UWE MWANGALIFU UNAPOOTA NDOTO

Na Mwl Peter Mabula

 

✓✓Uwe Mwangalifu Pale Unapoota Ndoto Maana Kuna Ndoto Ni Mwongozo kwako ili usaidike.

Ukiudharau mwongozo huo unaweza ukakwama au ukachelewa kupata baraka unayoitaka.

MUNGU Analinda Kila Kilicho Chako Katika Dunia Hii Ili Shetani Na Malaika Zake Waovu Wasije Kuharibu Kile MUNGU Ameweka Mbele Yako, ndio maana baadhi ya vitu anakujulisha kwa ndoto.

Hebu Fikiria Kuhusu Farao Mfalme Wa Misri, Ingekuwa Vipi Kama MUNGU Asingemletea Ndoto?

Mwanzo 41:1-4 " Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka."

Mbele ya Farao na Wamisri kulikuwa na miaka 7 ya kufuna Sana Kisha miaka 7 ya njaa kali.

Kama Mfalme wa Misri asingeota ndoto na kujua Nini afanye Wangekufa Kwa Njaa Karibu Nchi Nzima.

Ingekuwaje Kama MUNGU Asingemfanya Yusufu Kuwa Mfasiri Wa Ndoto?

Mwanzo 41:25-27 " Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; MUNGU amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa."

Yusufu asingetafasiri ndoto hiyo wangekufa kwa njaa.

Yusufu asingetafasiri ndoto hiyo pengine Angefia Gerezani.

Ndoto Zina Nguvu Na Kwa Jinsi Hiyo MUNGU Huwasiliana Na Watu wake wakati mwingine kwa ndoto, hivyo usidharau kila ndoto.

MUNGU akubariki.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Comments