MAOMBI YA KUFUTA MATUKIO YA KIPEPO YALIYOPANGWA KUHUSU WEWE.

 

Na Mwl Peter Mabula


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.

Karibuni sana tujifunze  Neno la MUNGU kisha tuombe ya ushindi.

Leo kwa Maombi tunafuta kila matukio ya kipepo  yaliyopangwa na ulimwengu wa roho wa giza.

Matukio ya kipepo/kichawi ni nini?

Matukio ya kichawi au kipepo ni mambo mabaya yanayopangwa na mawakala wa shetani ili yamtokee mtu waliyemkusudia katika muda walioupanga wao  hao mawakala wa shetani.

Matukio ya kichawi ni mambo yanayomtokea mtu  kulingana mipango ya kipepo iliyopangwa na vikao vya mawakala wa shetani dhidi ya mtu huyo.

Ninachotaka uone na ujue ni hiki, wanadamu wabaya wanaweza kupanga tukio baya kwa ajili ya mtu  katika muda fulani waliokusudia katika mwaka.

Mawakala wa shetani wanaweza kukaa kikao na kupitisha tukio baya ili likupate katika muda waliokusudia.

Katika Yeremia 18:18 tunaona watu wabaya wakikaa kikao kibaya dhidi ya Mtumishi wa MUNGU Yeremia na wakakubaliana kumpiga kwa kutumia vivywa vyao, wakakubaliana kumuua, walikubaliana kuichimbia shimo nafsi yake ili wamnase, waitegee mtego miguu yake ili anase, Yeremia aliomba maombi magumu sana kuhusu watu hao, aliomba hivi "  Niangalie, Ee BWANA, ukasikilize sauti ya wanaoshindana nami. Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate. Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.  Kilio na kisikiwe kitokacho katika nyumba zao, hapo utakapoleta kikosi juu yao kwa ghafula; kwa maana wamenichimbia shimo waninase, nao wameifichia miguu yangu mitego. Lakini wewe, BWANA, unajua mashauri yao yote juu yangu, ya kuniua; usiwasamehe uovu wao, wala usifute dhambi yao mbele za macho yako; bali wakwazwe mbele zako; uwatende mambo wakati wa hasira yako.-Yeremia 18:19-23"

 Mfano mwingine wa matukio ya kipepo ni ndugu wa Yusufu kupanga kumuua Yusufu bila kosa.

Mwanzo 37:18 "Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue."

Ukisoma Waamuzi 16:5 unaona kikao cha kipepo kati ya Delila na viongozi wa wafilisti ili Delila amsaliti Samson.

Ilipowezekana Samson kusalitiwa tunaona alifungwa, akawa mtumwa, akawaletea faida wao hao mawakala wa shetani kwa sababu alikuwa anasaga ngano na tukio baya zaidi walimtoboa macho.

Haya ni mfano hai wa  aina ya baadhi ya matukio ya kichawi anayoweza kupangiwa mtu na nguvu za giza.

Inawezekana majini wanapanga tukio ili mwenzi wako akusaliti ili upate madhara, Mama mmoja alikufa kwa presha baada ya kugundua mume wake amezaa nje ya ndoa.

Baba mmoja alifariki kwa mshtuko baada ya kumfumania mkewe akizini.

Mawakala wa shetani wanaweza kupanga madhara makubwa kwa mtu hata mwaka mzima unaisha  hajatimiza malengo yake.

Matukio ya kichawi ni mengi tu, ndugu mmoja alishindwa kuendelea na shule baada ya wazazi wake kufa ghafla kwa ajali, ni hatari sana.

Ndugu mmoja hata ndoa yake haijamaliza wiki tangu afunge ndoa mwenzi wake alifariki, ni matukio mabaya sana.

Leo unaweza kuomba na ikawa hivi kwa hao wakuu wa giza waliokupangia matukio mwaka huu.

Mithali 26:27 "Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia."

 Leo kwa mamlaka iliyo katika jina la YESU KRISTO futa matukio ya kipepo yote yaliyopangwa kuhusu wewe, watoto wako, familia yako au chochote chako mwaka huu.

●Kumbuka kila jambo huanzia katika ulimwengu wa roho hivyo matukio mabaya hupangwa na ulimwengu wa roho wa giza.

●Inawezekana hata umewahi kuona kwa ndoto juu ya mipango hiyo ya kipepo dhidi yako, usipuuzie ila omba katika jina la YESU KRISTO na matukio hayo ya kipepo hayatakupata.

