JUKUMU LA KUISHI MBINGUNI

 ✓✓Jukumu la kuishi Mbinguni liko mikononi mwako, maandalizi yake yako katika uwezo wako, maamuzi ya kwenda au kutokwenda unayo wewe.


✓✓Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kila siku unayo tiketi yako ya kwenda Mbinguni kwani hakuna cheo wala uzoefu utakaokuwezesha kuingia mbinguni.


Tiketi ya kwenda Mbinguni ni kumpokea YESU KRISTO Kama Mwokozi wako na Kisha kuendelea kuishi Maisha matakatifu ya Wokovu.


Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;"


Baadha ya kumpokea YESU KRISTO Kama Mwokozi yaani baada ya kuokoka unatakiwa uanze kuishi Maisha matakatifu ya Wokovu yanayofundishwa na Neno la MUNGU yaani Biblia takatifu.


1 Petro 1:14-15 " Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"


✓✓Ushauri wa bure ni kwamba Utafute kwanza ufalme wa Mbinguni na haki yake na hayo yote utazidishiwa.

Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."



✓✓Jitahidi kuishi maisha matakatifu kila siku.

 Kumbuka tiketi za ufalme wa MUNGU anazo Bwana YESU KRISTO.

Yohana 14:6 "YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; MTU HAJI KWA BABA, ILA KWA NJIA YA MIMI."


 Ndugu yangu, usikubali kuishi bila tiketi ya uzima wa Milele, tiketi hiyo ni kuokoka.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.


Comments