MAOMBI YA KUSAMBARATISHA VIKAO VYA WANAOKUJADILI KWA MABAYA.


Na Mwl Peter Mabula



Bwana  YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze kisha tuombe.

Isaya 54:15 '' Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.''

 Neno la MUNGU linaonyesha kwamba wakati mwingine huwa kuna wanaokusanyika kwa ajili yako katika ulimwengu wa roho wa giza, Lakini ukiomba katika KRISTO YESU Hakika utashinda.

✔️Kila kitu kwako huwa hakifanyiki kwa ghafla tu bali huwa kuna mipango na mikakati iliyofanywa kwa ajili yako, mipango hiyo hufanyika katika vikao vya mawakala wa shetani, lakini ashukuriwe MUNGU kwa YESU KRISTO maaa leo tunasambaratisha vikao vyote vya wanaotujadili kwa mabaya.

Kazini kwako unaweza kuona viongozi wako wanakujadili ili wakufukuze kazi au wakusimamishe au wakushushe cheo. Kwenye kikao hicho utawaona wanadamu lakini naomba nikuambie kwamba hakuna jambo hata moja unaloliona katika ulimwengu wa mwili kama tu jambo hilo halikuanzia katika ulimwengu wa roho.

 ✔️Vitu vyote vinavyokutokea katika maisha yako huwa vinaanzia katika ulimwengu wa roho ndipo vinakuja kutimia katika ulimwengu wa mwili.

Unaweza ukawaona wanadamu wanakujadili kwa mabaya kazini kwako kumbe katikati yao liko jini linalowaelekeza cha kuongea na cha kuamua juu yako.
Unaweza ukashangaa tu kwamba unashushwa cheo au kufukuzwa wakati wewe ndio hufanya kazi vizuri na kwa uaminifu lakini wanaofanya kazi kwa ulegevu ndio unawaona wanapandishwa vyeo, siri iko katika ulimwengu wa roho.

✔️Kama huwezi kushinda katika ulimwengu wa roho na katika ulimwengu wa mwili huwezi kushinda pia.

Ashukuriwe MUNGU maana Neno lake linasema '' yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.''

 Uchumba wako unaweza ukajadiliwa na wachawi na kama utashindwa kuwadhibiti hakika uchumba huo utavunjika na kukuachia maumivu makubwa.

Ni mara nyingi sana MUNGU husema na wewe kwa ndoto na maono ili kukujulisha kile wanachokupangia adui zako lakini wengi hudharau ndoto hizo ambazo baadae zikitimia kujuta na kusema kumbe ile ndoto ilikuwa kweli.
Ndoa yako kwenyUchumba wako unaweza ukajadiliwa na wachawi na kama utashindwa kuwadhibiti hakika uchumba huo utavunjika na kukuachia maumivu makubwa.
Ni mara nyingi sana MUNGU husema na wewe kwa ndoto na maono ili kukujulisha kile wanachokupangia adui zako lakini wengi hudharau ndoto hizo ambazo baadae zikitimia kujuta na kusema kumbe ile ndoto ilikuwa kweli.
Ndoa yako kwenye kikao cha wachawi wanaweza wakapitisha maamuzi ya kwamba lazima ndoa hiyo iwe na migogoro kila siku.
Kujua huleta ushindi. Leo umejua haya ili ujue pia jinsi ya kupambana kiroho na ushinde.
Kwenye ndoto unaweza ukaona kabisa msimamo wa maadui zako lakini wengi huwa hawajui jinsi ya kupambana kimaombi, wengi hukimbilia kuwaambia watu kwamba wawaombee lakini watu hao husahau maana ni mambo ambayo hayana uzito kwao.
Ndugu nakuomba pambana mwenyewe kwa jina la YESU KRISTO na ushindi wako ni mkubwa sana baada ya kuyajua haya.
Pia nakuomba kila mara na kila siku omba ukiharibu vikao vya wote wanaokujadili katika ulimwengu wa roho wa giza.
Ukikivuruga kikao cha mashetani wanaokujadili hakika walichokusudia kwako ndio kitakuwa kimeishia hapo.
Kwa maombi ya leo hata vikao vya wachawi vya mwezi ujao au mwakani unaweza kuvisambaratisha.
Ukiwa ni mtu unayeishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO na ukawa muombaji hakika utakuwa mtu hatari katika ulimwengu wa roho. Wakati mwingine mawakala wa shetani kila wakitaka kukujadili tu watajikuta wanasahau au viti vinawaka moto na wanahairisha kikao hicho,  kikao cha wachawi wanaweza wakapitisha maamuzi ya kwamba lazima Ndoa hiyo iwe na migogoro kila siku.

