SIMAMENI MKAUONE WOKOVU WA BWANA.

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai 

 

Kutoka 14:14 "BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."


Bwana YESU atukuzwe Ndugu yangu.

Karibu nikujuze  mambo niliyopewa muda huu ili nikujuze wewe mteule wa MUNGU unayemwabudu katika ROHO na kweli.


✓✓Simameni mkauone Wokovu  wa Bwana YESU ambao atawapa baada ya maombi yenu na utakatifu.


✓✓Simama ukauone ushindi wa MUNGU kwako.

Ukimtegemea Bwana YESU kwa maombi hakika utaona ushindi.


✓✓Ukimtegemea Bwana YESU kwa maombi hakika utaona baraka za MUNGU.


✓✓Ukimtegemea Bwana YESU kwa maombi hakika utaona uponyaji wake kwako.

Kumtegemea Bwana YESU ni kumtegemea MUNGU muumbaji wako.


✓✓Ukimtegemea Bwana YESU kwa maombi hakika utaona matendo yake makuu maishani mwako.


✓✓Ukimtegemea Bwana YESU kwa maombi hakika utaona  muujiza wa Bwana YESU kwako.


Ni muhimu sana kujua nguvu za unayemtegemea .

Tunaomtegemea YESU KRISTO tunajua hakika uwezo wake kwamba anaweza yote na hakuna anayeweza kushindana naye.

Hakuna mchawi wala jini anayeweza kushindana naye.


Ndugu Ukimtegemea Bwana YESU kwa maombi hakika utaona ushindi mkuu.

Ndugu simama ukauone Wokovu wa MUNGU maishani mwako maana hayo matatizo unayoyaona Leo hutayaona tena.

Hiyo huzuni inayokutesa hutaiona tena, endelea tu na YESU kwa kumtii na kulitii Neno lake.

MUNGU akubariki sana sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292.

Ubarikiwe sana

Comments