MAMBO MATANO MUHIMU KWA WATEULE WA MUNGU.

 

Na Mwl Peter Mabula

Bwana YESU KRISTO  atukuzwe ndugu!.

Karibu kwenye maarifa ya uzima.


1 Kor 4:1 ''Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa KRISTO, na mawakili wa siri za MUNGU. ''


✓✓Wateule wa Bwana YESU ni mawakili wa siri za MUNGU.


✓✓Wateule wa MUNGU ni watumishi wa KRISTO.


Kama mtumishi wa MUNGU na wakili wa siri za MUNGU lazima ujiweke kiutumishi na kuwa na utii mkuu kwa Bwana YESU aliyekuita ili umtumikie.


2 Kor 4:1 ''Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei;''


Mtumishi wa KRISTO lazima uzingatie yafuatayo;


1. HAKIKISHA UNAKUWA MWOMBAJI.


''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.-Yohana 14:13-14.


✓✓Waombaji Hubeba Siri Za MUNGU


✓✓Waombaji Hupokea Ufunuo Kutoka Kwa MUNGU


✓✓Waombaji Hupokea Maono Kutoka Kwa MUNGU


✓✓Waombaji hupokea neno la ufunuo kwa ajili ya Kanisa au huduma zao.


✓✓ Waombaji lazima wakae na neno na MUNGU.

Mimi Peter Mabula nakushauri ndugu unayesoma somo langu hili, hakikisha unakuwa Mtu wa maombi.


Luka 11:9 "Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa."


Ndugu zangu, utumishi ni huduma hivyo

Lazima Ulinde Huduma Uliyopewa Na MUNGU.

Linda huduma yako kwa maombi.


2. USILEGEE.


2 Kor 4:1 ''Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei;''


✓✓Usilegee Kwenye Huduma Yako

✓✓Usilegee Kuomba

✓✓Usilegee Kumtolea MUNGU zaka na sadaka.

✓✓Usilegee Kumwabudu MUNGU.


3. KATAA MAMBO YA AIBU .


2 Kor 4:2-3 ''lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU. Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;''


✓✓Mambo Ya Aibu Ni Matendo Yaliyojificha maovu

✓✓Ni Matendo Yanayotendeka Gizani maana ni ya giza.

✓✓Ni Matendo Ya Mwilini Yaliyo Machukizo kwa MUNGU


Mambo ya aibu ni Dhambi zote unazifahamu.


2 Kor 4:6 '' Kwa kuwa MUNGU, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa MUNGU katika uso wa YESU KRISTO''.


-Ndugu Yangu Hujaokolewa Kwenda Mbinguni Bali Umeokolewa Kwenda Duniani Kuhakikisha Ndugu Na Marafiki Zako Wote Wanaokoka, Ungeokolewa Kwenda Mbinguni Ungekuwa Umeshaondoka Lakini Umeokoka Uende Duniani, Mbinguni Utaenda Tu Maana Ni Haki Yako hivyo Kataa Dhambi, maovu na makosa yote.


4. PALILIA IMANI YAKO.


Warumi 5:1'' Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,"


Watu Wengi Wanafanya Mambo Ambayo Yako Kinyume Cha MUNGU Kwa Sababu Ya Upungufu Wa Imani. Ndugu Yangu Palilia Amani Yako, Ng'oa Vichaka Vinavyoizunguka Imani Yako, Ng'oa Mizizi Ya Miti Inayonyonya Imani Yako.


TUNAPALILIA IMANI KWA


✓✓Kusoma Neno La MUNGU

✓✓Kwa Maombi

✓✓Kwa Kumsifu MUNGU

✓✓Kumwabudu MUNGU

✓✓Kujumuika Na Watakatifu

✓✓Kumsikiliza ROHO MTAKATIFU

✓✓Kumtii KRISTO

✓✓Na Kutenda Kazi Ya MUNGU.


Ndugu Yangu, Ilinde Imani Yako, Ipalilie Imani Yako, Tengeneza Imani, Jenga Imani Yako, Nenda Kwa Imani Mathayo 17:20 '' YESU akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. ''


5. HAKIKISHA UWEPO WA MUNGU UPO PAMOJA NA WEWE.


Kutoka 33:15 "Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa."


Musa kama mmoja wa watumishi wa MUNGU aliona haiwezekani kutumika yaani kuwa Mchungaji kwa waisraeli bila uwepo wa MUNGU.


Hakikisha uwepo wa MUNGU  uko pamoja na Wewe.

Na uwepo wa MUNGU utakuwa pamoja na Wewe kama tu unaishi maisha matakatifu na unamsikiliza ROHO MTAKATIFU.


Wagalatia 5:16 "Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."


Hakikisha unakaa ndani ya Wokovu na Hakikisha una muda mrefu kutafakari ya  MUNGU Kila siku.


Zaburi 27:4-5 " Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.  Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba."


Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.

+255714252292(Ni namba hii  kupiga,  kuandika meseji na hadi whatsapp).

Comments