KUMBUKA NI WAPI ULIANGUKA UKATUBU.

 

Na Mwl Peter Mabula


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe!.


Karibu tujifunze Neno la MUNGU linalotuhitaji wote tunaohusika tuchukue hatua.



Kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



Ufunuo 2:5 "Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."



✓✓Je uasherati na uzinzi  ndio  mwanzo wa vifungo kwako?


Kumbuka ni wapi ulianguka ili sasa ukatubu na kuacha dhambi hizo.



✓✓Je kwenda kwa mganga ndio mwanzo wa wewe kuteswa na mapepo na kila aina ya uonevu?


Kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



✓✓Je kiburi chako ndio anguko lako?



✓✓Je  anasa za dunia ndio zimekuwa chanzo cha anguko lako hata shetani sasa anakutesa?


Ndugu kumbuka ni wapi ulianguka ili utubu.



◼️Wengi walimwacha YESU kwa sababu za mambo ya kidunia, ndugu kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



◼️Kuna watu waliacha ibada ndio maana sana wanateswa na vifungo vya Giza, kuna watu waliacha huduma walizopewa na MUNGU ndio maana kwa sasa shetani anawapepeta vile atakavyo, ndugu kumbuka ni wapi ulianguka ili utubu na kurejea katika Bwana YESU Mwokozi.



✓✓Je, wizi wako ndio imekuwa mlango wa shetani kukutesa? Je  mikataba ya ki shetani ulioingia ndio imekuwa chanzo cha laana kwako? Ndugu, kumbuka tena kumbuka sana ni wapi ulianguka ili sasa ukatubu.



✓✓Je kutokuwa Mwaminifu kwa MUNGU kutoa zaka ndio kumefunguliwa vifungo kwako na haujui imekuaje?


Ndugu, kumbuka ni wapi ulianguka ukatubu.



✓✓Je hujatimiza nadhiri uliyoahidi mbele za MUNGU ndio Maana majanga yamepewa kibali yakutese?


Ndugu, kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



✓✓Kuna watu kutoa mimba kwao ndio umekuwa mlango wa shetani kuwaonea.



✓✓Kuna watu uongo na dhambi za siri ndio vimekuwa chanzo cha maroho ya kuzimu kuwatesa.



◼️Ndugu, Biblia iko wazi mno kwamba kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



✓✓Je ukahaba wako ndio imekuwa chanzo cha kufungwa vifungo vingi vya Giza?


Ndugu ni saa ya kutubu na kurejea kwa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.



✓✓Je ni wapi ulianguka ili sasa utubu kwa Bwana YESU na vifungo vikuachie?



✓✓Je uliua hata damu ya uliyemuua inakulilia na shetani sana amekukalia kichwani?


Ndugu kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



✓✓Je uliacha ibada ya kweli katika Wokovu Wa KRISTO YESU ndio Maana nguvu za giza zinakutesa?


Ndugu, kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



✓✓Je uliwasema vibaya watumishi wa kweli ya Bwana YESU?


Je uliwatukana watumishi wa MUNGU waliokuambia ukweli? Ndio Maana shetani Sasa anakuonea?


Ndugu, kumbuka ni wapi ulianguka ili ukatubu.



Ndugu kumbuka ni wapi ulianguka ili Leo utubu.



◼️Najua unajua kabisa ni wapi ulianguka hivyo nakuomba utubu.


Ndugu Yangu, ni muhimu sana kutubu  kutengeneza kwa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.


Matendo  3:19 " Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"


MUNGU akubariki.


By Peter Mabula.


Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. 


+255714252292


Ubarikiwe.

Comments