MTU MWENYE AKILI NI YUPI?

 

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi asifiwe!.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Leo tinajifunza kuhusu Mtu mwenye akili.

1 Wakorintho 15:34 "Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui MUNGU. Ninanena hayo niwafedheheshe."

Akili ni nini?
✓✓Akili ni Uwezo wa Mtu kujua kitu fulani  au jambo fulani.

√Kuna watu Wana akili na Kuna watu wasio na akili.

Leo kwa Neno la MUNGU nataka nikuonyeshe watu wenye akili ili na Wewe ujione kama una akili au huna akili, ujione kama una akili au katika baadhi ya maeneo umepungukiwa akili.
Ujipime ili sehemu ambayo unapungukiwa akili basi uijue na kufanyia kazi ili kuongeza Akili.

Katika baadhi ya mambo ya kiroho Kuna watu hadi wapate ufunuo wa ROHO MTAKATIFU ndipo watapata akili za kujua iwapasayo.
Mfano hai ni huu ambapo Bwana YESU KRISTO aliwafunulia mitume akili zao ndipo wakayaelewa maandiko.

Luka 24:45 "Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko."

Kuna vitu unahitaji ufunuo wa ROHO MTAKATIFU ndipo utapata akili ya kuelewa.

   Hebu mwangalie huyu Mtu mwenye akili kulingana na Biblia ili kama unapungukiwa akili basi uhakikishe na Wewe unakuwa na akili.

Mtu mwenye akili ni yupi?
Mtu mwenye akili ni huyu hapa 

1. Mtu mwenye akili ni Mtu yule anayemtafuta MUNGU

Zaburi 14:2 "Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye MUNGU."

Kumtafuta MUNGU kunahusisha Mambo mengi baadhi ya muhimu sana ni Kumtafuta MUNGU kwa njia ya kumwabudu katika Roho na kweli, kumtafuta MUNGU kwa kuishi maisha matakatifu ayatakayo katika KRISTO YESU, kumtafuta MUNGU kwa kumtolea zaka na  sadaka njema, kumtafuta MUNGU kwa njia ya Maombi sahihi, kumtafuta MUNGU kwa kumsikiliza ROHO MTAKATIFU na kumtii.

Kuokoka ni kibali kikuu Cha Mtu  kumtafuta MUNGU hivyo kama unamtafuta MUNGU anapatikana ndani ya Wokovu wake.

Mtu mwenye akili ni Mtu yule anayemtafuta MUNGU.

Biblia hapo juu inasema MUNGU akachungulia Duniani ili aone kama Yuko Mtu mwenye akili amtafutaye.

✓✓Kumbe Ukitaka uwe Mtu mwenye akili basi tumia nafasi kubwa ya maisha yako kumtafuta MUNGU Baba wa Mbinguni.

2. Mtu mwenye akili ni Mtu yule anayesikia maneno ya YESU KRISTO na kuyafanya.

Mathayo 7:24 "Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;"

Mtu mwenye akili ni Mtu yule anayeyasikia maneno ya Bwana YESU KRISTO na kuyafanyia kazi kwa vitendo.
Mfano Bwana YESU KRISTO anasema hivi " Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." Hiyo Iko 
Mathayo 11:28, mtu mwenye mizigo ya dhambi n.k akimfuata Bwana YESU KRISTO kwa Toba na kumpokea kama Mwokozi hakika anasamehewa na mizigo yake ya dhambi yote inaondolewa kwake.
Ukifanya hivyo kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako hakika wewe utakuwa mwenye akili sana.

✓✓Mtu mwenye akili ni Mtu yule ambaye anaposikia Neno la KRISTO analifanyia kazi kwa vitendo.

Ndugu, Hadi hapo Wewe bado ni mwenye akili?

Mfano mwingine Bwana YESU KRISTO anasema Katika Mathayo 10:40 kwamba " Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma." Maana yake unapowapokea Watumishi halisi wa Bwana YESU hapo unakuwa unampokea YESU KRISTO waliyembeba na unakuwa umempokea MUNGU Baba wa Mbinguni.