Matukio ya kipepo/kichawi  yanaweza kuwa kifo, ajali, ulemavu wa ghafla, kuachwa, kufiwa na watu muhimu, kufukuzwa kazi, magonjwa, balaa, mikosi n.k

Inawezekana sio watu wote wanaoomba maombi Maombi haya wamekusudiwa, inawezekana sio wote wamepangiwa ratiba za kipepo, inawezekana sio wote wamepangiwa matukio ya kichawi, ila  ndugu omba.

 Usiwaogope mawakala wa shetani ila wazime kwa maombi maana umepewa kibali na MUNGU cha kuomba katika jina la YESU KRISTO na utatendewa kama ulivyoomba.

Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba(MUNGU) atukuzwe ndani ya Mwana(YESU)."

Inawezekana umepanga mipango mizuri sana mwaka ujao lakini mawakala wa shetani wamekupangia mipango mibaya sana mwaka huo huo, ndugu msaada wako ni maombi katika KRISTO YESU Mwokozi aliye hai.

 Inawezekana wanapanga mwezi fulani mwaka huo  unaokwenda kuuingia wakutumie roho ya mauti, inawezekana wanajua unaenda kufanikiwa sana mwaka huo ila wamekusudia upatwe na ugonjwa ili mipango yako isimame hadi mwaka unaisha hujafanya chochote.

Inawezekana mwaka huu walikupangia matukio ndio maana hadi mwisho wa mwaka hukufanikiwa hata jambo moja ulilokusudia, matukio ya mwaka huu na ratiba ya mwaka jana inawezekana wamepanga kuirudisha kwako mwaka ujao, ndugu wazimishe kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO na mipango yao kuanzia leo itavunjika.

Kuna Mtu mmoja, yeye binafsi hawakumgusa ila kwa mwaka mzima alienda kwao msibani zaidi ya Mara 4 kwa mwaka na kwao ni mbali hivyo alitumia pesa nyingi sana za malengo yake hivyo malengo hayakufanikiwa, ndugu mwaka ujao  omba leo na utamuona MUNGU akiwalinda hata watu wako wa karibu ili usipate hasara.

  Namshukuru Bwana YESU sana kwa ROHO wake anayetufunulia ya sirini, Mimi naamini waliokusudiwa na MUNGU watamtukuza MUNGU maana matukio yote  ya kichawi  hayatatokea Bali ushindi mkuu mwaka ujao utatokea.

 Sasa nini ufanye kuhusu matukio ya kichawi yaliyopangwa kuhusu wewe mwaka ujao?

1. Omba MUNGU akulinde dhidi ya kila hila ya shetani mwaka huu wote.

Zaburi 121:7 "BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako."

2. Omba ROHO MTAKATIFU akufanye uwe kule atakako MUNGU na sio kule wanakotaka uwe mawakala wa shetani.

Zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."

3. Omba MUNGU akupe neema ya kuisikia na kuielewa na kuitii sauti yake ili usiangukie kwenye matukio ya kipepo yaliyopangwa.

MUNGU huzungumza, kazi yako ni kuielewa sauti yake na kuitii.

Mfano ni huu.

Ezekieli 3:22 "Na mkono wa BWANA ulikuwako juu yangu huko; akaniambia, Ondoka, enenda uwandani; nami nitasema nawe huko."

Mfano  mwingine ni Yakobo aliyepona kuuawa na Esau. 

Mwanzo 35:1 "MUNGU akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie MUNGU madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako."

Kufuata maelekezo ya MUNGU ni jambo jema sana maana hakuna mpango wa giza utakupata.

4. Futa kimaombi matukio yote ya kipepo yaliyopangwa kuhusu wewe mwaka huu.

Mathayo 16:19 " Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."

5. Haribu madhabahu za giza zinazotengeneza matukio yeyote kuhusu wewe mwaka huu.

Kumbu 7:5 "Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."

6. Wachafulie usemi wanaokaa kikao ili kukupangia mabaya.

Waamuzi 7:22 '' ....... naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuendelea Serera, hata mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.'' 

Andiko hilo ukilisoma katika Tafasiri ya BHN Biblia inasema hivi '' ........ Mwenyezi-MUNGU aliwafanya Wamidiani waanze kuuana wao kwa wao kambini. Waliosalia wakatoroka hadi Serera panapoelekea Beth-shita, hadi mpakani mwa Abel-mehola karibu na Tabathi. ''

MUNGU aliwafanya maadui za Israeli kuuana wao kwa wao.

