watenda kazi wa shetani waabike, katika jina la YESU KRISTO wataabika na hawataendelea kukutesa tena.
MUNGU ana njia nyingi za kuwaabisha, omba waabike na wataaibika.
Wengine wanaweza kuabika kwa kushangaa kwamba eneo ambalo walikufunga sana kichawi ndilo eneo ambalo MUNGU anakupa kufanikiwa sana na kustawi.
Omba ndugu na katika jina la YESU KRISTO adui zako wote wataabika
2. Omba Maombi ya kuwafadhaisha adui zako, na watafadhaika na kukimbia.
Zaburi 48:5 "Waliona, mara wakashangaa; Wakafadhaika na kukimbia."
✓✓Omba MUNGU awafadhaishe adui zako wote wanaotoka ulimwengu wa roho wa giza.
Inawezekana wanaokufuatilia ni wengi sana lakini MUNGU ana uwezo wa kuwafedhehesha wote hata wasikufuatilie tena.
✓✓Omba MUNGU awafedheheshe wanaoiwinda kazi yako, uchumi wako, uzao wako, huduma yako, ndoa yako, uchumba wako, kibali chako, afya yako, mwili wako na kila kitu chako.
Katika jina la YESU KRISTO ukiomba maombi ya kuwafadhaisha adui zako hakika watafadhaika usiku na mchana hata watakuogopa na kukukimbia.
Kuna namna tu nyingi MUNGU anaweza kuwafadhaisha adui zako, omba katika jina la YESU KRISTO na adui zako wote watafadhaika sana na kukuogopa.
Isaya 13:8 "Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto."
3. Omba adui zako wote warudi nyuma ghafla na kushindwa kutimiza walichokipanga kuhusu wewe.
Zaburi 35:4-6 " Waaibishwe, wafedheheshwe, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.
Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa BWANA akiwaangusha chini. Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa BWANA akiwafuatia."
Maombi haya maana yake ni kwamba adui zako wasiendelee walichokusudia juu yako.
✓✓Omba warudi nyumba wanaoiwinda roho yako, ndoa yako, ufahamu wako huduma yako, mipango yako baraka zako.
Nani anapanga ufe au ndoa yako ivunjike? Omba leo katika jina la YESU KRISTO na adui huyo ataishia kurudi nyuma na kufadhaika.
Nani anapanga kuuvunja uchumba wako kichawi?
Nani anakutumia roho ya mauti na uharibifu?
Omba ndugu katika jina la YESU KRISTO ili Malaika wa MUNGU awarudishe nyuma adui zako na kuwaangusha chini na kuwafedhehesha.
Nani anakuendea kwa mganga wa kienyeji?
Omba leo katika jina la YESU KRISTO na aliyekupeleka kwa mganga na mganga mwenyewe na majini yao watarudi nyuma na kufadhaika na kupigwa na MUNGU.
Omba ndugu katika jina la YESU KRISTO.
Omba kwa Imani na utamuona MUNGU wa miujiza.
By Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments