MWANZO WA SIKUKUU YA CHRISTMAS


Mwl Peter Mabula 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu zangu wote. 
Tunapoelekea kusherekea sikukuu ya Christmas naomba pia nijibu swali hili ambalo rafiki yangu mmoja ameniuliza December 2023.
Ni swali kuhusu Mwanzo wa sikukuu ya Christmas. 

Christmas ninatokana na neno la kiingeleza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani Misa au Ibada ya KRISTO. Wengine Christmas huita Noeli, ni sawa kabisa

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka Lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis " yaani (siku ya) kuzaliwa".

Kuhusu tarehe ya kuadhimisha sikukuu ya Christmas  ni kwamba 
tarehe hiyo   iliwekwa na Viongozi wa Kanisa, ni tarehe ya kubuni ili kuhamisha watu wasiitumie siku hiyo ya December 25 kuabudu miungu kwani katika utawala wa Rumi wakati ule ambao ulikuwa utawala mkuu duniani, kulikuwa na maagizo ya kiserikali watu kuabudu miungu ambao waliita mungu Jua, Kanisa wakaona waivunje nguvu siku hiyo kwa kuihamisha kuwa siku ya kuzaliwa kwa YESU na baada ya hapo Watu wakaacha kuabudu miungu katika siku hiyo. Ingawa kwa baadhi ya maeneo hata leo shetani amepanda uongo mwingi wa watu kufanya maovu mengi katika siku hii

Ukisoms Warumi 14:5-6 sio kosa kuadhimisha siku yeyote kama ni unaiadhimisha kwa MUNGU na unampa utukufu yeye, Biblia inasema ''Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa BWANA; naye alaye, hula kwa BWANA, kwa maana amshukuru MUNGU; tena asiyekula, hali kwa BWANA, naye pia amshukuru MUNGU.''

Kama ulikuwa hujui ni kwamba  Wakati Bwana YESU anazaliwa katika Utamaduni wa Wayahudi wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa. Ndio maanahaikutunzwa siku kamili ya kuzaliwa Bwana YESU, baada ya hapo Ukristo ulienea katika Dola la Rumi ambako huko ni kawaida ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia sikukuu ya kuzaliwa kwake KRISTO. Ndiyo asili ya sikukuu ya Krismasi ingawa walishindwa kujua tarehe halisi ya kuzaliwa Bwana YESU 

Baadae Kuanzia mwaka 200 (kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus) wataalamu nchini Misri waliona tarehe 14 Nisan ya kalenda ya Kiyahudi ambayo ni sawa na 25 Machi ilikuwa tarehe ya kufa kwake KRISTO na pia siku ya utungaji mimba wake. Kwa kuongeza miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa, haya ni makadirio tu ya watu hawa, ingawa lengo lao ipatikane siku ya kuzaliwa Bwana YESU, sikubaliani nao maana Biblia haisemi tarehe ya kutungwa mimba Bwana YESU, hata Maria Mariamu alijikuta tu yuko Mimba sijui ni muda gani baada ya kupewa taarifa na Malaika. 

Chanzo kingine cha Kanisa kupachika sikukuu ya Christmas kwenye tarehe hiyo ni kwa nia ya kufanya ichukue nafasi ya sikukuu ya miungu ambayo iliitwa sikukuu ya mungu jua "Sol invictus" (yaani "Jua lisiloshindika").
Wataalamu wa Biblia kwa kuwaaminisha watu walijaribu kuhususisha YESU na jua la haki kimaandiko Kuwa Jua ni ishara ya KRISTO; katika sehemu mbalimbali za Biblia Kristo alifananishwa tayari na Jua wakitumia Mifano ya ni Luka 1:78, Ufunuo 21:23 na Malaki 4:2 hivyo katika mashindano na dini ya kuabudu Juailiyokuwepo wakati ule Wakristo wao waliamua kutumia lugha ya Biblia kwa kudokeza KRISTO ndiye Jua la Haki hivyo waache ibada ya jua, Wamwabudu KRISTO kupitia sikukuu hiyo ya tarehe 25 iliyokuwa na Nguvu sana wakati ule.

Kanisa walifanikiwa kwa wakati ule ingawa baadae shetani aliingiza uongo katika sikukuu hiyo ili kuwahamisha baadhi ya watu katika kuitumia siku hiyo kumwabudu MUNGU aliye hai.

Maoni yangu Kanisa wakati ule walitaka tarehe 25 December iwe birthday ya YESU na hata Kanisa la leo baadhi ya maeneo maeneo kwenye ibada ya Christmas hufundisha kwamba "Leo ni Birthday ya YESU" haipaswi kuwa hivyo, hatuadhimishi Birthday bali tunakumbuka  tukio la kuja kwa ukombozi wetu, sio Birthday ya YESU. Tunaitumia siku hiyo kuuambia ulimwengu wote kwamba YESU alikuja kwa ajili ya Wanadamu wote ndio maana nilianza na andiko la Warumi 14 la kuiadhimisha siku ila ni katika MUNGU tu. 
Itumie siku hii kwa Bwana YESU KRISTO kwa utakatifu wote bila kuweka michanganyo ya kidunia.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana. 
By Mwl Peter Mabula. 
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele. 
Ubarikiwe 

Comments