Ukiwakataa Watumishi wa Kweli wa Bwana YESU ujue umemkataa  YESU na MUNGU pia.

Wewe uliyeshika dini inayokataa Wokovu wa Bwana YESU KRISTO hakika hapa bado huna akili, sisemi haya kukukwaza bali nakujulisha kwamba unayo nafasi ya kulisikia Neno la Bwana wetu YESU KRISTO na ukalifanyia kazi ili uwe na akili kulingana na Biblia.

Mifano Iko mingi sana, ngoja nikupe huu Mfano mwingine wa Mwisho kwenye point hii
Bwana YESU KRISTO anasema Katika Yohana 10:28  kwamba "Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu."

✓✓YESU KRISTO ndio anayetoa uzima wa milele, Sasa Wewe Kanisa lenu la shetani mmefundishwa kwamba YESU KRISTO ameshamaliza kazi hivyo mnamfuata mwanzilishi wa dhehebu lenu tapeli na wakala wa shetani, nini hamna akili hakika kulingana na Biblia takatifu.

YESU ndiye anayetoa uzima wa milele, wewe viongozi wa dini yako wanakukataza kuja kwa YESU KRISTO na hata wanakutishia kukuua na Wewe umekubali, ndugu kwa mujibu wa Neno la MUNGU viongozi wako hawana akili na wanajitahidi kukufanya na Wewe usiwe na Akili.

✓✓Ndugu, mwenye uzima wa milele ni YESU KRISTO, mfuate katika Wokovu wake ili uwe mwenye akili.

Ndugu, Hadi Sasa bado una akili kwa mujibu wa Biblia?

Kama huna akili chukua hatua za kuokoka ili uwe mwenye akili maana wenye akili huyasikia maneno ya YESU KRISTO na kuyafanya au kuyaishi.

3. Mwenye akili ni Mtu yule anayetamani Neno la MUNGU  ili aliishi na ili aukulie wakovu.

1 Petro 2:2 "Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;"

✓✓Neno la MUNGU la jinsi ya KRISTO ni chakula Cha akili ukila chakula hiki unapata akili.

✓✓Neno la MUNGU ni maziwa ya akili ambayo mtu akiyanywa maziwa haya baada ya kuokoka mtu huyo anakuwa na Akili.

Ndugu usimpokee YESU KRISTO Kisha ukaacha ibada, ukaacha Maombi, mikesha, semina za Neno la MUNGU au ukaacha kujifunza Neno halisi la MUNGU kama unavyojifunza Leo, ukiacha haya hakika hutakuwa na akili sahihi muda mrefu maana hunywi maziwa ya akili ambayo ni Neno la MUNGU.

✓✓Sehemu nyingine Neno la MUNGU linaitwa Mkate wa uzima, wasio na akili hujitenga mbali na Neno la MUNGU lakini wenye akili huambatana daima na Neno la MUNGU bila kuchoka.

Ndugu yangu, Hadi hapo bado una akili zote kulingana na Biblia takatifu?

4. Mtu mwenye akili ni yule anayedumu katika maombi.

1 Petro 4:7 "Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.''

 Biblia inakutaka uwe na akili kwa kudumu katika Maombi.
Kwa Kanisa hai la KRISTO huu ni Ni muda wa maombi kila wakati katika ROHO MTAKATIFU.

Je ndugu unaendelea na Maombi ili uwe Mtu mwenye akili kulingana na Biblia takatifu?

5.  Mtu mwenye akili ni yule anayefunuliwa na MUNGU na  anazingatia nini cha kufanya kulingana na ufunuo aliopewa.

Mfano hai ni kwamba Yusufu alionekana ana akili sana kwa sababu alipofunuliwa na MUNGU alitoa Hadi njia za kufanya ili kuokoa taifa.

Mwanzo 41:39 "Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa MUNGU amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe."

