MUNGU NDIYE ANISAIDIAYE MWANADAMU ATANITENDA NINI?

 

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.
Karibu ujifunze kitu.
Huu ulikuwa ufunuo wa sauti  niliofunuliwa nikiwa safarini, Nikasikia Sauti ikisema "MUNGU ndiye anisaidiaye Mwanadamu atanitenda nini?" Hii ilikuwa ni baada ya kuwa katika vitisho vikubwa sana  nilivyopitia katika ulimwengu wa mwili.
Baada ya kutishwa sana sikuogopa ila nikiwa natafakari ndipo nikasikia "MUNGU ndiye anisaidiaye Mwanadamu atanitenda nini?"

✓✓ Inawezekana na Wewe unatishwa na mchawi au mganga, taarifa Moja muhimu kwako ni kwamba MUNGU akikusaidia hakuna  Mwanadamu  atakuweza.

✓✓Inawezekana Kuna mtu anakutisha sana na uko kwenye mazingira magumu sana, taarifa Moja ni kwamba Bwana YESU KRISTO akikusaidia hakuna Mwanadamu atakuweza.

✓✓Inawezekana Kuna Kuna wakala wa shetani anakutisha na kukupangia mabaya, taarifa Moja ni kwamba ROHO MTAKATIFU akikusaidia hakuna Mwanadamu atakuweza kamwe.

Neno la MUNGU linasema katika 
Waebrania 13:6 kwamba " Hata twathubutu kusema, BWANA ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?"

Ndugu yangu, MUNGU akikusaidia hakuna jini wala mzimu atakugusa.

MUNGU akikusaidia hakuna Mwanadamu atakushinda.

✓Inawezekana Kuna mtu anataka ufilisike au upotee kabisa kiuchumi au ufukuzwe kazi au usipate kazi kabisa,  taarifa Moja ni kwamba MUNGU anaweza kukusaidia hata katika mambo yanayohusu uchumi.

Mwanzo 49:25 "Naam, kwa MUNGU wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba."

Hakikisha tu umeokoka na YESU KRISTO ndie Mwokozi wako na unaishi maisha matakatifu ya Wokovu wake.

✓Inawezekana unapambana na maadui wengi, Israeli waliwashinda maadui wengi na wenye nguvu waitwao Wafilisti na Samweli akathibitisha kwamba ni MUNGU tu amewasaidia, na ndivyo ilivyokuwa.

1 Samweli 7:12 "Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia."

✓Inawekana Kuna adui yako na Yuko karibu yako sana na anadhani muda wowote anaweza kutimiza jambo lake baya, ndugu yangu, MUNGU Yuko karibu yako sana kuliko adui yako anayedhani Yuko karibu yako.

Ngoja nikupe mfano huu, Washami walikuwa wanaoigana na Israeli kipindi Cha Jehoshaphat na Waliambiana kwamba hawatapambana na Mwisraeli  isipokuwa Yehoshafati na wakamuona Yehoshafati kabisa wakawa karibu nae, lakini Yehoshafati alipogundua akamlilia MUNGU ili amsaidia, dakika Ile Ile kabla adui zake hawajamfanya lolote akamsaidia akawafukuza adui wale.
2 Nyakati 18:31" Ikawa maakida wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na BWANA akamsaidia; MUNGU akawafarakisha kwake."

Huyu MUNGU ni yeye tangu siku Ile Hadi Leo, anaweza kukusaidia katika jina la YESU KRISTO juu ya adui zako wote.

✓Huyu MUNGU anaweza kukusaidia hata kama maadui zako ni wengi sana na wako makundi makundi.

Mfano ni huu MUNGU alimsaidia Mtu aitwae Uzia juu ya adui zake Wafilisti, Waarabu na Wameuni.

2 Mambo ya Nyakati 26:7 "MUNGU akamsaidia juu ya Wafilisti, na juu ya Waarabu waliokaa Gur-baali, na juu ya Wameuni."

Huyu MUNGU katika KRISTO YESU anaweza kukusaidia dhidi ya adui zako wote.
Kazi yako ni kuomba katika jina la YESU KRISTO huku ukiishi maisha matakatifu ya Wokovu wake.
MUNGU alinisaidia Mimi Peter Mabula dhidi ya maadui wenye vitisho vingi, anaweza kukusaidia na Wewe rafiki yangu.
Omba kwa Imani, omba katika jina la YESU KRISTO na adui zako wote utawashinda maana MUNGU Baba wa Mbinguni atakusaidia.
MUNGU akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
MUNGU akubariki.

Comments