![]() |
Na Mwl Peter Mabula na Jemimah Mabula |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu nikujuze ujumbe wa Neno la MUNGU.
Siku Moja nikiwa katika maombi nilisikia sauti ikisema niombe juu ya kurudisha vilivyoibiwa na mawakala wa shetani kipepo na nifundishe pia somo ili watu waombe kurudisha vitu vyao vyema vilivyoibiwa kiroho, Nikapewa Andiko la Isaya 42:22.
Karibu sana.
Isaya 42:22 ''Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.''





Kuna walioibiwa ufahamu na mawakala wa shetani na leo watu hao ni vichaa maana ufahamu wao mzuri wameondolewa.
Bwana YESU leo anataka atende jambo jipya la kurudisha kitu chako kizuri kilichoibiwa kiroho, BWANA anangoja tu useme ''Narudisha vitu vyangu vilivyokuwa vimeibiwa, navirudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.''




Biblia inasema '' wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha''


Kuna watu japokuwa wana kazi nzuri lakini katika kazi hizo wanaishi kama watumwa, adui ameiba haki yao.


Biblia inasema '' wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha''




Kuna watu wakati huu lao ni kusema tu ''Nilikuwa tajiri sana zamani'' lakini hawaeelewi pesa yao ilipoteaje.
Mtu mmoja alipata neema ya kupelekwa mbinguni na kuonyeshwa mambo mengi ambayo Kanisa linatakiwa liyatendee kazi sana. Katika maagizo hayo mojawapo aliambiwa awaambie wateule kwamba kila kitu chao walichonacho, wanachotumia au wanachonunua ni lazima sana kukiombea na kukifutia maagano ya kipepo na kukifunika kwa damu ya YESU KRISTO.
Kuna watu kitendo cha kuwa tu karibu yako kinaweza kukuletea umasikini mkubwa.

