MAOMBI YA USHINDI WAKO LEO.

 

Na Mwl Peter Mabula

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Leo unayo nafasi ya kuomba na kupata ushindi.


Najua wewe ni muombaji  na unajua kwamba wakati mwingine ili kupambana na nguvu za giza unatakiwa uwe unaomba maombi ya vita yaani maombi ya kupambana na majeshi ya shetani na kuwashinda.


Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."


●Hawa mawakala wa shetani inakupasa kuwashinda, ila wakati mwingine sio kwa kuomba maombi laini laini tu ila inabidi uwe unajua kutumia silaha za ki maombi za kimaandiko na unajua kuomba.


●Wakati mwingine ili uwashinde wakuu wa giza inakupasa kuomba ukitumia silaha za MUNGU za kimaandiko.


Kuna funuo mbalimbali za namna ya kuomba kimaandiko Mimi Peter  leo ninakuketea ufunuo huu ambao Mimi nilifunuliwa na nikautumia katika maombi yangu.


Inawezekana maadui zako walishajua kabisa kwamba silaha yako kubwa katika maombi yako ni kusema "Toka jini, achia familia yangu, achia ndoa yako, achia afya yangu, achia biashara yangu, achia uchumba wangu, achia mwili wangu, achia uchumi wangu n.k) ni sawa kabisa kuomba hivyo  kama unaomba katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.


Leo kwenye maombi yako  wabadilishie maombi kidogo hao maadui zako ukitumia ufunuo huu wa leo wa ki maombi kupitia jina la YESU KRISTO Mwokozi.


Leo omba hivi.


1. Leo omba ukitupa moto wa YESU KRISTO kwenye madhabahu za giza wanazotumia maadui zako kukufunga vifungo au kukuharibia baraka zako, familia, ndoa, uchumba n.k


Luka 12:49 "Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi?"


Najua kuna wengine wanaojifunza somo hili leo ndio Mara ya kwanza kujua kwamba upo moto wa YESU KRISTO uliotupwa duniani ili kuharibu nguvu za giza na hila za shetani, huo moto uko kila mahali unakusubiri wewe muombaji uuelekeze pa kwenda kwenye madhabahu za kipepo ili kuharibu mipango yote ya giza kuhusu wewe inayoratibiwa hapo.


Kumbuka madhabahu za giza ndipo mahali mipango yote mibaya ya kipepo hupangwa dhidi yako.


Leo omba ndugu na katika jina la YESU KRISTO kuna ushindi mkubwa unaenda kuupata.


2. Leo omba ukiweka ncha ya upanga wa MUNGU kwenye nyumba za wachawi na wakuu wa giza wanaokuwinda.


Ezekieli 21:15" Nimeweka ncha ya upanga huo juu ya malango yao yote, ili mioyo yao iyeyuke, yakaongezeke makwazo yao; aha! Umefanywa kuwa kama umeme, umenolewa, ili uchinje."


Inawezekana kuna mtu ndio unajua kwa Mara ya kwanza kuhusu hili, ndugu ipo ncha ya upanga mkali wa MUNGU ambapo ncha hiyo huwekwa kwenye nyumba na malango ya mawakala wa shetani ili wasitoke kuja kwako kukuroga n.k


Huu upanga umenolewa, unakata kama umeme na ncha ya upanga huu unaweza kuuweka kwenye milango ya kiroho ya kupitia nguvu za giza zinapotaka kutoka ziliko ili zije kwako.


Inawezekana wewe huwa unakabwa na majinamizi, tumia ufunuo huu katika maombi yako na utanipa ushuhuda, weka ncha ya upanga wa MUNGU mahali wanakotokea na mahali wanapopitia hao majinamizi na hawatakukaba tena.


Unaweza ukashangaa mchawi anapotaka kuna kwako zana zake zinashindwa kuondoka kwenye nyumba yake, kumbe zikitaka kutoka zinakatwa na ncha ya upanga iliyowekwa na muombaji wanayetaka kwenye kumroga.