◾Kujua kunaleta ushindi.

 Leo umejua haya ili ujue pia jinsi ya kupambana kiroho na ushinde.

Kwenye ndoto unaweza ukaona kabisa msimamo wa maadui zako lakini wengi huwa hawajui jinsi ya kupambana kimaombi, wengi hukimbilia kuwaambia watu kwamba wawaombee lakini watu hao husahau maana ni mambo ambayo hayana uzito kwao.
Ndugu nakuomba pambana mwenyewe kwa jina la YESU KRISTO na ushindi wako ni mkubwa sana baada ya kuyajua haya.
Pia nakuomba kila mara na kila siku omba ukiharibu vikao vya wote wanaokujadili katika ulimwengu wa roho wa giza.
Ukikivuruga kikao cha mashetani wanaokujadili hakika walichokusudia kwako ndio kitakuwa kimeishia hapo.

Kwa maombi ya leo hata vikao vya wachawi vya mwezi ujao au mwakani unaweza kuvisambaratisha.

Ukiwa ni mtu unayeishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO na ukawa muombaji hakika utakuwa mtu hatari katika ulimwengu wa roho. Wakati mwingine mawakala wa shetani kila wakitaka kukujadili tu watajikuta wanasahau au viti vinawaka moto na wanaarisha kikao hicho.

 Nadhani umewahi kuona baadhi ya ajenda katika vikao zikiarishwa na kupangiwa siku nyingine kwa sababu tu ya uzito wa ajenda hizo. Kwa mwanamaombi halisi anayemcha MUNGU katika KRISTO ajenda zote zinazokuhusu wewe adui zako wanaweza kujikuta wanaahilisha kila mara hadi miaka inapita hakuna kilichokupata.

Maadui zako katika ulimwengu wa roho wa giza hukaa vikao ili kukujadili na kukuwekea mikakatai ya kukuharibia au kukuangamiza.

Maadui zako hukaa vikao ili kukujadili unaendeleaje kiroho.

Maadui zako hujadili watakuharibiaje uchumi wako, kazi yako au biashara yako.
Hukusanyikana katika vikao ili kuhakikisha mipango yako haiendi.
Maadui zako wanaweza kukaa vikao ili kupanga mikakati ya kukuharibia muujiza wako, uchumba wako au ndoa yako au baraka yako.

Maadui zako wanaweza kukaa vikao kwa ajili ya kuchunguza asili ya nguvu zako na ili wafanye mpango wa kuhakikisha nguvu zako za kiroho zinaondoka kwako.
Hebu ona kikao hiki kilichokuwa kinamjadili Samsoni ili wajue asili ya nguvu zake ili wapate kumwangamiza.

 Waamuzi 16:5 '' Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja. '

Wafilisti kama maadui wa samsoni walikaa kikao na Delila mkewe Samson ili tu kujua asili ya nguvu za samson, kwenye kikao hicho walipanga hadi kiwango cha pesa ili tu kumpa Delila kama atawafanikisha mpango wao.

Hata wewe mmoja wa rafiki zako wa karibu au ndugu yako anaweza akaitwa katika kikao cha wabaya wako ili wajue jambo fulani kuhusu wewe ili wakumalize kwa urahisi.

Wachawi wanaweza kukaa kikao kwa ajili yako ili kuhakikisha hufanikiwi.

Kuna mtu anaweza kwenda kwa waganga kwa ajili yako, huko kwa mganga atakaa kikao na mganga ili kukujadili kwa lengo la kukudhuru au kukuharibia.

Unaweza kuwa ni mwanafunzi mwenye akili nzuri lakini adui yako anakwenda kwa waganga na kufanya kikao ili kuharibu ufahamu wako. 
✔️✔️Leo sambaratisha vikao vyao.
Inawezekana jina lako hupelekwa kwenye vikao vya mashetani kila mara.
[8/16, 12:00 PM] Mwl Peter Mabula: ✔️Dalili moja wapo ya mtu jina lake kutajwa kwenye madhabahu za giza ni kusisimka nywele au mwili wote ghafla bila tatizo, wakati mwingine kutajwa kwa jina la mtu katika madhabahu za wachawi hukosa amani ghafla moyoni mwake.

