MUNGU ATANIOKOA NA MKONO WAKO MFILISTI.

Na Mwl Peter Mabula 

 

MUNGU ATANIOKOA NA MKONO WAKO MFILISTI.

Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la kutufanya tuombe na tushinde.
Ni ujumbe mfupi lakini ujumbe huu utakuwa msaada kwa Mtu aliyekusudiwa.

✓✓Usimchekee mfilisti anayetaka kukuangamiza Bali omba maombi makali kumhusu ili ajue kwamba wewe una JEHOVAH MUNGU wako.

1 Samweli 17:37A " Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu."

Nani amekuwa mfilisti kwako hata anataka kukuangamiza?

Nani anataka kuangamiza ajira yako?

Nani anataka kuangamiza ndoa yako na uzao wako?

Je mchawi anajisifu sana kwamba amekuroga usiolewe au usioe au usizae au usipate kazi?

✓✓Leo Mwambie huyo kwamba " MUNGU ataniokoa na mikono yako ewe mfilisti"

✓✓Kama unataka kufukuzwa kazi kwa sababu ya tamaa ya mfanyakazi mwenzako aliye juu yako, Leo omba kwa Imani ukisema "MUNGU ataniokoa na mikono yako ewe mfilisti "

Nani anataka akufanye uwe kichaa?

Nani anataka akufanye tasa?

Nani anataka akufanye uonekane unanuka katika jamii?

Nani anataka akufanye uonekane sio lolote?

Wewe pambana kiroho na wakala huyo wa shetani.

Omba kwa Imani kama Daudi aliyesema "MUNGU ataniokoa na mikono ya mfilisti huyu"

✓✓MUNGU aliyekulinda tangu utotoni mwako anaweza kukuokoa dhidi ya anayekufanyia hila za kichawi ili ukataliwe.

✓✓MUNGU anaweza akakuokoa na anayekuwangia kila siku.

Amuru mapigo kwa wachawi wote wanaokuroga, amuru kwa njia ya maombi katika jina la YESU KRISTO.

Omba MUNGU awaangamize wafilisti wako wote.

Wafilisti wako ni pamoja na.

1. Majini.

2. Mizimu.

3. Roho za kichawi.

4. Vitendea kazi vya waganga.

5. Roho za kishirikina.

6. Wakuu wa Giza.

7. Wanadamu wanaotumika kipepo ili kukuangamiza.

Kwepa laana zao kwa maombi.

✓✓✓Mkimbilie Bwana YESU KRISTO ili akufanye uwe salama.

Omba na viapo vyao vya kipepo vitawarudia wao.

Omba na hila zao zitawarudia wao.

Wambie kwamba MUNGU kwako ni MUNGU wa kukuokoa.

Usiwahurumie maana watakuangamiza hivyo kata rufaa mbinguni ilia Bwana YESU akushindie.

Zaburi 68:20 "MUNGU kwetu sisi ni MUNGU wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, MUNGU atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa."

Wakikutisha wambie kwamba

"MUNGU ataniokoa na mikono yako ewe mfilisti "

Omba ndugu na hata ukisikia kufunga basi funga na MUNGU wa mbinguni atakushindia.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Whatsapp, Maombezi, Ushauri na sadaka ya kuipeleka Injili mbele)
Ubarikiwe sana

Comments