USIKAE KATIKA MADHABAHU YA BAALI.

 

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Madhabahu ya Baali  ni madhabahu ya shetani.

■Madhabahu ya shetani ni kila madhabahu iliyo kinyume na KRISTO YESU Mwokozi.

●Madhabahu ya Baali haitaki Wokovu wa KRISTO, Haimtaki YESU kama Mwokozi.

Ndugu usikubali kukaa katika madhabahu ya Baali.

Mtumishi wa MUNGU Eliya aliamua kuitengeneza Madhabahu ya MUNGU iliyokuwa imevunjika kwa sababu ya jamii kubwa ya watu kumfuata mungu Baali ambaye ni shetani mwenyewe. 

Wakati huo Baali alikuwa na nabii wake mwanamke Jezebel ambaye alitumia kila mbinu kuwawafanya watu wa MUNGU wamwabudu shetani na kumtumikia yeye.

Eliya nabii akamua kuitengeneza madhabahu ya MUNGU aliye hai.

1 Wafalme "18:30 Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya BWANA iliyovunjika."

Hata leo Baali angali ana watumishi wake.

Ndugu ndio maana nakuomba sana usikubali kukaa katika madhabahu ya Baali.

■Hakikisha unakaa katika madhabahu ya MUNGU aliye hai.

Madhabahu ya MUNGU ina;


1. Jina la YESU KRISTO.

2. Damu ya YESU KRISTO ya agano la milele.

3. Nguvu za ROHO MTAKATIFU.

4. Neno la KRISTO.

■Madhabahu ya MUNGU inaongozwa na ROHO MTAKATIFU.

■Madhabahu ya MUNGU inahusika na utii kwa MUNGU Baba, YESU KRISTO na ROHO MTAKATIFU.


Ndugu kaa katika madhabahu ya MUNGU aliye hai.



■Madhabahu ya MUNGU aliye hai inafundisha watu kuacha dhambi, uovu na makosa.



Ndugu, kaa katika madhabahu ya MUNGU aliye hai.


Neema ya KRISTO YESU iwe nawe daima.


YAHWEH MUNGU wa pekee akubariki.


By Peter Mabula. 


Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi aliye hai. 


+255714252292.


Ubarikiwe

Comments