UTAFUTE UFALME WA MUNGU.

 




Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu atukuzwe ndugu yangu.
Jifunze kitu kupitia ujumbe wangu huu mfupi.

Nafasi ya kwanza ya mwanadamu maishani mwake inatakiwa kuwa ni kuutafuta ufalme wa MUNGU ambao uko pekee katika Wokovu wa KRISTO YESU.

Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."

✓✓Ndugu, usikubali kutafuta kwanza mengine kisha ufalme wa MUNGU baadaye.

✓✓Ndugu, usikubali kutafuta maisha kwanza huku ukipanga kuokoka baadae.

✓✓Ndugu, usikubali kutafuta kwanza mke/Mume harafu mambo ya Wokovu baadae.

✓✓Ndugu usikubali kutafuta pesa kwanza kisha ufalme wa MUNGU baadae.

✓✓✓Biblia inakutaka kutafuta kwanza ufalme wa MUNGU na haki yake.

Haki ya ufalme wa MUNGU ni utakatifu katika KRISTO YESU.

Wengi walitafuta maisha kwanza na hawakuyapata na huku ufalme wa MUNGU pia wameukosa.

Wengi walitafuta dunia kwanza na hawakuimaliza huku ufalme wa MUNGU wameukosa, wakiambulia magonjwa na majeraha tu.

Wengi walitafuta mambo yao kwanza lakini hata hayo hawakuyapata.

Ndugu mpendwa nakuomba ifuate Biblia ndio utafanikiwa.

Na Biblia inakushauri kwamba utafute kwanza ufalme wa MUNGU na hayo mengine utazidishiwa na MUNGU.

Kuna watu wana juhudi sana katika kutafuta pesa lakini kwa sababu hawana ulinzi wa MUNGU ndio maana hujikuta wakinufaisha wengine wanaotumia nguvu za Giza.

Sio kwamba usifanye kazi Kabisa, hapana, Bali Fanya kazi ukiwa ndani ya ufalme wa MUNGU.

Mpate Mwenzi ukiwa ndani ya ufalme wa MUNGU na yeye awe yuko katika ufalme wa MUNGU ndipo itakuwa kustawi kwako na kufanikiwa kwako.

Itafute mbingu kwanza.
Mtafute MUNGU kwanza .
Mtii YESU KRISTO Mfalme wa ufalme wa MUNGU.
Na kumtii YESU ni kutii maagizo yake yote anayoagiza katika Biblia takatifu. Yeye Bwana YESU anasema " Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.- Yohana 15:23

Pia anakushauri kwamba litii Neno lake.
Yohana 14:15 "Mkinipenda, mtazishika amri zangu."

Ndugu yangu utafute kwanza ufalme wa MUNGU.
Neno hili ni lako maana ni ufunuo kwa ajili yako.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
+255714252292( Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments