NAMNA YA KUULINDA MOYO WAKO.

 

Na Mwl Peter Mabula


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu. 

Biblia Inasema Tuulinde Moyo Kuliko Vyote Tulindavyo.

Mithali 4:23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima."

Kwa Jinsi Gani Utaulinda Moyo Wako? 


Moyo Wako Utaulinda Kwa Kuzingatia Haya Mambo 8.  


1. Ili Uulinde Moyo Wako Weka Neno La MUNGU Kwa Wingi Moyoni Mwako.


Zaburi 119:11 "Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi."


2.  Ili Uulinde Moyo Wako Epuka Vikundi Vibaya.


1 Wakorintho 15:33 "Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema."


Zaburi 1:1 "Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha."


3. Ili Uulinde Moyo Wako Usifikiri Mambo Ya Mwilini.


Warumi 8:8 "Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza MUNGU."


4.  Ili Uulinde Moyo Wako Hakikisha Unasahau Mabaya Yaliyopita.



 Isaya 43:18 "Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani."


5. Ili Uulinde Moyo Wako Hakikisha Unaridhika Na Ulichonacho.


1 Timotheo 6:6 "Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa."


Uatauwa ni ucha MUNGU. 


Mithali 15:16 "Kuwa na mali chache pamoja na kumcha BWANA; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu."


6.  Ili Uulinde Moyo Wako Jitahidi Kuomba Mara Kwa Mara.

1 Wathesalonike 5:17-19" ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU. Msimzimishe ROHO;"


7. Ili Uulinde Moyo Hakikisha Unamtafuta MUNGU Kila Wakati.


Zaburi 34:4 "Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote."


8. Ili Uulinde Moyo Wako Usikubali Kutawaliwa Na Mawazo Mabaya. 


Yakobo 2:4 "je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?"


Marko 7:21-23 " Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi."

MUNGU Wangu Na Akubariki. 

Mtii KRISTO Na Hakikisha Unajazwa ROHO MTAKATIFU Na Anza Kuenenda Kwa ROHO. Ikatae Dhambi, Iogope Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usifanye Dhambi.

Bwana YESU KRISTO Yu Karibu. 

Shika Wokovu Asije Mtu Akakunyang'anya. Hata Kama Utadharaulika Lakini Mtii Bwana YESU KRISTO Na Usimwache Hata Kidogo.

MUNGU akubariki. 

By Peter Mabula. 

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. 

+255714252292

Comments