Sio watu wote uwaonao ni wema, wengine wamembeba shetani kabisa na ukizubaa watakuachia maumivu makuu katika maisha yako.
Ndugu, kama huwa unaliona Kanisa kuwa adui yako nakuomba kuanzia leo anza kuliona Kanisa kama rafiki yako mkuu na nenda Kanisani ukaabudu, kufanya Maombi na kuombewa pia
Kama semina na mikutano ya Injili kwako unaiona kuwa si kitu napenda kukuambia MUNGU anaweza kupeleka huko hitaji lako la tangu zamani unaloombea na Mtumishi huyo anayeihubiri kweli ya KRISTO atakuombea na utashangaa sana kupata ushindi.
1 Kor 15:57 '' Lakini MUNGU na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu YESU KRISTO.''
Changamka leo katika maombi na maombezi ili kurudisha vitu vyako vilivyoibiwa na mawakala wa shetani.
Sio kila rafiki yako ni wa baraka, uwe makini sana maana shetani anao watoto wake wanaoweza kukuibia kabisa vitu vyako kiroho.
Mume anaweza kuibiwa akili zake kichawi na akawa kazi yake ni kumpiga tu mkewe wa ndoa bila hata kosa hata moja.
Mume anaweza kuibiwa akili yake njema na kuanza kutokujali familia yake na ndoa yake, mdada wa kazini anaweza kuwa chanzo kabisa cha kumwendea kwa mganga na kumuibia ufahamu.
Leo unaweza kukuta binti mdogo anayetumika kipepo amejenga nyumba nzuri kumbe kwa pesa za kuhongwa na mume wa mtu aliyeibiwa ufahamu.
Mama uliyeibiwa mume wako kiroho naomba leo ita jina la YESU KRISTO katika maombi ili kurudisha ufahamu wa mwanzo wa mume wako.
Baba ambaye unadhani kabisa mke wako kaibiwa ufahamu na vijana wadogo, urudishe ufahamu huo kwa maombi katika jina la YESU KRISTO.
Leo kuna mambo ya ajabu sana.
Unakuta kijana aliyesema jana jioni kwamba anampenda binti na anataka kumuoa lakini leo asubuhi tu anasema hamtaki binti huyo.
Mume aliyemwambia mkewe jana usiku kwamba ''i love you so much'' lakini ni huyo huyo leo asubuhi tu amempiga mkewe na kumvunja mguu au mkono, Ni hatari ndugu zangu.
Biblia inasema '' wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha''
1 Yohana 3:22-24 ''na lo lote tuombalo(MUNGU), twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake YESU KRISTO, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo ROHO aliyetupa. ''
Naamini sasa umeshajua ni kitu gani ambacho umeibiwa kiroho na mawakala wa shetani.
Kama mtaa wenu umeibiwa kiroho na wakuu wa giza kiasi kwamba mtaa mzima ni maskini tu basi rudisha leo baraka yako kwa jina la YESU KRISTO.
Kama ukoo wenu umeibiwa fahamu ndio maana kazi za wana ukoo wenu ni ulevi na uzinzi tu basi leo omba maombi ya kurudisha.
Kama sura yako imeibiwa ndio maana hakuna anayeweza kukubali aingie katika uchumba na wewe, basi leo kwa jina la YESU KRISTO rudisha baraka yako.
Kama afya yako imeibiwa ndio maana kila siku wewe ni kuumwa tu basi leo kwa maombi yako irudishe kwa jina la YESU KRISTO.
Kama akili yako imeibiwa ndio maana kiwango chako cha kufaulu kama zamani kimeondoka, basi leo kwa jina la YESU KRISTO rudisha ufahamu wako na jifunike kwa damu ya YESU KRISTO.
Inawezekana una kiwanja lakini kila ukipata pesa za ujenzi vinaibuka vikwazo na pesa hiyo inapotea tu.
Inawezekana kabisa hata kiwanja huna lakini pesa unayopokea inaweza kukunua viwanja viwili lakini shetani anakuibia pato lako , leo ita damu ya YESU KRISTO ya pasaka ikupe ushindi.
Biblia inasema '' wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha''
Zaburi 2:8 ''Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.''
Urithi wako unaweza kuibiwa hivyo urudishe leo kwa jina la YESU KRISTO.
Baraka yako iliyoibiwa irudishe leo kwa maombi yako na utashinda.
Furaha ya kwenye ndoa yako au familia yako iliyoibiwa irudishe leo kwa jina la YESU KRISTO.
Hapa chini ni ya MAOMBI YA KURUDISHA VILIVYOIBIWA KIPEPO
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake.
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini.
MAOMBI YA KURUDISHA VILIVYOIBIWA KICHAWI.
BABA wa mbinguni hakuna kama wewe.
Asante kwa kunilinda na kunipa nafasi hii ya kuomba mbele zako maombi utakayoyajibu wewe MUNGU Muumbaji wangu.
Katika jina la YESU KRISTO aliye hai ninarudisha mali zangu zote zilizoibiwa kipepo na majini, wachawi, washirikina, wakuu wa giza na waganga wote.
Ninairudisha afya yangu njema ya kuishi bila kuumwaumwa, Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninarudisha furaha iliyopotea katika ndoa yangu, kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha uchumba wangu uliokuwa unaelekea katika ndoa takatifu ila ukavunjika,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninarudisha mipango yangu mizuri ili ianze kutekelezeka,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha amani katika ndoa yangu au uchumba wangu,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha pesa zangu ambazo huibiwa kichawi na mawakala wa shetani,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha kuelewana katika ukoo wangu na familia yangu,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha amani kwa wazazi wangu wasioelewana,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha kupendwa na kukubaliwa kazini kwangu,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha ujuzi wangu ulioibiwa na shetani,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha kila baraka yangu iliyokuwa imeibiwa,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Narudisha kila mali yangu iliyokuwa imeibiwa kiroho,Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ujasiri wangu wa KiMUNGU uliokuwa umeibiwa naurudisha leo kwa jina la YESU KRISTO.
Huduma yangu iliyokuwa imeibiwa, Nairudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila kilicho changu ambacho ni baraka kutoka kwa MUNGU na adui wameiba, Narudisha kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kwa jina la YESU KRISTO ninaomba Eee MUNGU Baba Malaika wako ambao ambao hufanya kituo kwa wamchao wakuchao kama inavyosema Zaburi 34:7 waende wakakusanye kila baraka yangu iliyokuwa imeibiwa na mawakala wa shetani.
Malaika wako ambao ni roho watumikao kama inavyosema Waebrania 1:14, Nakuomba wakalete kila baraka yangu iliyokuwa imeibiwa.
Asanye JEHOVAH mwenye nguvu kwa kunishindia.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi,
Amen Amen.
MUNGU akubariki sana.
Endelea kuomba na utamuona MUNGU wa Miujiza.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
+255714252292
Ubarikiwe
Comments