MAOMBI YA KUOMBEA AFYA.

Mwl Peter Mabula 




Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote. 

Leo tunaanza maomb yetu kwa kuombea afya.


Afya ni nini?


✓✓Afya ni hali nzuri ya mwili ya kukaa bila maradhi/Magonjwa.


Hiyo ndio maana ya afya kiroho na kimwili pia.


✓Afya sio unene.


✓Kuwa na ngozi laini ya mwili sio afya.


✓Kula sana sio afya.


Kwanini afya ni muhimu sana kwako?


✓✓Kwa sababu afya ikiondoka magonjwa yanachukua nafasi.


Afya ni jambo la kiroho hivyo usisahau kuomba kuhusu afya.


Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye."


Biblia inaposema kwamba MUNGU atakurudishia afya ina maana pia ya kwamba afya haikuwepo ndio maana kwa neema yake MUNGU anairudisha afya hiyo.


Sio kwamba ni mwili tu unahitaji afya, hapana, hata ndoa inahitaji afya,uchumba unahitaji kuwa na afya ndipo mtafikia hatua ya kufunga ndoa, n.k


 Leo Mimi nitajikita zaidi katika afya ya mwili.


✓✓Hakikisha leo unaomba maombi ya kuiita afya ndani yako, kwa familia yako, watoto wako, wazazi wako, ndugu zako, rafiki zako na watu wanaokuhusu ambao utapata msukumo kuwaombea.


✓✓Kumbuka sana afya ikiondoka ujue magonjwa yanachukua nafasi mwilini.


Biblia inaposema katika Yeremia 30:17 kwamba MUNGU atairudisha afya maana yake hiyo afya ilikuwa haipo ndio maana MUNGU anairudishwa.


Kama afya ilikuwa haipo maana yake kuna aliyeichukua.


✓✓Anayeweza kuichukua afya yako hata ukawa mtu wa kuumwaumwa ni shetani na mawakala zake,hao ndio wanaweza wakaiondoa afya ndani ya mtu na kumwekea magonjwa.


✓✓Dhambi zako pia zinaweza kuondoa afya ndani yako, ndio maana Bwana YESU baadhi ya aliowaponya aliwaambia "Umesamehewa dhambi zako"


Mathayo 9:2 "Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako."


Kumbe tunagundua kwamba dhambi ndio ilikuwa chanzo cha kuumwa kwao baadhi ya watu, hivyo  afya kuondoka ndani yao.


✓✓Kwa hiyo afya inaweza kuondoka ndani yako, ndani ya mtoto wako au mwenzi wako n.k kwa sababu tu ya kurogwa na wachawi, kuvamiwa na  nguvu za giza na dhambi.


Kuna watu kwa sababu ya kukosa afya ndio maana wao kila Mara wanaumwa na wengine wameweka hadi bajeti ya dawa kila wakipokea mshahara.


✓✓Ndugu, afya ni suala la kiroho, usipolishughulikia kiroho unaweza kuteseka sana.


✓✓Kuna watu wamerogwa afya zao zikaondoka, kinachofuata hapo ni magonjwa kuchezea miili yao.


 ✓✓Kuna watu wamefungwa vifungo vya kipepo na afya zao zikaondoa, magonjwa yanachukua nafasi.


Mimi Peter kwa kuombea watu mbalimbali na kufunuliwa kwa mafunuo juu ya kinachowasibu nimewahi kuona mambo mengi ngoja nikupe shuhuda mbili kutoka katika huduma yangu ya kuombea watu kwa simu.


Baba mmoja alikuwa anaumwa kila Mara na hali ilikuwa ni mbaya, akiponishilikisha nikamuombea na kwenye ulimwengu wa roho nikaona alivikwa vazi la magonjwa nilishangaa sana. Yaani wachawi walipokuwa wanamroga walimvalisha vazi liitwalo ugonjwa, kila akienda hospitalini hakupona, lakini maombi ya kulivua vazi la magonjwa alipona.


Mtu mmoja alikuwa anaumwa muda mrefu kumbe alirushiwa mapepo ya magonjwa, akipima hospitalini hakuna ugonjwa lakini katika hali halisi anaumwa sana, tulipofanya maombi ya kung'oa hizo nguvu za giza ndani yake akapona saa ile ile.


 Wachawi huwinda afya yako au ya mtu wako wa karibu, wakiiondoa hiyo afya ujue magonjwa yanachukua nafasi, na mpaka kuna watu wengi walioshindwa kumfuata YESU KRISTO Mwokozi walikufa kwa magonjwa hayo ya kichawi.


Kuna watu walirogwa na magonjwa yao yaliwaua kwa sababu hawakujua siri ya kupona kwamba ni kuufuata Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.


Nini ufanye katika maombi leo ya kuombea afya?


1. Kwa njia ya maombi ihitaji afya itokayo kwa MUNGU.


Yeremia 33:6" Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli."


Afya ya MUNGU ikiingia tu ndani yako unapona.


2. Kataa magonjwa kwa Maombi.


Zaburi 91:10" Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako."


Tauni inawakilisha magonjwa hiyo kataa magonjwa kwako, kwa familia yako, kwa mwenzi wako wa ndoa, kwa watoto wako n.k


3. YESU KRISTO anaponya magonjwa yote, hivyo mwambie akuponye kama unaumwa, aponye na watu wako wanaoumwa.


Mathayo 9:35 "Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina."

4. Omba MUNGU akuondolee magonjwa na yataondoka.


Kumbu  7:15 "Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao."