 ✔️✔️Ndugu yangu ukiona vitu kama hivyo omba kwa imani kwa jina la YESU KRISTO ili kuharibu vikao vyote vya wanakujadili kwa hila, wasambaratishe kwa damu ya YESU na kwa moto wa ROHO MTAKATIFU, liite jina la YESU na utashinda. kataa kila kusudi baya dhidi yako.

◾Haribu vikao vya wanaoijadili biashara yako kwa hila.

◾Vunja vikao vyote vya wachawi wanaoijadili afya yako. 
Kuna watu wanaumwa ukimwi lakini ni ukimwi wa kutengeneza na mashetani tu, ndugu ni muhimu sana kuharibu vikao vyote vya wanaokujadili kwa mabaya.
Inawezekana kabisa wanapanga ufe au wanapanga upooze.
Inawezekana kabisa wanapanga uzeeke bila kuolewa.
Inawezekana kabisa wanapanga kwenye vikao vyao vya giza kwamba kila mwaka uwe unafiwa tu.
Inawezekabisa wanaiwekea mipaka familia yenu ili mtu akifanikiwa tu kidogo afe.

✔️✔️Leo vunja vikao vyote vya wanaokujadili.
[8/16, 12:02 PM] Mwl Peter Mabula: Asante kwa kunielewa na leo omba sana ukiharibu vikao vyote vya mawakala wa shetani dhidi yako.

✔️Haribu vikao vyote vya shetani vinavyokujadili.

✔️Haribu silaha zote za shetani zilizopitishwa kwenye vikao vya kichawi na kiganga.

✔️Vunja kila ulimi na kinywa kilichokujadili kwa hila.

✔️Vunja vikao vyote vya maadui zako wa sirini.

✔️Vunja vioo vyote vya wachawi unavyoonekana wewe kwao.

✔️Haribu TV zote za kichawi na kamera za kichawi zinazokumulika na kukuona.
MUNGU Baba  anasema
 ''Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.-Mika 5:9 ''

Hapa chini ni  ya MAOMBI YA KUSAMBARATISHA VIKAO VYA WANAOKUJADILI KIPEPO.

Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake.
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini.


MAOMBI YA KUSAMBARATISHA VIKAO VYA WANAOKUJADILI KIPEPO.

YAHWEH MUNGU uliye hai ninakushukuru na kukuabudu BWANA.

 Asante kwa uzima wako kwangu na asante kwa nafasi hii ya kuomba mbele zako maombi muhimu ya kuniletea ushindi wangu leo. 

Nakushukuru MUNGU wangu kwa ufunuo huu wa leo.

Niko mbele zako MUNGU wangu nikivunja vikao vyote vya siri wanavyokaa maadui zangu ili kunijadili.

Nasambaratisha vikao vyote vya watu wabaya wanaoijadili kazi yangu na biashara yangu. 

Niko kinyume na vikao vyote vya wachawi dhidi yangu na navifuta leo na kuvisambaratisha  kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote washirikina wanaokaa kwa ajili yangu,Nasambaratisha  kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya watu walioniendea kwa waganga wa kienyeji, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya wasionitakia mema, Nasambaratisha kwa  jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya wachawi wanaotaka kuharibu uchumba wangu/ndoa yangu, Nasambaratisha  kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya wanadamu wanaotumika kipepo dhidi yangu, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha kila aina ya vikao vya siri vya giza, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao mapepo vilivyokaa baharini au porini,Nasambaratisha  kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya wachawi vya mchana na usiku, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha kila vikao vinavyopanga kunifelisha, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaritisha vikao vyote vya kupanga ajali na mikosi na balaa, Nasambaratisha  kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambatisha mchawi na uchawi wake, Nasambaratisha  kwa jina la YESU KRISTO.

nasambaratisha mganga wa kienyeji na uganga wake, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambatisha mshirikina na ushirikina wake, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha mkuu wa giza na giza lake, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya kunipangia kuumwa, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nsambaratisha vikao vyote vya kuniletea misiba, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Nasambaratisha vikao vyote vya giza vya kuniletea madeni, Nasambaratisha kwa  jina la YESU KRISTO.

Nasamabatisha vikao vyote vya kuniletea ajali na balaa, Nasambaratisha kwa jina la YESU KRISTO.

Asante MUNGU BABA mwenyezi kwa kunipa ushindi leo.
Asante Bwana YESU maana damu yako na jina lako vimenishindia.
Asante ROHO MTAKATIFU maana katika wewe nimeshinda.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
Amen Amen.
MUNGU akubariki sana.
Omba sana katika jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU wa Miujiza.
MUNGU akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments