ANA LAANA.

 

By Peter Mabula

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU aliye hai.

Yeremia 17:5 "BWANA asema hivi, AMELAAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU, AMFANYAYE MWANADAMU KUWA KINGA yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA."

✓✓Ana laana Mwanadamu yule anayemtegemea mwanadamu mwenzake kama kinga yake.

✓✓Ana laana Mwanadamu yule anayemsahau MUNGU Baba wa Mbinguni.

✓✓Ana laana Mwanadamu yule anayetegemea waganga wa kienyeji na majini.

✓✓Ana laana Mwanadamu yule anayetegemea hirizi, matambiko na mazindiko.

✓✓Ana laana Mwanadamu yule anayetegemea mizimu au kushirikiana na mizimu.

Ndugu yangu, nakuomba usiwe mwana wa laana bali fanyika mwana wa baraka.

Kuna Watu wana laana.

2 Petro 2:14-15 " wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, WANA WA LAANA;wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;"

Wana wa laana ni wazinzi, wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa, wenye kutamani mabaya na wanaomwacha YESU KRISTO na Wokovu.

✓✓Ana laana Mwanadamu yule anayemchukia YESU KRISTO na amekataa Wokovu wake.

Kumwacha YESU ni kufuata laana,kumchukia YESU ni kujitafutia laana.

1 Wakorintho 16:22 "Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha."

Ndugu yangu, naomba usiwe wewe kulaaniwa kwa sababu ya ya hayo niliyoyataja hapo juu.

Nakuomba hakikisha unakuwa Mwanadamu aliyebarikiwa na sio kuwa Mwanadamu aliyelaaniwa.

Yeremia 17:7" Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake."

Mtu asiye na laana ni mtu yule anayemtegemea MUNGU katika KRISTO YESU.

Mtu asiye na laana ni mtu Yule anayemtumaini MUNGU na kumwabudu katika KRISTO YESU.

Mtu asiye na laana ni mtu yule aliye na ROHO MTAKATIFU na anaongozwa na yeye.

Ndugu hakikisha unaishi maisha ya kubarikiwa na MUNGU na sio kuishi maisha ya laana.

MUNGU akubariki.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments