KIPAWA, KARAMA NA KIPAJI.

 

Peter Mabula na Jemimah Mabula


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu mpendwa.

Jifunze kitu kupitia ujumbe huu mfupi niliokuandalia.


Vipawa ni nini?


■Vipawa ni uwezo, nguvu, zawadi ya tofauti iliyo zaidi ya wengine anayopewa mtu ili amtumikie MUNGU.


Matendo  2:38 "Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI zenu, NANYI MTAPOKEA KIPAWA cha ROHO MTAKATIFU."


●Kipawa ni kipaji anachopewa mtu na MUNGU ili amtumikie MUNGU.


Waefeso 4:7 "Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake KRISTO."


Karama ni nini?


■Karama ni zawadi za Neema ambazo ROHO MTAKATIFU humpa mtu  anayeokolewa na YESU KRISTO ili amtumikie MUNGU. 


Matendo  11:17 "Basi ikiwa Mwenyezi MUNGU AMEWAPA wao KARAMA ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana YESU KRISTO, mimi ni nani niweze kumpinga MUNGU?"


Wewe ndugu uiyeokoka na una umepewa karama fulani, je unaifanyia kazi karama yako?


Je unawafanya watu kuokoka kupitia karama yako? Kama unafanya hivyo unafanya vyema sana.


Warumi 12:6-8 " Basi kwa kuwa TUNA KARAMA ZILIZO MBALIMBALI, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha."


■Kuna vipawa vya asili yaani alivyozaliwa navyo mtu, kwa jina lingine vinaitwa vipaji, lakini pia kuna vipawa huja tu baada ya kuokolewa na YESU KRISTO.


Hivyo karama na vipawa wakati mwingine vinaweza kufanana.


Wapo watu hutumia vipawa vyao vizuri na wengine hutumia vipawa vyao vibaya.


Sijui wewe unatumiaje kipawa chako ulichopewa na MUNGU ili umtumikie katika kazi yake.


Kanisani kumejaa vipawa vingi lakini sio wote wenye vipawa wanavitumia kwa kazi ya MUNGU.


Kuna watu wana vipawa vya kuongea sana lakini wanavitumia kwa umbea, uongo na majungu na sio kutumia kipawa hicho kupeleka injili ya KRISTO.


Wengine wana vipawa vya kuhubiri lakini akihubiri saa moja yeye amejitaja jina Mara 20 huku YESU KRISTO ambaye ndiye mwenye injili akimtaja Mara 1 tena katika mfano dhaifu, hiyo ni hatari sana.


Mwingine ana kipawa cha kuimba na katika albamu yake ya nyimbo za injili 9 hajamtaja YESU kwenye wimbo hata mmoja, hiyo ni hatari sana maana mtu anajiita mwimbaji wa nyimbo za injili harafu hamjui mwenye injili kwamba ni YESU KRISTO.


Biblia haitaki tujihubiri wenyewe bali tumhubiri YESU KRISTO anyeokoa.


2 Wakorintho 4:5 "Kwa MAANA HATUJIHUBIRI WENYEWE, bali KRISTO YESU ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya YESU."


■Kama wewe ni Mtumishi wa MUNGU una karama au kipawa,  mhubiri YESU KRISTO anayeokoa.


■Kama wewe ni Muimbaji una kipawa cha MUNGU imba kumhusu YESU KRISTO anayeokoa, Biblia inasema hapo juu kwamba hatutakiwi sisi tujihubiri wenyewe bali tumhubiri YESU KRISTO Mwokozi. 


Najua wapo wanaotumia vizuri sana vipawa vyao lakini hata wanaotumia vibaya vipawa vyao nao ni wengi sana.


Ndugu, wewe unayesoma ujumbe huu na umepewa kipawa na Bwana YESU basi tumia kipawa chako kwa utukufu wa MUNGU na sio wewe kutafuta utukufu.


Usitumie kipawa chako kama utavyo wewe bali tumia kipawa chako kama atakavyo MUNGU.


Warumi 12:6-9 "Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema."

MUNGU akubariki.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292.

Ubarikiwe

Comments