BAADHI YA DALILI ZA MAPEPO.

 

Na Mwl Peter Mabula



Mathayo 12:43 "PEPO MCHAFU, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate."

Baadhi ya dalili  za mtu ambaye ama ana majini au anafuatiliwa na majini:-

1.    Unakuwa unaota ndoto kila mara upo baharini au uko  ndani ya maji unaogolea.

2. Kufurahia Sana kuangalia filamu za kutisha mfano filamu za majoka au watu wanaobadilika kuwa nyoka au wanyama wa kutisha au majitu ya kutisha, yaani wewe unajisikia raha Sana ukiangalia filamu hizo.

3. Kupenda sana kuvaa mapete nje ya pete ya ndoa halali au   nje ya pete ya uchumba halali, Mfano mapete makubwa hata mawili au zaidi.

Pia kupenda sana  kuvaa macheni, hereni n.k kiasi kwamba usipovaa unajiona kama hujakamilika.

4. Kila mara  unaota unacheza na nyoka, kuota nyoka anaingia mwilini mwako au wanyama au wadudu wengine wakiingia mwilini mwako, 

5.    Kila wakati unajikuta umeona au umeokota pete na unafurahia kuvaa pete hiyo; mara nyingi majini wanaotaka kujihusisha  na wanadamu hutegesha mikufu au pete ili kujiunganishwa na mtu huyo.

6.    Mara nyingi unapotembea unakuwa unasikia harufu ya udi, ubani au baadhi ya  marashi lakini hata hujui chanzo cha marashi hayo yanatokea.

 Si lazima majini hayo yawe ndani yako lakini yanaweza kuwa yanakufuatilia ili kukudhuru.

 7.   Wakati wa usiku  kila mara unasikia vitu vimepiga kwenye bati au darini bila kujua chanzo na mwisho wake.

  8.  Kudondoka chooni  bila sababu za msingi ni dalili nyingine ya mtu anayefuatiliwa na majini.

  9. Kufurahi alarm za ibada za dini wasio na YESU KRISTO, yaani unaposikia alarm hizo unafurahia sana.

  10.  Kukonda kupita kiasi katika hali ambayo sio ya kawaida yaani hali ambayo haitokana na kukosa chakula.

  11.  Kupenda kuvaa nguo za nusu uchi au matiti nje, yaani unafurahia sana nguo fupi Sana.

12. Kupenda kwenda kwa waganga wa kienyeji, yaani ukitatizika tu kidogo unapata wazo wa kwenda kwa mganga.

13. Kutokupenda kwenda Kanisani.

14. Kupenda sana kufanya dhambi fulani.

15. Kupenda ushoga, usagaji na machukizo ya namna hiyo, wewe unajikuta unapenda Mambo hayo, hata Kama wewe sio shoga wala sio mwanamke msagaji lakini unatamani hata kufanya uchafu huo.

16. Kila mara kuota unazini.

17. Kutamani kujiua.

18. Kuwa mtu wa hasira katika hali ambayo sio ya kawaida, yaani hasira hiyo inachochewa na majini ndani ya mtu.

19. Kuwa na vitabia vya ajabu ajabu vinavyopingana na Neno la MUNGU ambalo ni Biblia takatifu.

20. Kupenda sana Mambo ya kidunia yaliyo machukizo kwa MUNGU.

Mfano kupenda sana nyimbo za kidunia n.k

Ndugu, nakuandikia haya ili kama una majini kimbilia Kanisa ukaombewe katika jina la YESU KRISTO na utakuwa huru.

Luka 9:42 "Alipokuwa katika kumwendea, pepo akambwaga chini, akamtia kifafa. YESU akamkemea pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia babaye."

Nilizokuandikia hapo juu ni baadhi tu ya dalili za kuwa na mapepo/majini ndani ya mtu au ni dalili za mtu kutaka  kuvamiwa na majini/mapepo.

Ndugu yangu, kama ni wewe au ni mtu unamfahamu na unahisi kabisa ana majini basi mwelekeze Kanisa la kiroho jirani na aliko na watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO watamuombea na majini yatamwachia.

Ndugu yangu, ni kwamba Bwana YESU KRISTO huwa anaondoa majini ndani ya watu na palipo na jina la YESU KRISTO mapepo hawabaki hapo.

Mathayo 8:16 "Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,"

Palipo na nguvu za ROHO MTAKATIFU mapepo hawakai hapo na palipo na damu ya YESU KRISTO jini hakai hapo, hivyo ndugu yangu hakikisha tu unaombewa katika jina la YESU KRISTO utafunguliwa.

Hakikisha tu watu wa familia yako wanaombewa katika jina la YESU KRISTO na watafunguliwa kutoka majini na mizimu.

Ni jina la YESU KRISTO pekee ndio linaweza kuondoa nguvu za giza, litumie jina la YESU KRISTO katika Maombi yako siku zote na utakuwa huru.

Jina la YESU KRISTO ni jina kuu sana.

Wafilipi 2:9-11 " Kwa hiyo tena MUNGU alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa MUNGU Baba."

Mwenye kuelewa naamini ameelewa na atafanyia kazi ujumbe huu kama nilivyomwelekeza katika ujumbe huu.
MUNGU akubariki sana ukifanyia kazi
katika jina la YESU KRISTO.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe 

Comments