MAOMBI YA KUFUTA UCHAWI ULIOWAHI KUFANYIKA KATIKA MAISHA YAKO.

Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la MUNGU. 




Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Tunaendelea na Maombi yetu ya kufunga. 
karibu tujifunze Neno la MUNGU kisha tuombe maombi ya ushindi katika jina la YESU KRISTO.

Maombi yetu yatahusu mambo matatu yafuatayo;

1. Maombi ya kufuta uchawi wa kutamkiwa.

● Kutamkiwa wewe binafsi.

● kutamkiwa uzao, iwe ni mababu au wazazi wako waliorogwa kwa kutamkiwa kisha uchawi huo ukakuathiri na wewe uliye sehemu ya uzao wao.
Hata vifungo na magonjwa baadhi yanaweza kutokana na uchawi hivyo tunapofuta uchawi tunakuwa tumefuta na magonjwa ya kichawi pamoja na vifungo vingine. 

2. Maombi ya kufuta uchawi uliopitishiwa kwenye vitu kuja kwenye mwili wako.

3. Maombi ya kufuta uchawi kupitia ardhi.

Kutoka 22:18 '' Usimwache mwanamke mchawi kuishi.''

Kabla ya yote naomba ujue maana ya uchawi na mchawi.

Uchawi ni nini?

●Uchawi ni ufundi wa kutumia dawa ili kuleta madhara.

Uchawi ndio usihiri, Uchawi ndio urogaji na ndio juju na ndio ushirikina.

●Kuroga maana yake ni kuzuru kwa kutumia uchawi

●Mchawi ni mtu anayeweza kuwadhuru watu  kwa njia ya kuwaroga

 Kuna watu wengi sana wameathiriwa na uchawi katika maisha yao ikiwemo kurogwa miili yao ili wateswe na magonjwa. 

Kuna watu walirogwa zamani lakini madhara ya uchawi ule yapo hadi leo katika maisha yao.

Leo tunafuta uchawi wote uliowahi kufanyika zamani kutuhusu, tunaufuta kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai. 

Tunafuta madhara ya uchawi yaliyotamkwa kutuelekea sisi, tunafuta kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu.

Biblia ikataza uchawi na inakataza mwanadamu mwenye akili timamu kuwaendea wachawi na waganga.

Walawi 19:31 '' Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.''

 MUNGU anakataza uchawi maana ni kitu kinachoweza kumnajisi mtu.

●Uchawi ni dhambi na uchawi ni uadui kwa MUNGU.
Mkristo hatakiwi kuwa mchawi.

Uchawi ni machukizo makuu.

Wachawi wapo sana na wanaroga sana lakini ashukuriwe MUNGU kwa kutupa jina la YESU KRISTO lililo kiboko ya wachawi wote na uchawi wao.

Biblia inathibitisha kwamba wachawi wapo na hutenda kazi zao mbovu za kichawi.

 Nahumu 3:4 ''Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake.''

Kuna watu wamewahi kurogwa fahamu na akili zao zamani lakini hadi sasa hawajawahi kupona vyema.

Kuna watu biashara zao zimewahi kurogwa, uchumi na vipato vyao na hawajawahi kupona katika hayo, Leo uchumi wako utapona, biashara yako itapona na kipato chako kitapona kwa jina la YESU KRISTO kupitia Maombi. 

Kuna watu wamewahi kurogwa afya zao ndio maana  hadi sasa hupona magonjwa kwa muda tu kisha magonjwa yale yanarudi, Ndugu leo kuna kupona katika jina la YESU KRISTO.

Kuna watu uzao wa tumbo zao ulirogwa na walikuja kuzaa uzao uliorogwa yaani walipata watoto waliofungwa kipepo.

Kanisa la MUNGU ni lazima lijitenge na uchawi.

Kanisa la MUNGU ni lazima likemee uchawi.

Zamani wachawi walikuwa wanauawa kwa mawe ndivyo Biblia isemavyo, Leo tunauua uchawi ndani ya wachawi kwa njia ya maombi yetu.

Leo malaika wa MUNGU wako tayari kupeleka mapigo kwa wachawi wote waliotusumbua, na kama wakiendelea na uchawi huo basi tunamuomba MUNGU  wetu awaadhibu kupitia maombi yetu na adhabu ya MUNGU itawapata wote.