Ulishawahi kuona wakala wa shetani anashindwa hata kutoka kwake nyumbani akiwa katika hali yake ya kichawi?


Leo wa-surprise hao maajenti wa kuzimu kwa maombi katikajinalaYESUKRISTOMwokozi wetu aliye hai..


Walizoea sehemu ya kupigania vita ya kiroho na wewe ni nyumbani kwako, leo vita ihamishie nyumbani kwao.


Kila mchawi huwa ana mlango wake wa kuondokea kutoka kwake kwenda kuroga, hapo anapopitia ndipo weka ncha ya upanga wa MUNGU.


Upanga upo siku zote unakusubiri wewe muombaji kujitambua na kulijua Neno la MUNGU na namna ya kutumia maarifa ya maandiko katika maombi sawasawa na kusudi la MUNGU.


Ngoja nikupe ushuhuda mimi mwenyewe  Peter Mabula Siku moja usiku niliomba sana nikitumia andiko hili la Ezekieli 21:15, nikitumia huo upanga.


Kesho yake asubuhi rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kwamba ameniona kwenye maono nimezungukwa na majoka, mengine ya ajabu sana pamoja na wakuu wa giza, nimeshika upanga huku naomba, nilipouelekeza huo upanga kwa hao majoka kwa sekunde moja upanga uliwakata wote na kuwaua, akaniambia yaani upanga ule unakata kama umeme tu uwashwavyo, yaani kwa sekunde nguvu zile za giza zimekufa.


Nilimtukuza MUNGU kwa ushuhuda huo maana ingawa niliomba mimi lakini sikuona kwenye ulimwengu wa roho kinachoendelea hadi rafiki yangu huyo aliponijulisha alichokiona nikikifanya mimi.


Rafiki yangu mmoja pia nilipompa andiko hilo aliomba na MUNGU akampa kuona jinsi upanga huo unavyoweza kuangamiza majeshi ya pepo wabaya kwa sekunde moja.


Ndugu, leo tumia huo upanga dhidi ya nguvu za giza na nchi ya upanga huo uweke kwenye milango ya kiroho ya mawakala wa shetani.


Ndugu, leo omba na katika jina la YESU KRISTO utashinda.


3. Baada ya hapo kwa kutumia damu ya YESU KRISTO omba kwa jina la YESU KRISTO  ukitakasa sehemu ambazo zilikuwa hazijatakaswa.


Yoeli 3:21 "Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana BWANA ndiye akaaye Sayuni."


Damu ya YESU KRISTO ndio hufanya kazi za kutakasa yaani kusafisha kiroho na kufuta hatia na maagano ya kipepo.


Inawezekana wewe unaumwa, unahitaji damu ya YESU KRISTO ili kukutakasa na utaona uponyaji.


Mfano ni huu wa mtu mmoja aliyemwendea YESU KRISTO.


Mathayo 8:2-3 "Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.


 YESU akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika."


Mfano takasa kwa damu ya YESU mwili wako, afya, jina,familia, ndoa, kazi n.k.


1 Yohana 1:7 "bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Ye6su, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."


4. Omba kwa jina la YESU KRISTO  ukitumia damu ya YESU KRISTO ili kupatanisha.


Mambo ya Walawi 17:11" Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi."


Damu ya YESU KRISTO inaweza kukupatanisha na kazi yako hata ukaipata.


Damu ya YESU KRISTO inaweza kukupatanisha na watu muhimu wa kukusaidia.


Kuna mambo mengi unahitaji upatanisho, omba leo na MUNGU atakutendea muujiza huo wa upatanisho kupitia damu ya YESU KRISTO ya agano.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.

By Peter  Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.

+255714252292(Kwa chochote  au lolote au sadaka au  whatsapp ni namba hii tu).


Nakuomba share kwa marafiki zako  ujumbe huu kama ulivyo, usibadili chochote, usijiweke jina lako wakati hujaandaa wewe somo, hiyo ni tamaa chafu sana.

Ubarikiwe

Comments