KUPASUA VITI VYA ENZI VYA KICHAWI VYA AGANO LA KURITHI.

 

Na Mwl Peter Mabula

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU kutoka katika sehemu ya somo langu, hii ni sehemu fulani ya somo hilo.


Waebrania 9:16-17 " Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.''


✓✓Ndugu, wewe umerithishwa nini cha kipepo na Bibi, Babu, Baba, Mama au mtu yeyote uliekuwa unaishi naye?


✓✓Wako watu wamerithishwa agano la urithi la utasa.


✓✓Wako watu wamerithishwa agano la urithi la pombe.


✓✓Wako watu wamerithishwa agano la urithi la kutesa wenzi wao wa ndoa.


✓✓Wako watu wamerithishwa agano la urithi la umasikini, hata akipata kazi muda mfupi anafukuzwa, au anabaki na kazi yake yenye mshahara mkubwa lakini maendeleo hata ya kununua nguo mbili mpya kwa mwaka hana na hajui pesa yake huishia wapi.


 ✓✓Wako watu wamerithishwa agano la urithi la magonjwa.


✓✓Ndugu zangu ukisoma Biblia hakuna magonjwa ya kurithi, hivyo ukiona ukoo au familia wana magonjwa ya kurithi ya ukoo ujue ni kazi za shetani katika ukoo huo zinawatesa. Leo Kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai vunja madhabahu za giza za ukoo na haribu viti vya enzi vya kichawi vinavyotokana na Agano la kurithi.


Ndugu, je wewe umerithi nini?


✓✓Je umerithi kufilisika?


✓✓Je umerithi kifo cha mapema?


✓✓Je umerithi kutambika?


✓✓Je umerithi tabia ya ugomvi?


✓✓Je Mume wako au Mke wako ukimuangalia kwa makini  tabia mbaya zake,  na tabia hizo hizo ndugu  zake wengi wanazo pia unahisi ni agano gani la urithi amerithi?


Leo katika jina la YESU KRISTO haribu na kulifuta agano hilo la urithi la kipepo.


Kuna ukoo Babu alioa kisha akaachana na mke wake baada ya kuzaa watoto kazaa, Baba naye hivyo hivyo alioa kisha akaacha, watoto nao hivyo hivyo, na ajabu wajukuu nao ni hivyo hivyo, ndia maana unashangaa Sasa Mume wako au Mke wako anatamani muachane au anapanga muachane na kumbe ni muda wa agano  la urithi la kwao  linataka lianze kufanya kazi yake.


Ndugu Yangu, Vita yako wewe unaijua, hivyo kama kuna agano la urithi ndio chanzo kwako au kwa ndoa yako au kwa familia yako au kwenye mwili wako, hilo agano la urithi lifute kwa jina la YESU KRISTO.


Waebrania 9:14" basi si zaidi DAMU yake KRISTO, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa MUNGU kuwa sadaka isiyo na mawaa, ITAWASAFISHA DHAMIRI ZENU na MATENDO MAFU, mpate kumwabudu MUNGU aliye hai?"


Ndugu, hakikisha unalifuta kwa damu ya YESU KRISTO kila agano la urithi linalokutesa wewe, kutesa ndoa yako, kutesa mwili wako, kutesa familia yako n.k


Omba katika jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU wa miujiza akikutendea maajabu.


ROHO MTAKATIFU akikupa hata ufunuo zaidi wa maombi omba na hata akikupa ufunuo wa sadaka au wa kufunga tena baada ya maombi haya fanya hivyo na utamuona MUNGU.


 Nini ufanye kimaombi?


1. Tubu kwa ajili ya chanzo cha maagano hayo kukufikia wewe.


 Isaya 59:1-2  '' Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. ''


2.  Haribu agano la urithi ulilorithishwa kichawi.


Haribu kwa damu ya YESU KRISTO.


Damu ya YESU KRISTO ndiye inaweza kukusafisha dhidi ya kila udhalimu ukiwemo maagano ya kurithi ya kipepo.


1 Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."


3. Vunja maagano ya giza yote ya uliyorithi kutoka kwa wazazi wako au mababu zako.


Hosea 10:4 "Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba."


Vunja kwa jina la YESU KRISTO.


4. Futa kwa damu ya YESU KRISTO kila maagano ya urithi ya kipepo yale uliyoona ndotoni au kwenye maono na ukajua kwamba unajulishwa juu ya agano la kipepo la urithi.


Ufunuo 12:11 "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa."


 5. Bomoa na kuvunja madhabahu za giza zilizotengeneza maagano ya kipepo ya urithi katika ukoo wako.


Kumb 7:5 '' Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga. ''


6. Acha tabia mbaya zote zinazotokana na nguvu za giza za kurithi, ziache kwanza kisha omba kwa MUNGU ili tabia hizo zikuachie na zisikufuate tena.


1 Thesalonike 5:22 '' jitengeni na ubaya wa kila namna. ''


7. Omba Bwana YESU amiliki na kutawala maisha yako.


Yohana 15:16" Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni."


Ndugu yangu omba na utamuona MUNGU akikuondolea kila kazi ya shetani ya kiukoo inayokufuatilia.

MUNGU akubariki sana.

Kama hujaokoka nakuomba okoka Leo Kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na jina lako litaandikwa Mbinguni katika kitabu cha uzima.

Hakikisha Baada ya Kuokoka unaishi maisha matakatifu ya Wokovu.

MUNGU akubariki.

By Mwl Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292

MUNGU akubariki.

Comments