MAOMBI YANGU MIMI PETER LEO KWA AJILI YA MARAFIKI ZANGU WOTE KOKOTE WALIKO.

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Ee MUNGU Baba mwenye enzi na Utukufu, nakushukuru kwa ajili ya nafasi uliyompatia mtoto wako huyu uliyemuumba kwa upendeleo na makusudi ya kuvitawala vyote ulivyoviumba , sawasawa na Mwanzo 1:27 inayosema "MUNGU akawabarikia, MUNGU akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Kwa utukufu ule ule uliokuwa nao tangu awali, umjalie maisha mema ya kukupendeza, umwokoe na mashambulizi ya pepo wabaya na umkinge mbali na Kila mitego yote ya ibilisi aliye baba wa uongo na mshitaki wake, kwa Jina la YESU KRISTO, hati yake ya mashitaka naiondoa, na kutubu kwaajili yake Ee BABA.
Naomba Rehema zako ziwe juu yake BABA na msamaha wako umfunike kwa uweza wa Jina la YESU KRISTO.

Umuone huyu anayetafuta mwenza wa ndoa, afanikiwe kea jina la YESU KRISTO Mwokozi.

Na huyu anayetafuta kazi Ee BWANA umpatie kwa wingi wako na maarifa yako.
Nakusihi Eee BWANA uinusuru ndoa ya huyu iliyo kwenye tatizo, na kwa jina la YESU KRISTO umpatie watoto mwanandoa huyu anayehitaji watoto kwenye ndoa yake.

Eee MUNGU Nakusihi zikumbuke ahadi zako za kuwabariki uzao, kwa Jina la YESU KRISTO.
Eee MUNGU Nakusihi umletee msaada wako kutoka mbinguni mgonjwa huyu anayeumwa, na huyu aliyekata tamaa umpe tumaini jipya Kwa Jina la YESU KRISTO.
Anayehitaji kazi eee Bwana YESU KRISTO nakusihi umjalie kupata kazi nzuri.

Mkumbuke kijana huyu wa kike na wa kiume katika masomo yake anayesoma, mpe afya njema na amani yako itawale daima kwa Jina la YESU KRISTO.
Asante MUNGU Baba maana wewe ni MUNGU wa karibu na sio MUNGU wa mbali.
Namuombea huyu afanikiwe katika mahitaji yake yote aliyokuhitaji wewe kwayo.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba, kuamini na kupokea.
Amen Amen Ameeeeeeeeeeen.

MUNGU akubariki na kukulinda.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe

 

Comments