MAOMBI YA KUTUMIA DAMU YA YESU KRISTO ILI KUONDOA MATATIZO YA KIAGANO, KAFARA, VIAPO NA MANUIZO YA KIPEPO.
![]() |
Na Mwl Peter Mabula |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU kisha kisha tuombe maombi ya ushindi.
Siku
moja usiku katika ndoto, kulikuwa na vita sana, mambo yalikuwa magumu
lakini ghafla akaja mtu mwenye utukufu mwingi akisema ''Tumia Damu ya
YESU KRISTO''
KAZI 12 ZA DAMU YA YESU KRISTO.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuna mamlaka nne za MUNGU kwa Mkristo ambazo mamlaka hizo humfanya Mkristo kuwa mshindi daima.
Mamlaka
hizo ni Jina la YESU KRISTO, Nguvu za ROHO MTAKATIFU, Damu ya YESU
KRISTO na Neno la MUNGU la ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.
Leo nazungumzia Damu ya YESU KRISTO Katika kipengele kiitwacho Kazi za Damu ya YESU KRISTO.
Kwanza
kabisa ni muhimu kila mtu kujua kwamba Damu ya YESU KRISTO ni kwa ajili
ya Watu wote duniani, cha kufanya tu ni kumpokea YESU KRISTO kama
Mwokozi.
Ufunuo 5:9
"Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe(YESU) kukitwaa hicho
kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia MUNGU
kwa DAMU yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,"
Damu
ya YESU KRISTO ina kazi kubwa mno katika ulimwengu wa roho na matokeo
ni makubwa sana katika ulimwengu wa mwili kwa Wateule wa MUNGU.
Wakolosai
1:19-20 " Kwa kuwa katika yeye(YESU) ilipendeza utimilifu wote ukae; na
kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani
kwa DAMU ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi,
au vilivyo mbinguni."
Lengo
la somo hili ni wewe uwe unaomba katika jina la YESU KRISTO huku
ukitumia Damu ya YESU KRISTO ili uwe huru na uwe mshindi dhidi ya nguvu
za giza.
Pia lengo la somo hili ujue kazi za damu
ya YESU KRISTO maana hata ujasiri tu wa kupaingia patakatifu, huo
ujasiri utakuwa nao ukiwa tu na Damu ya YESU KRISTO.
Waebrania 10:19 "Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa DAMU YA YESU,"
Kuna kazi nyingi za Damu ya YESU KRISTO kwa Mkristo aliye na YESU KRISTO na anajua kuomba maombi akitumia damu ya YESU KRISTO.
Hivyo ukiona Watu au dhehebu wanajitenga mbali na damu ya YESU KRISTO ujue upo mahali pasipo sahihi.
Waebrania
13:20 "Basi, MUNGU wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji
Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu YESU,"
Damu
ya YESU KRISTO sio vitu vya duniani , hivyo mtu asikudanganye lakini
damu ya YESU KRISTO ipo tayari kwenye ulimwengu wa roho kwa ajili yako.
Damu
ya YESU KRISTO ni ya muhimu Sana maana hata Mbinguni watakatifu walioko
huko ni wale tu waliosafishwa Kwa damu ya YESU KRISTO.
Ufunuo
7:14 "Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio
wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na
kuyafanya meupe katika DAMU YA Mwana-Kondoo(YESU KRISTO)."
Baadhi ya kazi za Damu ya YESU KRISTO.
1. Damu ya YESU KRISTO hutengeneza agano jipya kati ya MUNGU na Mwanadamu aliyemwamini KRISTO.
Marko 14:24 "Akawaambia, Hii ndiyo DAMU YANGU YA AGANO, imwagikayo kwa ajili ya wengi."
Agano maana yake ni patana au kupatana hivyo tunapatana na MUNGU muumbaji wetu kwa damu ya YESU KRISTO.
Kuna maagano ya kabla ya YESU KRISTO kuja duniani lakini ni MUNGU mwenyewe ndiye aliyezungumzia agano jipya ambalo atalileta.