Hata kwako inawezekana kabisa una maadui wengi kazini kwako,  kwenye biashara au ndoa yako ina maadui wengi, au una maadui kwenye ukoo, kwenye mtaa au sehemu yako ya biashara lakini unaweza kuomba maombi ya kuwachafulia usemi maadui zako na utashangaa mwakani maadui hao wanakosana wao kwa wao, utashangaa hata vikao walivyopanga kukaa  kukujadili vinakufa, matukio waliyoyapanga kuhusu wewe mwaka ujao  utashangaa hayawezi kutokea maana watekelezaji watakosana hata kama hawapendi kukosana.

7. Amuru mapigo kwao.

Yeremia 51:20-21 "Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;"

Omba ndugu na utashinda.
 Mimi Peter Mabula natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
Hapa chini ni  MAOMBI YA KUFUTA MATUKIO YA KIPEPO YALIYOPANGWA KUHUSU WEWE MWAKA HUU UNAOENDA KUINGIA.
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba

Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.

MAOMBI YA KUFUTA MATUKIO YA KIPEPO YALIYOPANGWA KUHUSU WEWE MWAKA HUU UNAOENDA KUINGIA.

BABA katika jina la YESU KRISTO,  Niko mbele zako MUNGU wangu nikikushukuru kwa ajili ya Siku hii na kwa ajili ya  nafasi hii ya Maombi mbele zako.

Niko mbele zako pia MUNGU Baba nikitubu na kuomba msamaha  kwa jambo lolote nililotenda kinyume na kusudi lako, naomba BWANA unisamehe.

Naomba unisamehe dhambi zangu zote, maovu na makosa. 

Naomba BWANA unitakase roho yangu,  nafsi yangu na mwili wangu.

Bwana YESU nisafishe kwa damu yako ya thamani ili niwe safi bila mawaaa mbele zako na mbele za MUNGU Baba yangu wa Mbinguni. 

Mfalme wa wafalme na MUNGU mwenye nguvu niko mbele zako BWANA  nikiomba kufuta kila matukio mabaya yaliyopangwa kuhusu mimi mwaka huu mpya ambao utanipa neema kuuingia. 

Imeiandikwa katika Mathayo 16:19 kwamba kila jambo nitakalolifunga Duniani katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu,  hilo jambo na Mbinguni litafungwa. 

Sasa kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninafuta na kufunga kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu mimi au familia yangu au ndoa yangu, hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu biashara yangu au kazi yangu, hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu mwenzi wangu wa ndoa au watoto wangu, hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu  uchumi wangu au kibali changu au pesa zangu, hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu mwili wangu au afya yangu, hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu nafsi yangu au roho yangu,  hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu  tumbo langu la uzazi au sehemu yeyote ya mwili wangu,  hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila matukio ya kipepo yaliyopangwa kuhusu eneo langu, hayo matukio nayafuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate nikiwa safarini au nikiwa nyumbani. 

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate nikiwa usingizini au nikiwa njiani au barabarani.

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate kazini au nikiwa mbele za watu. 

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate nikiwa nimekaa au nikiwa nimesimama.

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate mchana  au usiku.

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate asubuhi au jioni. 

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yanipate adhuhuli au alfajiri. 

Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yaipate familia yangu au watoto wangu.

 Kwa jina la YESU KRISTO ninafuta kila matukio ya kichawi yaliyopangwa yampate mwenzi wangu popote. 

Kila tukio la kipepo lililopangwa na mchawi, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio  lililopangwa na majini, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio lililopangwa na majoka au mapepo,  hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio  lililopangwa na mizimu au miungu,  hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio  lililopangwa na majini mahaba, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio  lililopangwa na kila maroho wa kuzimu,  hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio  lililopangwa na shetani na mawakala zake wote, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio la kipepo lililopangwa na mganga wa kienyeji au mshirikina, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

L
Kila tukio la kipepo lililopangwa na watu wangu wa karibu, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Kila tukio la kipepo lililopangwa na mtu yeyote asiyenipenda, hilo tukio la kipepo nalifuta kwa jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 

Mahali kokote na katika muda wowote litakapopangwa tukio lolote la kishetani  kuhusu mimi au familia yangu au ndoa yangu au nchi  yangu,  hilo tukio la kishetani nalifuta kwa jina la YESU KRISTO na halitafanyika kamwe. 

Nakushukuru MUNGU wangu maana  hakuna tukio lolote la kishetani lililopangwa litakalofanikiwa.

Nakushukuru MUNGU wangu maana  hakuna tukio lolote la kishetani  litakalopangwa ambalo litafanikiwa.

Katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai  nimeomba na kushukuru. 

Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeen.
Hakika umeshinda.
MUNGU akubariki sana. 
By Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO. 
+255714252292 (Sadaka, Maombezi, ushauri wa kiroho n.k
Ndugu nakuomba endelea na Maombi na utamuona MUNGU wa miujiza

Comments