Walawi 20:27 ''Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.''

MUNGU wetu yuko tayari kutushindia leo dhidi ya wachawi wote waliofunga maisha yetu.

Leo kwa jina la YESU KRISTO maisha yetu yanaenda kuwa huru.

JEHOVAH MUNGU wetu anasema  '' Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.-Malaki 3:5''

 Kuna ukoo huwa wanazika kila mwaka kwa sababu tu ya maneno ya mchawi aliyoyatamka zamani kwa ukoo ule.

Kuna watu nyoka hutembea katika miili yao.

Kuna watu fahamu zao zimefungwa katika mafundo ya uchawi.

Leo kila fundo la uchawi linapasuka kwa jina la YESU KRISTO.

Kuna watu miguu yao imerogwa kiasi kwamba hata waende wapi hawawezi kufanikiwa.

Kuna watu mikono yao imerogwa hata wafanye kazi gani hakuna kufanikiwa kiuchumi.

Biblia inasema kwamba kwa sababu hiyo ya uonevu wa shetani na wachawi wake ndio maana Bwana YESU alikuja ili tu kuziharibu kazi zote za shetani wakiwemo na wachawi.

1  Yohana 3:8 '' atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.''

 Hakikisha leo kazi zote za uchawi zilizowahi kufanyika zikikuhusu, hakika zinaharibika na kutoweka kwa jina la YESU KRISTO.

YESU KRISTO alidhihirishwa ili azivunje na kuzifuta kazi zote za shetani.

Leo futa uchawi wote uliowekewa kwenye uti wako wa mgongo.

Leo futa kwa damu ya YESU KRISTO kila uchawi ulifanyika kuhusu tumbo lako.

Leo hakikisha uso wako hautumiki tena kichawi, utakase uso wako kwa damu ya YESU KRISTO na hakikisha uchawi hauharibu kibali chako tena.

Leo ni siku ya kushinda kama ukiomba katika jina la YESU KRISTO.

Leo futa uchawi wa kutamkiwa uliowahi kutamkiwa, Futa kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.

Leo futa laana zote zilotamkwa na mchawi kwa wazazi wako au wazazi wa wazazi wako na laana hizo zimekupata na wewe,  leo Futa kwa damu ya YESU KRISTO katika  jina la YESU KRISTO.

 Leo futa uchawi wote uliowekwa kwenye vitu ili uchawi huo uupate mwili wako, futa kwa damu ya YESU KRISTO katika  jina la YESU KRISTO.

Futa uchawi wote uliotamkwa katika ardhi yeyote inayokuhusu.

Siku napata ufunuo wa somo hili nilifuta kila uchawi uliofanyika katika ardhi ambayo mimi Peter Mabula nimewahi kukanyaga, Kila mabaya yanayonena mabayo kuhusu mimi yaliyo katika ardhi ambako nimewahi kukanyaga nilifuta kwa jina la YESU KRISTO na kuachilia damu ya YESU KRISTO kwenye hiyo ardhi, nilitaja mikoa hadi wilaya maana mawakala wa shetani hutumia sana ardhi ili kuwafunga watu wa MUNGU.

Leo ni siku moja ya kushinda katika jina la YESU KRISTO kama ukiomba katika kweli, katika imani na katika utakatifu autakao MUNGU

 Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kueleea naamini  ameelewa .

Hapa chini ni MAOMBI YA KUFUTA UCHAWI ULIOWAHI KUFANYIKA KATIKA MAISHA YAKO.

Maombi haya ni kwa ajili ya mtu ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba.

Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.

■Baada ya kuomba maombi ya kutubu na kuacha dhambi omba maombi haya chini.

  MAOMBI YA KUFUTA UCHAWI ULIOWAHI KUFANYIKA KATIKA MAISHA YAKO.

 Katika jina la YESU KRISTO aliye hai.

Ninafuta kila uchawi uliotamkwa kunihusu mimi, naufuta huo uchawi na naharibu madhara yake  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila mchawi aliyenitamkia nikiwa nasikia au hata nikiwa sisikii, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.

