TALANTA YAKO ITUMIE ILI KUULETEA FAIDA UFALME WA MUNGU.

 

Na Mwl Peter Mabula

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.


Talanta ni Nini?


Talanta ni fedha ya mtaji inayohitajika kuzalishwa ili kuongezeka.


✓✓Kibiblia talanta ni karama au Huduma unayotakiwa kuifanyia kazi ili kumletea faida MUNGU.


✓✓Talanta ni Huduma aliyoweka MUNGU ndani yako kwa lengo la kumzalia matunda.


Mathayo 25:14-18 " Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.  Akampa mmoja TALANTA TANO, na mmoja TALANTA MBILI, na mmoja TALANTA MOJA; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule ALIYEPOKEA TALANTA TANO akaenda, akafanya biashara nazo, AKACHUMA FAIDA talanta nyingine tano. Vile vile na yule MWENYE MBILI, yeye NAYE AKACHUMA nyingine mbili FAIDA. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake."


Ufalme wa MUNGU unakuhitaji ushughulike na unakuhitaji kuzitumia karama zako alizokupa ROHO MTAKATIFU baada ya wewe kuokoka.


Warumi 12:6-8 " Basi kwa kuwa TUNA KARAMA ZILIZO MBALIMBALI, kwa kadiri ya neema mliyopewa; IKIWA UNABII, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; IKIWA HUDUMA, tuwemo katika huduma yetu; MWENYE KUFUNDISHA, katika kufundisha kwake; MWENYE KUONYA, katika kuonya kwake; MWENYE KUKIRIMU, kwa moyo mweupe; MWENYE KUSIMAMIA kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha."


✓✓Nguvu uliyonayo mteule ni talanta ambayo unatakiwa uitumie kuwaleta watu kwa YESU KRISTO. 


Je unaitumiaje talanta yako?


✓✓Mali zako au fedha zako ni talanta unayotakiwa kuitumia kuipeleka injili ya KRISTO mbele. 


Je unaitumiaje talanta yako?


✓✓Karama na Huduma uliyopewa na ROHO MTAKATIFU ni talanta unayotakiwa kuitumia vyema ili kumzalia KRISTO matunda.


Wewe una Mali za MUNGU na hizo Mali MUNGU anataka faida itakayotokana na kuzalisha kwako kutoka katika Mali hiyo aliyokupa MUNGU.


✓✓Mali za MUNGU kwako ni karama, vipawa,Huduma, utumishi,muda,fedha na vyote alivyokubariki.


Ndugu hakikisha unamletea MUNGU faida inayotokana na uhai aliokupa,  kutoka katika talanta ambayo MUNGU amekupa.


Ikiwepo Huduma basi tuwemo katika Huduma.


Hakikisha wakati au muda wa Huduma uliyopewa na MUNGU unakuwa katika Huduma hiyo.


Wakati wa Huduma uliyopewa na MUNGU hakikisha unauzingatia muda huo na  timiza Huduma yako.


✓✓Muda wako wa kuwa kwenye uimbaji kwaya hakikisha unakuwepo.


✓✓Muda wako wa kuhubiri hakikisha unakuwepo.


✓✓Muda wako wa kushuhudia mitaani hakikisha unakuwepo.


✓✓Muda wako wa kumtolea MUNGU hakikisha unakuwepo.


✓✓Muda wako wa kufanya kazi ya MUNGU ya aina yeyote hakikisha unakuwepo.


Sababu zinazoweza kumfanya mtu asiitumie talanta yake aliyopewa na MUNGU.


1. Kutokumwamini MUNGU.


2  Nyakati 20:20 "......... mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa."


Usipomwamini MUNGU ni dhambi.


Usipomwamini MUNGU ni vigumu kumtumikia hata umzalie matunda.


2. Hofu


Mathayo 25:25 "basi NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako."


Una hofu ya nini  katika kutumia talanta yako aliyokupa Bwana YESU?


Ukitaka uifanyie kazi talanta yako kataa hofu.


3. Shughuli za kidunia.


Marko 4:19 "na SHUGHULI ZA DUNIA, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine ZIKIINGIA, HULISONGA LILE NENO, LIKAWA HALIZAI."


Talanta ya MUNGU kwako huambatana na Neno la MUNGU.


Mambo ya kidunia ukiyapa nafasi sana moyoni mwako yataliondoa Neno la MUNGU ndani yako na kukufanya usifanyie kazi talanta yako.


Udanganyifu wa Mali ni mambo ya kidunia.


Tamaa za mambo yeyote yanayokuondoa kwa YESU ni sumu Kali ya kuharibu utendaji kazi wa talanta yako hata izae matunda.


4. Uchanga wa kiroho.


Waefeso 4:14 "ILI TUSIWE TENA WATOTO WACHANGA, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu."


Uchanga wa kiroho unaweza kukufanya usimtumikie MUNGU katika talanta aliyokupa.


Inakupasa kufanya juhudi ili ukue kiroho.


Juhudi za kukufanya ukue kiroho ni maombi, kusoma Neno la MUNGU na kulitafakari na kukataa mazoelea mabaya na kukataa dhambi.


5. Uoga.


Mathayo 10:28 "Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum."


Uoga hautakiwa kuwa katika kundi la wateule wa MUNGU.


Kataa woga na tafuta namna ya kuondoa uoga wako kwa Neno la MUNGU.


Muogope MUNGU tu na sio kumuogopa shetani au kuwaogopa wanadamu.


6. Upofu wa kiroho.


2 Wakorintho 4:4 "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU."


Kuna watu ni vipofu wa rohoni.


Hawa wanaweza kufanya hata yasiyowapasa kwa sababu tu ya upofu wao wa kiroho.


Vipofu wengine wa kiroho ni wale wanaotumia talanta zako kwa shetani na sio kwa MUNGU, mfano waimbaji wa nyimbo za kidunia.


7. Kutokujua wajibu wako mteule kwamba unatakiwa kuzaa matunda.


Yohana 15:4-5 " Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote."


Unahitaji kujitambua kama mteule wa KRISTO na tambua wajibu wako.


Ndugu, Unahitaji sana  kumtumikia Bwana YESU KRISTO.

MUNGU akubariki ukifanyia kazi ujumbe huu.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292

Ubarikiwe sana

Comments