OLE WAKE YEYE AMPAYE JIRANI YAKE POMBE.

Na Mwl Peter Mabula

 



Habakuki 2:15 "OLE WAKE YEYE AMPAYE JIRANI YAKE KILEO, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!"

Ole ni nini?

Ole ni tamko la kuelezea mapigo,majuto na masikitiko.

Hivyo ole imebeba mapigo, majuto na masikitiko.

Unapoambiwa na Neno la MUNGU kwamba "Ole" maana yake usipogeuka na kuacha kitu hicho kibaya tarajia kupata mapigo, majuto na masikitiko.

Sasa Neno la MUNGU leo linasema ole wake ampaye mtu pombe, ndio maana ya hilo andiko hapo juu.

✓✓Ole wako wewe unayempa mtu pombe.

✓✓Ole wako wewe unayejenga bar ili watu waje hapo kunywa pombe na kupanga dhambi au kuchochea dhambi, hasa uzinzi.

✓✓Ole wako wewe ambaye unatoa kiwanja chako huku ukijua ili tu watu wajenge sehemu ya kuuzia pombe.

✓✓Ole wako wewe Bamedi au mhudumu wa kugawa pombe Bar.

✓✓Ole wako wewe muuzaji wa pombe.

✓✓Ole wako wewe mtengenezaji wa pombe.

✓✓Ole wako wewe mhubiri mlevi unayedanganya watu kwamba wanywe tu pombe hakuna tatizo, na kumbe unawafundisha hivyo ili upate wanachama wa kukusapoti katika ulevi wako.

✓✓Ole wako wewe mtu wa Kanisa unayefanya sherehe na watu wabaya wanakushawishi kwamba pombe ziwepo na wewe unakubali.

✓✓Ole wako wewe ambaye kila siku unatumwa pombe madukani na unapeleka.

✓✓Ole wako wewe msambazaji wa pombe.

✓✓Ole wako wewe ambaye nyumbani kwenu friji imejaa pombe na wewe kila siku unatumwa pombe kwenye friji na unaenda.

Ole wako wewe umpaye jirani yako pombe.

Habakuki 2:15 "Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!"

Na hilo ndilo Neno la MUNGU.

Mwenye sikio la kiroho la kusikia na asikie leo na kuacha dhambi inayohusu pombe.

YESU KRISTO anaokoa hivyo ukimwamini na kumpokea leo unaokoka.
MUNGU akubariki.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.

Comments