MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ILI AFANYE JAMBO JIPYA.

Mwl Peter Mabula na Jemimah Mabula 
 


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU na kisha tuombe maombi ya ushindi sana.


Wakati huu tunamuomba MUNGU afanye jambo jipya katika maisha yetu.


Kama magonjwa yalitutawala leo MUNGU Baba anafanya jambo jipya kwa kuleta uponya wake.


Isaya 43:19 ''Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.''


 MUNGU wetu anaenda kufanya jambo jipya, Hata baraka ambazo tuliziona haziwezekani kwetu leo kwa maombi yetu kupitia jina la YESU KRISTO tunaenda kufanikiwa.


Kwanini MUNGU afanye jambo jipya?


●Ni kwa sababu '' hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.-Luka 1:37''


Kwanini JEHOVAJ MUNGU wetu atende jambo jipya?


Yeye MUNGU anakuuliza wewe akisema ''Tazama, mimi ni BWANA, MUNGU wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? -Yeremia 32:27 "

Kwa sababu MUNGU wetu anaweza yote basi hakika kwa maombi yako ya imani na utakatifu kupitia jina la YESU KRISTO anaenda kufanya jambo jipya kwako ambalo ulidhani haliwezekani.


Kutoka 23:25 "Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako."


Kwanini MUNGU afanye jambo jipya?


Ni kwa sababu yeye yuko juu ya vyote na juu ya wote.


Biblia inamthibitisha MUNGU wetu kwamba;


''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.-Zaburi 83:18''


Kama aliponya magonjwa yote

Mathayo 9:35 ''Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, NA KUPONYA MAGONJWA YOTE  na udhaifu wa kila aina.''


Sio kwamba aliponya magonjwa fulani tu bali magonjwa yote.


Unateswa na kaugonjwa gani hata usipone?


Ukimwamini Bwana YESU na ukampokea na kuanza kuishi maisha matakatifu hakika uponyaji wake utakuwa mali yako hata kama ulidhani hutapona.


Kama aliponya magonjwa yote atashindwa nini kutengeneza jambo jipya kwako?


Mimi Peter Mabula juzi Nilikuwa namuombea rafiki yangu mmoja kwa simu kutokea Kilimanjaro ndipo niliposikia sauti ya ROHO MTAKATIFU ikisema kwamba niombe  juu ya MUNGU kutenda jambo jipya kisha akanipa ujumbe huu ili nikufundishe wewe na uombe maombi ya ushindi ukiliendea hitaji lako.


Siku hiyo kwa simu kwa muda wa masaa mawili kamili niliombea watu wengi na wengine katika hao walinishuhudia usiku ule ule kile ambacho MUNGU ametenda katika mahitaji yao waliyonishirikisha.


Hakika MUNGU alifanya jambo jipya katika afya zao na katika mahitaji mengine.


Ni kweli mama yangu umeteseka sana na magonjwa lakini jambo jipya atakalolifanya Bwana YESU kwako ni kukupa uponyaji.


Hayo magonjwa uliyoyaona tangu miaka mingi hutayaona tena yakiwa katika mwili wako. Mwamini tu Bwana YESU na Neno lake na hakikisha huigizi kwa MUNGU bali umeamua kabisa kuishi maisha matakatifu katika Bwana YESU.


Ni kweli umekuwa tasa muda mrefu sana sana JEHOVAH mwenye nguvu anaenda kukubariki uzao.


Ulidhani tumbo lako halitatoa mtoto na hadi mumeo akawa anakujeruhi kwa maneno yake, lakini wakati huu BWANA anaenda kutenda jambo jipya kwa kuwabariki uzao uliobarikiwa.


 Ni kweli familia yenu imekuwa na matatizo mengi sana lakini kwa maombi yako ya leo kupitia  jina la YESU KRISTO, MUNGU BABA anaenda kufanya jambo jipya kwa kuwapa ushindi, furaha na amani.


Inawezekana kabisa kila mwaka katika ukoo wenu mnazika, hadi  wakati huu mmeanza kufikiri ni zamu ya nani kufa mwaka huu. Habari njema ni kwamba Bwana YESU kupitia maombi yako anaenda kufanya jambo jipya la kuondoa vifo visivyo mpango wa MUNGU. Mtatimiza miaka ya ahadi kwa jina la YESU KRISTO.


Kufa tutakufa wote lakini sio kufa kwa mpango wa shetani na mawakala wake, leo omba utashinda hakika kwa jina la YESU KRISTO.


Kama aliumba mbingu  na dunia kama inavyosema Biblia katika Mwanzo 1:1 '' Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi.'' 


Je atashindwa nini kukuponya hako ka ugonjwa kanakokusumbua? Leo omba hakika utashinda.


Katika maombi haya  omba ukitumia  ufunuo huu wa kumwambia MUNGU atende jambo jipya, hakika utashinda.


Kama wachumba wanakuacha kila ukipata, hakika wakati huu utapata mchumba na utafunga ndoa kanisani, omba tu na dumisha utakatifu.


