MUNGU ANATAKA NINI KWAKO.

 

Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe sana Ndugu yangu.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU.

Unajua MUNGU Siku zote anataka nini?

       1.   MUNGU anataka uokoke na ubaki kwenye wokovu wake.

Yohana 3:16-18 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda

ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. '' 

       2.   MUNGU anataka uishi maisha matakatifu siku zote.

1 Petro 1:15-17 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. ''

       3.    MUNGU anataka  uishi kwa matendo mema.

Waefeso 2:10 ''  Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo. ''

      4.    MUNGU anataka usiipende dunia na machukizo yake. 

1 Yohana 2:15-17 '' Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ''

      5.    MUNGU anataka uenende kwa  ROHO wake na kuongozwa na ROHO wake.

■Kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.

Warumi 8:14 '' Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

 ■Kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU.

Wagalatia 5:16 ''Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.   '' 

      6.   MUNGU anataka usitende dhambi maana dhambi ina madhara makubwa.

1 Kor 6:9-11 '' Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la BWANA YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu. ''

       7.   MUNGU anataka umpe heshima yake siku zote maana ni  BABA Mzazi wa roho yako. 

Zaburi 29:1-2  ''Mpeni BWANA, enyi wana wa MUNGU, Mpeni BWANA utukufu na nguvu; Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni BWANA  kwa uzuri wa utakatifu.'' 

Tumpe MUNGU utukufu wake hata baada ya kutendewa muujiza na yeye.

Luka 17:17-19  '' YESU akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa MUNGU utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa. ''

Ndugu yangu, naamini kabisa baada ya kusoma ujumbe huu umeona ni wapi hutendi vyema. pale ambapo hutendi vyema rekebisha ndugu.

Pale ambapo unachukua wewe heshima ya MUNGU, hakikisha unairudisha heshima hiyo kwa MUNGU.

Kama umepishana na mpango wa MUNGU wa wokovu kwa sababu ya matendo yako, basi badilika na nenda katika KRISTO kwenye wokovu.

Warumi 10:9-11 '' Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. ''

Kama maisha yako umemwazima shetani ili ayatumie, hakikisha unamnyang'anya maisha yako na usikubali kumwazima tema milele, bali kimbilia kwenye mpango wa MUNGU yaani kimbilia kwa YESU KRISTO ili uokolewe.

Yakobo 4:7-8 ''Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.   ''

■Tengeneza uhusiano wako na MUNGU kwa kuanza kumtii na kulitii Neno lake.

■Tunza uhusiano wako na MUNGU maana ukimkosea MUNGU hakuna msaada tena kwako maana hakuna mwenye nguvu na uwezo kama BWANA MUNGU.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU KRISTO Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU KRISTO Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
+255714252292.
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments