JINSI YA KUACHA DHAMBI SUGU ZINAZOKUSUMBUA.

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Iko wazi sana kwamba watenda dhambi wote wasiopata neema ya kutubu sehemu yao hao ni jehanamu.

1 Wakorintho 6:9-10 " Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."

Hivyo ukitaka usiende jehanamu ndugu mpokee YESU KRISTO, tubu na kuacha dhambi zako zote.

Sasa kama kuna dhambi inakusumbua, umefanya siri sana na umejaribu kuiacha lakini hujaweza kuiacha, ndugu ni wazi kwamba watenda dhambi kama wewe sehemu yao ni jehanamu.

Lakini ukiamua leo kuokoka na kutubu na kuacha dhambi zote kuanzia leo makazi yako jehanamu yanafutwa na makazi yako sasa yanakuwa mbinguni ambako Bwana YESU KRISTO huwatengenezea wateule wake Makazi.

Yohana 14:2-3 " Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo."

Ndugu yangu, usikubali kujifariji kwenye dhambi yeyote bali tubia dhambi hizo na kuziacha.
Mimi Mwl Peter Mabula Nimekuandalia baadhi ya njia za kukusaidia kuiacha dhambi sugu inayokusumbua, fanyia kazi points hizi 11 zote bila kuacha hata moja na utakuwa mshindi dhidi ya dhambi.

1. Mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako ili utakaswe na kufanyika mtoto wa MUNGU.

Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;"

2. Tubia dhambi hizo na kuziacha.

Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"

3. Jitenge na marafiki wabaya waliokusaidia mwanzo wewe kuingia dhambini.

Zaburi 1:1" Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha."

4. Hakikisha unakuwa mhudhuliaji wa kila

kipindi cha ibada Kanisani kuanzia katikati ya wiki na jumapili pia.

Waebrania 10:25 "wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."

5. Tendea kazi Neno la MUNGU unalofundishwa Kanisani.

Mathayo 7:24,26 " Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; ..... Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;"

6. Uwe muwazi kwa Baba yako wa kiroho ili akusaidie kwa ushauri na maombi.

Waefeso 4:11-12 " Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; KWA KUSUDI LA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa KRISTO ujengwe;"

7. Jiunge na kundi la maombi Kanisani na hakikisha unakuwa muombaji maana kazi mojawapo ya maombi ni kuutiisha mwili ili tamaa zisikusumbue.

1 Wathesalonike 5:17 "ombeni bila kukoma;"

8. Amua kuwa kiumbe kipya kisicho husika na dhambi maana ukiwa na nia hiyo ROHO

MTAKATIFU atakuja kwako na kukusaidia jinsi ya kuishi ili ubaki katika utakatifu.

2 Wakorintho 5:17 "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya."

9. Jiunge na huduma Kanisani ili jambo hilo

likusaidie kuwa busy na huduma na kwa kuwa kwenye huduma kutakusaidia wewe kuwa kwenye mtandao mkubwa wa kuombewa mara kwa mara na wana Kanisa.

Matendo 2:46-47" Na siku zote kwa moyo mmoja WALIDUMU NDANI YA HEKALU, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha NA KWA MOYO MWEUPE, WAKIMSIFU MUNGU, na kuwapendeza watu wote. BWANA akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa."

Mfano ukijiunga na kwaya itakuwa kwako rahisi kuombewa maana wanaoombea huduma za Kanisani ni wengi.

10. Sahau mambo ya nyuma na yafute kabisa kwenye akili yako ili yasikufanye ukose ujasiri wa kuendelea mbele.

Isaya 43:18 "Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani."

11. Hakikisha unakuwa kielelezo cha matendo mema.

2 Timotheo 1:13-14 " Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika KRISTO YESU. Ilinde ile amana nzuri kwa ROHO MTAKATIFU akaaye ndani yetu."

Ndugu yangu, hakikisha unazishinda dhambi zote.

Kumbuka siku ya mwisho itakuwa.

Mathayo 13:41-43 '' Mwana wa Adamu

atawatuma malaika zake, nao watakusanya

kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika

tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Ndipo wenye haki watakapong'aa kama jua katika ufalme wa BABA yao. Mwenye masikio, na asikie. ''

Na kama ukifanya kwenye dhambi hiyo Biblia inasema hivi.

Waebrania 9:27 "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;"

Hivyo hakuna mwanadamu yeyote yule duniani anayeweza kukuombea ukatoka jehanamu ukaenda Mbinguni.

Kama yuko mtu aliyekudanganya hivyo nakuomba muone tu mtu huyo kama tapeli au wakala wa shetani anayetaka usitubu sasa na kuacha dhambi kwa ajili ya uzima wa milele.

Ndio maana Biblia siku zote inatushauri

kwamba 'Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;-Matendo 3:19 ''

Hivyo Hakikisha ndugu unaziacha dhambi zote ukiwa hai.

Hakikisha unazishinda dhambi zote ikiwemo na hiyo dhambi sugu inayokusumbua.
MUNGU akubariki.
By Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe utakayefanyia kazi ujumbe huu na ukaacha dhambi zote.

 

Comments