Uchawi ulioleta magonjwa au mateso kwangu au kwa familia yangu, huo uchawi naufuta Leo katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Uchawi uliofanyika sehemu yeyote ya mwili wangu, huo uchawi naufuta katika mwili wangu katka jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila uchawi ulionenwa njia panda au dirishani mwa chumba changu, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO

 Kila neno la siri la kichawi alilolitamka mchawi wa aina yeyote kunihusu mimi, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila mchawi anayeitamkia maneno mabaya ndoa yangu, uchumba wangu, biashara yangu, uzao wangu au masomo yangu, mwili wangu Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO na naachilia damu ya YESU KRISTO katika eneo hilo aliloliloga.

Kila mchawi anayenitamkia kifo au kuumwa au ajali au kufukuzwa kazi,  Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

 Kila mchawi aliyenena uchawi kuhusu mababu zangu zamani au wazazi wangu na uchawi huo unafuatilia maisha yangu, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Ninafuta kila kazi ya wachawi iliyofanyika zamani katika uzao wa babu yangu au wazazi wangu, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai 

 Kila laana ya mchawi iliyotamkwa ili inipate, leo napangua kwa damu ya YESU KRISTO katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.

Kila majanga yaliyokusudiwa kichawi, kila balaa zilizopangwa kichawi, kila ajali zilizopangwa kichwi, leo nakataa kwa jina la YESU KRISTO na Leo naufuta uchawi huo kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

 Kila uchawi uliotegwa kwenye vyakula au nguo zangu ili nidhurike, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO na naachilia damu ya YESU KRISTO katika hivyo vyakula na nguo.

Kila uchawi nilioukanyaga aridhini na sasa unanitesa, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO na naachilia damu ya YESU KRISTO kufuta uchawi huo katika ardhi.

Kila uchawi uliowekwa kwenye  vitu nilivyonunua, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai 

Kila nguo yangu iliyoibwa kichawi leo naichoma moto kwa damu ya YESU KRISTO huko iliko na kuanzia leo hakuna antena ya mchawi itaniona.

Kila kiungo cha mwili wangu, kila kucha au nywele au nguo za ndani vilivyotumika kichawi, Leo naufuta uchawi huo kwa damu ya YESU KRISTO katika  jina la YESU KRISTO.

Kila uchawi uliowekwa katika mwili wangu, Leo naufuta uchawi huo nikiachilia  damu ya YESU KRISTO na ninaomba kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila kiungo cha mwili cha bandia kilichopandwa na wachawi ndani ya mwili wangu ili kunizuia kupata baraka fulani, Leo nakiondoa kiungo hicho feki, nakiondoa  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila uchawi uliowekwa kwenye vitu nilivyopewa kama zawadi, Leo naufuta uchawi huo kwa damu ya YESU KRISTO katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

 Kila uchawi ulitegwa katika ofisi yangu au kiti changu, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.

Sasa pia nafuta kila uchawi unaonena katika ardhi, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO na naachilia damu ya YESU KRISTO kwenye ardhi hiyo ili kufuta na kunyamazisha huo uchawi. 

Najua kabisa damu huwa haifi hivyo damu za wanyama zilizomwagwa katika ardhi zikiambatana na maneno ya laana kwangu, Nazifuta leo damu hizo kwa damu ya agano ya YESU KRISTO katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

 Kila mchanga uliowahi kuchukuliwa kwenuye nyayo zangu na ukatumika kichawi kunifunga,
Leo naufuta uchawi huo kwa damu ya YESU KRISTO katika  jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila uchawi wa aina yeyote uliofanyika popote kunihusu mimi au ndoa yangu au uzao wangu au familia yangu au ukoo wangu, Leo naufuta uchawi huo  kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

 Nakushukuru MUNGU Baba maana umenipa ushindi kupitia damu ya YESU KRISTO aliye hai.

Naamini nimeshinda katika kila eneo la Maisha yangu lililokuwa limefungwa kichawi.

Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.

Amen amen  Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen.

Hakika umeshinda. 
Endelea na maombi, chochea zaidi na utayaona  matokeo kwa maco yako katika maisha yako kuanzia leo.
Omba kwa imani.
Omba katika jina la YESU KRISTO. 
MUNGU akubariki sana. 
By Peter Mabula. 
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU Mwenyezi. 
+255714252292.
Ubarikiwe sana.

Comments