Yeremia
31:31-33 " Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya AGANO
JIPYA na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. Si kwa mfano wa agano
lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili
kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja,
ingawa nalikuwa mume kwao, asema BWANA. Bali agano hili ndilo
nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA;
Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami
nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu."
Kwa
hiyo ni kwamba kwa sasa sisi tuko katika agano jipya katika damu ya
YESU KRISTO na hili agano jipya linaenda hadi kurudi kwa Bwana YESU mara
ya pili.
2. Damu ya YESU KRISTO hufuta dhambi zote za mtu anayetubu kwa MUNGU katika KRISTO YESU.
Mathayo 26:28 "kwa maana hii ndiyo DAMU YANGU YA AGANO, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."
Yaani Damu ya YESU KRISTO ina uwezo wa kulipa madeni yote ya dhambi ya Watu wote duniani wanaoamua kuokoka.
Ufunuo
1:5 "tena zitokazo kwa YESU KRISTO, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa
kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na
kutuosha dhambi zetu katika DAMU YAKE,"
3. Damu ya YESU KRISTO huleta upatanisho kati ya Mwanadamu anayeokoka na MUNGU.
Warumi
3:25 "ambaye MUNGU amekwisha kumweka AWE UPATANISHO KWA NJIA YA IMANI
KATIKA DAMU YAKE,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia
katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa."
MUNGU amemweka YESU KRISTO ili awe upatanisho kwetu kwa njia ya imani katika damu yake ya agano jipya.
Hivyo kama unahitaji upatanisho ujue unaihitaji damu ya YESU KRISTO ya upatanisho.
Wakolosai
1:20 "na kwa yeye(YESU) kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha
kufanya amani kwa DAMU YA MSALABA WAKE; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo
juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
4. Damu ya YESU KRISTO husafisha Dhamiri, nafsi na mioyo yetu.
Waebrania
9:13-14 " Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama
ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha
mwili; basi si zaidi damu yake KRISTO, ambaye kwamba kwa ROHO wa milele
alijitoa nafsi yake kwa MUNGU kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha
dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu MUNGU aliye hai?"
Damu ya YESU KRISTO husafisha dhamiri.
Dhamiri ni nini?
Dhamiri ni nia ya kufanya jambo.
Watu wengi wana nia mbaya tu Katika nafsi zao, hao wana dhamiri mbaya.
Inawezekana
moyoni mwako unawaza mabaya tu, hutaki kuyawaza lakini uajikuta
unayawaza, ndugu dhamiri yako inatakiwa kusafishwa kwa damu ya YESU
KRISTO.
Ndugu, Omba
maombi leo katika Jina la YESU KRISTO huku ukitumia damu ya YESU KRISTO
kukusafisha dhamiri yako, ili uwe na dhamiri njema kuanzia sasa.
1
Yohana 1:7 "bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru,
twashirikiana sisi kwa sisi, na DAMU yake YESU, Mwana wake, yatusafisha
dhambi yote."
5. Damu ya
YESU KRISTO inaleta ulinzi katika mwili, afya, familia, biashara, ndoa
n.k kulingana na maombi ya mkristo mhitaji anayeomba.
Ufunuo 12:11 "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa."
Hapa unahitaji tu kufanya maombi ili damu ya YESU KRISTO ifanye kazi kama ulivyoomba katika maombi yako.
6. Damu ya YESU KRISTO hututakasa na kutufanya tuwe huru.
Waebrania 13:12 "Kwa ajili hii YESU naye, ili awatakase watu kwa DAMU yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango."
Damu ya YESU KRISTO hutakasa.
Kutakasa ni nini?
Kutakasa ni kuondoa uchafu na kufanya kitu au mtu au eneo kuwa safi kiroho.
Damu ya YESU KRISTO kwa maombi yako inaweza kutakasa eneo la mwili wako unalotaka litakaswe, afya, ndoa, nyumba, ardhi n.k
7. Damu ya YESU KRISTO hutufanya tukae ndani ya YESU KRISTO.
Yohana
6:54-56 " Aulaye mwili wangu na KUINYWA DAMU YANGU anao uzima wa
milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula
cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na
kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake."