5. Omba MUNGU akuponye eneo linalozuia baraka zako.


Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye."


✓✓Mfano Kuna watu wamerogwa mirija ya uzazi, tumbo la uzazi, mayai ya uzao, mbegu za  kiume za uzao n.k ili tu  wasizae, omba MUNGU akuponye eneo hilo na utapona na kuzaa au kumzalisha mke wako wa ndoa.


✓✓Kuna watu wamewekewa vitu mwilini wao vinatembea, vitu hivyo huwa vimeelekezwa vizuie kitu fulani mwili mfano kutoa mimba ili mtu asizae, kupunguza damu mwilini ili mtu awe mgonjwa mwenye upungufu wa damu n.k, omba MUNGU akuponye eneo hilo na kitu hicho kitayeyuka, utakuwa huru kabisa.


Na maeneo mengine ya mwilini yenye tatizo lolote, omba MUNGU akuponye eneo hilo na utapona kabisa


6. Vunja na kuibomoa madhabahu ya giza inayoleta magonjwa kwako au kwa watu wanaokuhusu.


Kumbukumbu  7:5 Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."


Omba Ndugu katika jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU wa miujiza.


Omba Ndugu katika jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU wa miujiza.


Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kueleea naamini  ameelewa .


Hapa chini ni MAOMBI YA KUOMBEA AFYA.

Maombi haya ni kwa ajili ya mtu ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba.


Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.



MAOMBI YA KUOMBEA AFYA.


MUNGU Baba wa Mbinguni hakuna aliye kama wewe.

Ninakushukuru kwa neema yako na uzima wako mfalme wa wafalme. 


Niko mbele zako nikiomba kwa ajili ya afya yangu.


Eee Bwana MUNGU ninaomba unisamehe dhambi,  maovu na makosa, nifundishe kukucha wewe katika wokovu wa KRISTO YESU siku zote.


Niko mbele zako sasa JEHOVAH RAPHA MUNGU  Mponyaji nikiomba uponyaji wako katika afya yangu.


Neno lako linasema katika Yeremia 30:17 kwamba "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, 


Eee MUNGU Baba ninaomba kwa neema yako unirejeshee afya sawa sawa na Neno lako takatifu.

Nakusihi BWANA nirejeshee afya ili nisiteseke tena kwa magonjwa.

Naomba afya itokayo  kwako katika miguu yangu, kifua na kichwa changu ili kuwe uponyaji.


Naomba afya itokayo kwako  MUNGU Baba katika eneo lolote la mwili wangu lenye hitilafu ya ugonjwa.


Eee MUNGU Baba nakusihi ponya jeraha zote moyoni mwangu. 

Nakuomba Bwana YESU KRISTO ponya jeraha zilizotokana na magonjwa na ponya jeraha zilizotokana na kusingiziwa. 


Nakuomba BWANA ponya jeraha katika moyo wangu zilizotokana na kuonewa na zilizotokana na kuachwa au kuonewa kazini.


Neno lako MUNGU linasema utaponya jeraha zote ndani ya moyo wangu,  nakusihi BWANA uniponye jeraha zote zinazotokana na hila za watu wabaya na zinazotokana na vifungo vya giza.


Neno lako linasema utatakasa damu ambayo ulikuwa hujaitakasa.

Ndivyo inavyosema Yoeli 3:21 kwamba " Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Sayuni."


Eee MUNGU Baba naomba unitakase damu yangu yote katika mwili wangu.

Nitakase BWANA kwa kuondoa virusi, Bacteria na wadudu wote waleta magonjwa na wawezao kuondoa afya ndani yangu.


Sasa kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO niko kinyume na kila maajenti wa shetani wanaowinda afya yangu.

Imeandikwa katika Zaburi 91:10 kwamba " Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako."

Hivyo mabaya yote yaliyopangwa kunipata mimi, hayo mabaya nayakataa kwa jina la YESU KRISTO  na hayo mabaya hayatanipata mimi katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 


Mabaya yaliyopangwa usiku au mchana, hayo mabaya hayatanipata mimi  katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kwa jina la YESU KRISTO nakataa ugonjwa wa kuambukizwa au ugonjwa wa kutumiwa kipepo.


Bwana YESU KRISTO Neno lako linasema katika Mathayo 9:35 kwamba wewe Bwana YESU KRISTO unaponya magonjwa yote na madhaifu yote, naomba Bwana YESU uniponye kila ugonjwa ninaoufahamu na nisioufahamu.

Bwana YESU naomba uniponye kila udhaifu katika mwili wangu sawasawa na Neno lako maana Neno lako linasema unaponya madhaifu yote.


Kila madhabahu za giza zinazotengeneza mabaya na kuyaelekeza kwangu, hizo madhabahu za giza nazibomoa na kuzivunja kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Neno la MUNGU katika Kumbukumbu  7:5 linalosema " Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."

Hivyo kwa jina la YESU KRISTO ninavunja madhabahu za giza zote na ninaifunga kila kazi ya kishetani inayofanyika katika madhabahu za giza kwa ajili yangu, uzao wangu au familia yangu.

Ninakushukuru MUNGU Baba maana umetenda sawasawa na maombi yangu leo.

Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba na Kupokea. 

Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen. 


Ndugu, wewe ni mshindi. 

Endelea kuomba zaidi na utamuona MUNGU wa Miujiza akitenda.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292

Ndugu Endelea kuomba na MUNGU ni mwema sana.

Comments