USHAURI KWA MTU MMOJA

Na Mwl Peter Mabula 

 

Nasukumwa sana kumshauri mtu mmoja jambo hili.
Ni muda sana Leo nasukumwa kumshauri mtu huyu hata kama simjui na sijui anaishi wapi na dhambi yake ni nini? Mimi sijui.
Sijui kama ni mtumishi au kama ni mtu wa aina gani na ana hadhi gani, ila kwa sababu ya msukumo huo ndani yangu basi naamini atausoma ujumbe wangu na ROHO MTAKATIFU aliyeniongoza Mimi kumshauri ndugu huyu, basi atamsaidia ndugu huyu katika hili kama akitii.
Jambo lenyewe ni hili:
👇👇👇👇👇👇
"Hiyo dhambi ambayo umeshindwa kuiacha naomba ujue kwamba dhambi hiyo inaiba maisha yako.
Sasa kwanini uendelee kuibiwa maisha yako kila siku?
Kumbuka kuna ziwa la moto kwa watu wadhambi kama wewe, lakini pia ukitubu kwa YESU KRISTO na kubadilika leo hakika kuna uzima wa milele kwa Watakatifu.
Mlango wa kuingia mbinguni unahitaji UTAKATIFU na HAKI KATIKA KRISTOYESU ndio mtu anapita.
YESU KRISTO hakika anaokoa, ukimpokea Leo hakika unaokoka.
Hata kama dhambi zako ni nyingi kiasi gani, ukitubu kwake na kuziacha dhambi hizo hakika unaokoka"
👆👆👆👆👆👆👆
Hicho ndicho nilisikumwa sana kukushauri ndugu yangu.
Neema ya KRISTO bado ipo hivyo ni vizuri wewe kutubu na kuacha uovu huo.
Hata Mimi sijui kwanini nimekuambia maneno haya lakini yule aijuaye kesho yako ameniambia nikuonye.
Wakati wa wewe kuokoka haswaa ni sasa.
Bwana YESU anakupenda sana na anataka usiende ziwa la moto, Bali uende uzima wa milele.
Waebrania 3:15 "hapo inenwapo, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha."
Mimi nimemaliza.
Ubarikiwe sana kama ukiacha uovu huo na kuanza kumtii MUNGU Baba.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Naomba nisaidie pia kuusambaza ujumbe huu.

Comments