Kama watu wote wanajua kwamba wewe haiwezekani kuolewa, hakika wakati huu utaolewa na utazaa watoto wa kiume na wa kike kwa utukufu wa MUNGU.


Kama watu wanadhani hutapata kazi hakika kupitia ufunuo huu dai kazi yako kwa MUNGU na utapata kazi hiyo, mkumbuke tu MUNGU kupitia kazi hiyo atakayokubariki.


Wanaopanga ufukuzwe kazi, watafukuzwa wao baada ya kuomba maombi haya ya ufunuo huu wa kumwambia MUNGU afanye jambo jipya katika kazi yako.


MUNGU BABA anasema leo kwamba;


''Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.   -Yeremia 29:12''


 BWANA wa majeshi leo anaenda kufanya jambo jipya kupitia maombi yako katika KRISTO YESU.


 Mambo haya matatu yazingatie.


1. Utakatifu tu ndilo jambo muhimu kwako kuanzia leo.


 2. Wokovu wa KRISTO tu ndilo jambo special utakalotakiwa kulishika siku zote.


3. Kuomba kwa imani katika KRISTO leo kutafanya jambo jipya kwako.


Kama wachawi hawajawahi kukukimbia leo watakimbia wote kwa jina la YESU KRISTO.


Ni kweli mama umeteseka miaka mingi katika ndoa yako, lakini Bwana YESU KRISTO anaenda kutenda jambo jipya la kukupa furaha ya kudumu.


 Ni kweli ndugu yangu umeteseka sana na magonjwa  lakini leo Bwana YESU KRISTO anaenda kufanya jambo jipya .


Kama kwa miaka mingi watu walikuona wa hivi hivi, leo hutakuwa wa hivi hivi bali utakuwa mbarikiwa.

Mimi Peter Mabula Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kueleea naamini  ameelewa .

Hapa chini ni MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ILI AFANYE JAMBO JIPYA.

Maombi haya ni kwa ajili ya mtu ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba.


Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.


MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ILI AFANYE JAMBO JIPYA.



BABA katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai. 


Ninakushukuru kwa kunilinda na kunipa neema ya kuishi.


Pokea sifa na heshima MUNGU wangu uliyeziumba mbingu na nchi.


Neno lako linasema kwamba unaweza ukatenda jambo jipya.

Biblia katika Isaya 43:19  kwamba ''Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.''


Eee YAHWEH MUNGU wangu nakuomba fanya jambo jipya katika afya yangu kwa kuniponya.


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kuuponya mwili wangu unaoumwa.


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kuondoa kitu ambacho hutembea ndani ya mwili wangu. 


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kuuponya uchumi wangu na uzao wangu.


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kuiponya ndoa yangu na kuipa watoto wa kiume na wa kike.


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kuiponya familia yangu dhidi ya corona na dhidi ya magonjwa mengine yote.


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kunipa kibali na ushindi dhidi ya mawakala wote wa shetani. 


Nakuomba MUNGU Baba fanya jambo jipya kwa kuniepusha na kila mipango ya kipepo yote. 


Neno lako MUNGU Baba linasema "hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.-Luka 1:37''


Nakusihi BWANA niponye na iponye familia yangu.


Nakuomba MUNGU Baba nijaalie kuingia katika ndoa takatifu. 


Nakuomba MUNGU Baba nijaalie kupata kazi.


Kila haki yangu ninayoidai nakusihi Eee MUNGU Baba mweza yote uniwezeshe kuipata haki yangu hiyo.


Ni kweli kabisa madaktari walisema naumwa sana lakini wewe MUNGU Baba unaweza kufanya jambo jipya kwa kuniponya, nakusihi BWANA  uniponye kwa nguvu zako.


Kuna mahali wanadamu wananikatisha tamaa kwamba haiwezekani,  kuhusu ndoa, uzao, uchumi,  biashara,  kufaulu masomo, kupona n.k lakini neno moja tu ninalofahamu ni kwamba MUNGU Baba wa Mbinguni wewe  uko juu ya yote unaweza kunifanikisha hata pale ambapo kibinadamu palikuwa hapawezekani.

Neno lako linakuthibitisha katika Zaburi 83:18 kwamba "Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.''


Wewe MUNGU Baba uliye juu ya yote naomba unisaidie, uniwezeshe na kunishindia katika afya, uzao, kibali na uchumi.


Zaidi ya yote nakuomba MUNGU Baba unipe maisha marefu yenye furaha, baraka na amani.

Nakushukuru sana MUNGU Baba maana jambo ambalo lilikuwa haliwezekani kwa kibinadamu wewe unaliweza na utanitendea.

Nakushukuru sana MUNGU Baba wa Mbinguni maana umetenda sasa jambo jipya kwangu.

Ni katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai nimeomba na kupokea.

Amen amen  Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen. 


Hakika umeshinda. 

MUNGU akubariki sana. 

Nakuomba endelea kuomba na ongeza zaidi Maombi. 

By Peter Mabula. 

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. 

+255714252292.

Ubarikiwe

Comments