DHAMBI ISIYOTUBIWA INAWEZA KUZUIA KUJIBIWA MAOMBI.

 

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai 

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Karibu ujifunze kitu kupitia ujumbe huu mfupi.


✓✓Dhambi isiyotubiwa inaweza kuwa kikwazo kikubwa cha mtu kujibiwa maombi yake.


✓✓Dhambi ni uasi kwa MUNGU, ndivyo maandiko yasemavyo, na uasi huo inaweza kumfanya mtu  asijibiwe maombi yake hata kama ni muombaji sana.


Toba ya kweli ni jambo la muhimu sana ili mahitaji yako yajibiwe na MUNGU.


1 Yohana 1:8-10 " Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.  Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu."


✓✓Kutubu ndiko kumruhusu MUNGU akuangalie hata kukutendea mema.


Ndugu, dhambi isiyotubiwa inaweza kuzuia maombi yako hata kama unaomba sana sana.


Inahitajika sana toba kwa mtu wa namna hiyo ili ndipo mema aliyoyahitaji kwa MUNGU yaje.


Matendo  3:19 " Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"


MUNGU akubariki.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Comments