ENDELEA KUMWAMINI MUNGU.

 

Na Mwl Peter Mabula





Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU kwa ufupi.
Ujumbe wangu Leo unasema "Endelea kumwamini MUNGU  katika KRISTO YESU."

✓✓MUNGU ni MUNGU wa nafasi nyingine,  sehemu ambayo akili yako imefika mwisho akili ya MUNGU ndio huanzia hapo.

Kesho haitakuwa kama leo. 
Upo ushindi wa MUNGU katika jina la YESU KRISTO. 

Ninachojua MUNGU katika KRISTO YESU anaenda kukupa ushindi wewe na sio adui yako.
Mngoje MUNGU wa Mbinguni na utaiona miujiza yake katika maisha yako na familia yako.

Zaburi 27:14 "Umngoje BWANA, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA."

✓✓Uwe hodari, piga moyo konde mngoje MUNGU wa miungu.

Zaburi 37:7 "Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa saburi; Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila."

✓✓Usimkasirikie anayefanikiwa wala usimkasirikie anayekufanyia hila, wewe mngoje MUNGU wa mbinguni na utaona atakavyotenda na atakavyokulipizia kisasi juu ya adui anayekutesa.

Zaburi 37:34 "Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona."

✓✓Wewe mngoje MUNGU huku ukiishi maisha matakatifu katika Wokovu.

MUNGU wetu atakuja na utauona ushindi unaouhitaji.

Isaya 35:4 "Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, MUNGU wenu atakuja na kisasi, na malipo ya MUNGU; atakuja na kuwaokoa ninyi."

Nimepata ufunuo huu ili kukutia moyo katika vita na magumu unayoyapitia.
Hakika Bwana YESU KRISTO atakuja na ushindi wako.
Muhimu sana endelea kuomba na kuishi maisha matakatifu,  nami nakuombea.
MUNGU akubariki sana. 
By Peter Mabula. 
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. 
+255714252292
Ubarikiwe

Comments