Kuinywa
Damu ya YESU KRISTO ni kutafakari uwezo ulioko ndani ya Damu YESU
KRISTO na kuutumia huo uwezo ulio ndani ya damu katika damu ya YESU
KRISTO.
Pia ni muhimu kujua kwamba Mtu ambaye
ameula mwili wa KRISTO na kuinywa damu yake ile iliyomwagika msalabani,
ni yule ambaye anakaa ndani ya YESU KRISTO, na YESU KRISTO anakaa ndani
yake.
8. Damu ya YESU KRISTO imetununua tuliokoka ili tuwe wa MUNGU kwa ajili ya uzima wa milele.
Matendo
20:28 "Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo ROHO
MtakaTtifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha
kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa DAMU YAKE mwenyewe."
Biblia inasema MUNGU ametununua sisi Kanisa kwa damu yake, hiyo ni kupitia YESU KRISTO Mwokozi wetu.
9. Damu ya YESU KRISTO hutufanya tuhesabiwe haki mbele za MUNGU.
Warumi 5:9 "Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika DAMU yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye."
10. Damu ya YESU KRISTO huleta ukombozi kwetu tuliompokea YESU KRISTO kama Mwokozi wetu.
Waefeso 1:7 "Katika yeye huyo, kwa DAMU yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake."
Yako
maeneo yako mengi yanahitaji ukombozi wa damu ya YESU KRISTO, kazi
yako ni kufanya maombi ya ukombozi na damu ya YESU KRISTO itakukomboa.
Damu ya YESU KRISTO huleta ukombozi.
1
Petro 1:18-19 " Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu
viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu
usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa DAMU YA THAMANI, kama ya
mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO."
11. Damu ya YESU KRISTO hutufanya tuwe karibu na YESU KRISTO.
Waefeso 2:13 "Lakini sasa, katika KRISTO YESU, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa DAMU yake KRISTO."
12. Damu ya YESU KRISTO hunena mema.
Waebrania 12:24 "na YESU mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili."
Ni
jukumu lako tu kuishi maisha matakatifu ya Wokovu na kuomba katika jina
la YESU KRISTO ukiomba damu ya YESU KRISTO inene mema na itanena.
Inawezekana unasemwa vibaya sana na Watu, Omba damu ya YESU KRISTO inene mema kwako.
Inawezekana
unataka damu ya YESU inene mema kwenye ndoa yako, biashara yako, afya
yako, kibali chako, kazi yako, mwili wako, Familia yako, Ardhi
yako n.k
Ndugu Omba na damu ya YESU KRISTO itanena mema.
Ndugu, husika na YESU KRISTO na damu yake kwenye maisha yako.
Warumi
6:22 "Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na
kufanywa watumwa wa MUNGU, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho
wake ni uzima wa milele.'
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
.
Hakika damu ya YESU KRISTO na jina la YESU KRISTO ndio ushindi mkubwa zaidi wa Mkristo.
Zakaria 2:5 ''Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.''
Katika maombi ni muhimu sana kuita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kukulinda.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuilinda ndoa yako na kitanda chako na chumba chako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuilinda biashara yako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kulinda baraka zako ulizopewa na MUNGU.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuwalinda watoto wako na mke/mume wako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuinusuru ndoa yako iliyo katika kuangamia.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuilinda huduma yako uliyopewa na MUNGU
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto Kuilinda nyumba yako au kiwanja chako au eneo lako la biashara.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kulinda uchumba wako mtakatifu.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuwalinda ndugu zako na ukoo wako na familia yako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kukukinga na kila mishale ya shetani.
Ita damu ya YESU KRISTO katika kitu chako chochote unachotaka kilindwa na nguvu za MUNGU.
Jambo
la kuzingatia kwanza ni utakatifu tu, kama hujaokoka hakikisha unaokoka
kwanza na tubu uovu wako na kuuacha maana viwango vya MUNGU kukujibu na
kukuzingira ni pamoja na wewe kuwa mtakatifu.
Kataa ya dunia maana hayo yataisha.