Najua watu wengi sana wanafunuliwa na MUNGU iwe kwa ndoto, Neno la ufunuo, sauti ya MUNGU, Maono n.k lakini wanakuja kuonekana hawana akili kama hawakufanyia kazi maelekezo ya ufunuo wa MUNGU.
Mfano umefunuliwa mtu fulani atapata ajali wewe unamficha na wala kuombi ili kufuta ajali hiyo.
Hapo una akili lakini akili yako haifanyi kazi.
Mtu mwenye akili anapopokea ufunuo wa MUNGU anafanyia kazi pia sawasawa na ufunuo huo.
Wengi Leo akifunuliwa kitu anachukulia ufunuo huo kama kitu Cha kulingishia watu, ndio wale jambo baya alililiona kwenye ulimwengu likitokea yeye anasema "Mimi nilikuwa najua" wakati ni jambo ambalo lilikuwa chini ya uwezo wake kwa kuomba Maombi katika jina la YESU KRISTO ili kuzuia jambo hilo baya alililiona ili lisitokee.
Yale tu ambayo MUNGU amekuambia ni lazima yatokee, hayo ndio huwezi kuombea.

Ndugu, Jitahidi sana  uwe kwenye kundi la watu wenye akili.

✓✓Watu wenye akili wanamtafuta MUNGU Baba wa mbinguni.

✓✓Watu wenye akili wanasikiliza maneno ya YESU KRISTO kupitia Injili na wanayafanyia kazi.

Ndugu, Wapo pia watu ambao  hawana akili wewe hakikisha unakuwa kwenye kundi la watu wenye akili ambao MUNGU anawaangalia.

Zaburi 53:2 "Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye MUNGU."

✓✓ Watu wenye akili wanatamani Neno la MUNGU ili waukulie Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.

✓✓ Watu wenye akili wanadumu katika maombi kupitia jina la YESU KRISTO.

✓✓Watu wenye akili wanamsikiliza ROHO MTAKATIFU na kufuata maelekezo yake.

Ndugu, hadi hapo je bado Wewe ni mwenye akili?

Kinyume cha mtu mwenye akili ni mtu asiye na Akili, wako wengi sana wasio na akili baadhi ni hawa.

1. Mtu anayezini, yaani mzinzi, mzinifu, mwasherati, anayelawiti kinyume na maumbile na kila uzinifu hana akili.

  Mithali 6:32 ''Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.''

✓Ndugu vipo hapo? Wewe bado ni Mtu mwenye akili kulingana na Neno la MUNGU?

✓✓Kama Wewe sio mwasherati, husaliti Ndoa yako, hukutani kimwili na Mchumba wako, hulawiti, sio shoga wala kahaba basi wewe ni mwenye akili.

Lakini kama unafanya dhambi hizo hakika wewe huna akili.
Je Hadi hapo ndugu bado Wewe ni mwenye akili?
Kama bado ni mwenye akili MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

Biblia inaendelea kusema mtu mzinzi au mwasherati hana akili kabisa.
Ona mfano wa kijana huyu asiye na akili na Mwanamke huyu asiye na akili.
Mithali 7 isome yote ila Mimi nakuletea mistari hii tu 7,10,13,18 na 19

Biblia inasema "Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, ....... Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;..............  Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, ........... Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. .......... Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali;

Huyu ni Mwanaume asiye na akili akakutana na Mwanamke asiye na akili.

Je wewe Ndugu unayesoma ujumbe wangu huu, Wewe ni mwenye akili katika hili.

✓✓Ndugu, acha uzinzi na uasherati ili utoke kwenye kundi la watu wasio na akili.

2. Mtu asiye na akili huonea watu.
 
   Mithali 28:16 "Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake."

Kama unaonea watu wewe umepungukiwa akili na huna akili kabisa.

Ndugu,Katika kuishi kwako  duniani hakikisha unakuwa mtu mwenye akili
✓✓Mtu mwenye akili anampokea YESU KRISTO kama mwokozi wake na anaanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa Bwana YESU.

✓✓Mtu mwenye akili anaacha dhambi zote, anaacha uzinzi, uongo, achawi, wizi, umbea n.k
Uwe mwenye akili kuanzia leo.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU KRISTO Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU KRISTO Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
+255714252292(Whatsapp, Sadaka ya kuipeleka Injili mbele, Ushauri na Maombezi)
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments