SAUTI NILIYOISIKIA MWAKA 2015.

 

Na Mwl Peter Mabula


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.


Siku moja mchana mwaka 2015 nilisikia sauti ikiniambia ''KWANINI YESU KRISTO? ''


Nikataka kujibu lakini kabla sijajibu ile ile sauti ikaniambia kwamba ''NI KWA SABABU YA UZIMA WA MILELE''


Nilitiwa nguvu sana kwa sauti hiyo ya live niliyoisikia, kwa sababu kila ninachoambiwa na ROHO wa MUNGU huwa nakiandika basi niliandika haraka haraka ujumbe ule na kuendelea kuutafakari kwamba ''Kwanini YESU KRISTO? Ni kwa sababu ya uzima wa milele.''


Ndugu zangu wote, hakuna wokovu nje na KRISTO YESU.


Matendo  4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."


✓✓Tukimtaja YESU KRISTO tunakuwa tunamtaja aliye pekee anayeweza kuwapeleka wanadamu uzima wa milele.


✓✓Tukimpokea YESU KRISTO tunakuwa tumepokea uzima wa milele ambao uko tayari kwa ajili yetu kama tu tukidumu katika utakatifu wake KRISTO.


✓✓Linapotajwa jina la YESU maana yake hapo panatajwa uzima.


Ndio maana uponyaji hutokea baada ya jina la YESU KRISTO kutajwa.


✓✓Kuokoka ni kuchagua uzima wa milele.


✓✓Kuishi maisha matakatifu ndani ya KRISTO ni kuubeba uzima wa milele.


✓✓Kuishi maisha ya matakatifu ya wokovu ni kama kutanguliza mwili wako uzima wa milele.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

+255714252292

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Comments