MAOMBI YA KUMWITA JEHOVAH RAPHA KATIKA UZAZI.

 

Na Mwl Peter Mabula 


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote. 
Karibu tujifunze Kisha tuombe Maombi ya ushindi.

MUNGU Baba  ana sifa nyingi sana na ana utendaji wa aina nyingi sana.

●Ukimwita kama MUNGU mlinzi wako hakika atakuja kukulinda.

Zaburi 121:5-7" BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele."

●Ukimwita kama MUNGU Mwokozi wako hakika atakuja na kukuokoa.

Kutoka 6:6 "Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;"

MUNGU Baba ni Mwokozi ndio maana anasema ''Nitawaokoa''

Hata ukisoma Wakolosai 1:13 Biblia inasema ''Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;''

Kwa sababu MUNGU ni Mwokozi Biblia inasema ''Alituokoa"

●Ukimwita MUNGU kama mleta amani  atakuja na kuileta amani hiyo.

Kwenye Eneo la kuleta amani MUNGU Baba anaitwa JEHOVAH SHALOM.

Waamuzi 6;24 '' Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri. ''

MUNGU anayo amani yake ambayo anaweza kuileta kwa mtu au katika familia au katika kundi la watu wake.

Wafilipi 4;7 '' Na amani ya MUNGU, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika KRISO YESU. ''

●Na ukimwita MUNGU kama MUNGU mponyaji hakika atakuja kwako na kuponya eneo lako linalohitaji uponyaji.

Katika kipengele cha uponyaji Waisraeli walimwita MUNGU kwa jina la JEHOVAH RAPHA.

●JEHOVAH RAPHA maana yake MUNGU mponyaji au MUNGU aponyae.

Kutoka 15:26 ''akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.''

Neno "BWANA Nikuponyae" katika Biblia za kiebrania ni JEHOVAH RAPHA.

 ●Walimwita JEHOVAH RAPHA kwa sababu alikuwa anaponya kila eneo analolitaka kuliponya.

Walimwita JEHOVAH RAPHA kwa sababu ndivyo alivyo.

Leo katika maombi haya ya kuombea uzao mwite MUNGU Baba kama JEHOVAH RAPHA yaani mwite kama MUNGU mponyaji wako na atakuponya kwenye kila eneo linalohitaji uponyaji.

●Kwa sababu wewe unahitaji uponyaji kwenye eneo  la uzao mwite JEHOVAH RAPHA  aponye na ataponya.

Kama ndoa yako inahitaji uponyaji kwenye eneo la uzao mwite JEHOVAH RAPHA atawaponya wewe na mwenzi wako ili mzae.

■Kuna watu hawajapata watoto kwa sababu mirija ya uzazi imeziba, Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji  ataponya mirija yako ya uzazi na utazaa.

Yeye ni MUNGU anayeweza  kukuponya kimwili hadi kiroho.

Yeremia 30:17 ''Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.''  

■Kuna watu hawajapata watoto katika ndoa zao kwa sababu Mume hana mbegu za uzao, huwa anatoa tu majimaji  yasiyo na mbegu au anatoa mbegu dhaifu ambazo hazina uwezo wa kukutana na yai ndani ya mke wake, Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya au atamponya mwenzi wako wa ndoa au mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.

■Kuna watu wana uvimbe ndio maana wameshindwa kushika mimba,Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya au atamponya mwenzi wako wa ndoa au mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.

■Kuna watu wamerogwa ndio maana  hawawezi kuzaa,  Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya au atamponya mwenzi wako wa ndoa au mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya, MUNGU atafuta hizo nguvu za giza na utakuwa huru.

■Kuna watu wamewekewa kichawi kitu kinaitwa roho ya kuharibu mimba, Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya  kwa kukuondolea hiyo roho ya kuharibu mimba au atamponya mwenzi wako wa ndoa au mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.

2 Samweli 22:20-22 " Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.  BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.  Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi MUNGU wangu."

 ■Kuna watu hawana nguvu za kiume ndio maana wameshindwa kuzaa katika ndoa zao,Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya au atamponya mwenzi wako wa ndoa au mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.

■Kuna watu ni tasa  yaani hawana uwezo wa kubeba mimba,  Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya kwa kukuondoalea utasa  au atamponya mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.

■Kuna watu ni wanaume wagumba yaani wasio na uwezo wa kuwatungisha mimba wake zao, Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya kwa kukuondolea ugumba  au atamponya mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.  

■Kuna watu wanaumwa magonjwa mbalimbali  na magonjwa hayo ndio yamewazuilia ama kushika mimba au kukaa na mimba ama kutungisha mimba n.k, Leo mwite JEHOVAH RAPHA, MUNGU mponyaji atakuponya au atamponya mwenzi wako wa ndoa au mtu yeyote unayemuombea katika maombi haya.

Nini ufanye katika maombi?

1. Tubia kwa YESU KRISTO dhambi zako zote ili uwe na uhusiano mzuri na MUNGU Baba hata aweze kukuponya.

Zaburi 103:3 "Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,"

2. Msihi MUNGU kama JEHOVAH RAPHA  ili aponye eneo lolote kuhusu uzao linalohitaji uponyaji wake(Litaje eneo hilo katika maombi)

Mwanzo 20:17 "Ibrahimu akamwomba MUNGU, MUNGU akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana."

Mfano hai ni Isaka alimuombea mke wake ili aponr utasa akapona.

Mwanzo 25:21 "Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba."

3. Jiombee uponyaji wa MUNGU na muombee mke wako au mume wako wa ndoa uponyaji wa MUNGU.

Yeremia 33:6 "Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli."

4. Kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO kataa roho ya utasa au ugumba.

Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya MWANA."

5. Omba MUNGU akuponye magonjwa yeyote kwenye mwili wako yaliyo na mchango katika kukuzuia kupata watoto katika ndoa yako.

Kumb 7:15 "Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao."

Ndugu yangu omba katika jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU wa Mbinguni. 
Omba kwa Imani na utamuona MUNGU wa Miujiza. 
MUNGU akubariki sana. 
By Peter Mabula. 
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. 
+255714252292
Ubarikiwe sana.

Comments