Kumbuka
Biblia imesema kwamba MUNGU atakuwa ukuta wa moto ili kulinda mji, na
katika mji kuna watu hivyo MUNGU atawalinda watu. wewe ni mteule wake na
una haki ya kulindwa na MUNGU BABA. ukuta wa moto haiwezekani adui
kuuvuka hata akakuroga na kukudhuru.
Biblia pia imsema kwamba tunamshinda shetani kwa damu ya YESU KRISTO na kwa Neno la ushuhuda.
Ufunuo
12:11 '' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la
ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ''
Ni muhimu sana kuita damu ya YESU ili ikuzingire adui zako wasikuone.
Damu ya YESU ndio inaweza kugeuka ukuta wa moto na kukulinda.
Usikubali adui zako wakakuona tena kwenye tv zao za kichawi.
Usikubali
wachawi wakuroge tena bali ita damu ya YESU KRISTO ambayo haijawahi
kushindwa. Damu ya YESU KRISTO ina kazi 4 kwetu na moja ya kazi hizo nne
ni kutulinda hivyo utakuwa salama kama utaita damu ya YESU KRISTO
katika maisha yako, kazi yako, biashara yako, huduma yako, masomo yako,
ndoa yako n.k.
Maombi hapa chini ni ya kukufundisha ili wewe uombe katika hitaji lako na uombe kwa imani na kwa muda mrefu.
Maombi ya kuita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kukuzunguka.
JEHOVAH
MUNGU uliye hai ninakuabudu na ninakutukuza. Ni wewe MUNGU mbinguni, ni
wewe MUNGU duniani na ni wewe MUNGU kwenye ulimwengu wa roho na kwenye
ulimwengu wa mwili pia.
Nakushukuru MUNGU wangu kwa uzima ulionipa na nakushukuru maana hata sasa ninaishi kwa ulinzi wako.
Nakuita
BWANA siku ya leo nikiamini kama neno lako linavyosema kwamba ''Kwa
sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba
mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. - Marko 11:24'' Naamini sasa kwamba
ninayoomba nitapokea kwa jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru BWANA YESU kwa ajili ya damu yako ya agano la milele ambapo kwa damu hiyo tunapata uzima, ushindi na ulinzi.
Sasa
BWANA kwa jina la YESU KRISTO naita damu ya YESU ya agano ili iwe ukuta
wa moto kunizingira mimi na familia yangu, adui aliyezoea kunionea
usiku nikiwa nimelala sasa hataniona tena maana damu ya YESU KRISTO
inanizunguka sasa pande zote, kwa jina la YESU KRISTO naita damu ya YESU
KRISTO ili iwe ukuta wa moto kunizunguka mimi na biashara yangu ili
waharibifu wasinione kamwe kwa jina la YESU KRISTO. naita damu ya YESU
KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuizingira nyumba yangu na wazazi wangu na
watoto wangu na ndugu zangu katika jina la YESU KRISTO. naita damu ya
YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kulinda uchumba wangu pamoja na
mchumba wangu, naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto
kuzunguka mimba yangu na mtoto aliye ndani katika jina la YESU
KRISTO. naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuzizunguka
pesa zangu zilizo benki au dukani katika jina la YESU KRISTO. naita
damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuizingira ndoa yangu ili
adui anayepanga kuiangamiza hataiona tena maana imefunikwa kwa damu ya
YESU KRISTO katika jina la YESU KRISTO.
naita
damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kunizingira pande zote,
kunizingira mimi na mali zangu zote, shetani hataniona mimi wala mali
zangu kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kulinda nyumba yangu na walio ndani yake katika jina la YESU KRISTO.
naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kulinda kanisa letu na mchungaji wetu katika jina la YESU KRISTO.
naita
damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuwalinda watumishi wa
BWANA YESU wote walio katika nchi yangu katika jina la YESU KRISTO.
naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kila kona ya maisha yangu katika jina la YESU KRISTO.
naita
damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili adui yeyote akija kwangu
aangamie kwa jina la YESU KRISTO katika jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru BWANA maana umejibu maombi yangu.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na ninapokea ushindi sasa Amen Amen.
Naamini
kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe
uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama
wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako ,
nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia
kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
+255714252292.
Ubarikiwe sana
Comments