WOKOVU.

 




■Wokovu sio wa kundi Bali wokovu ni wa mtu mmoja binafsi.

Waebrania 5:9 "naye(KRISTO) alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

●Ukitaka wokovu uwe wa kundi basi baadhi ya wana kundi wakirudi nyuma basi na wewe utarudi nyuma.
Lakini ukijitambua kwamba wokovu ni kwa ajili yako binafsi basi utaendelea na YESU KRISTO hata kama ulionao wamekengeuka.
Utaendelea na utakatifu hata kama jamii yako iko mbali na MUNGU.

Yuda 1:3 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."

●Wokovu sio wa familia kiasi kwamba baba au mama akiacha kwenda Kanisani na wewe unaacha.

Waebrania 9:28 "kadhalika KRISTO naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu."

●Wokovu sio wa ukoo kiasi kwamba mkuu wa ukoo wetu akisema "Inatosha kumwabudu MUNGU wa kweli, basi tuigeukie mizimu" wewe mteule usikubali kufuata miungu hiyo hata kama ukoo mzima wameigeukia.
Kumbuka wokovu wa KRISTO ni kwa ajili ya mtu mmoja binafsi anayejitambua.
Hakikisha unang'ang'ania taji yako ya uzima ulioipata baada ya kumpokea Bwana YESU.
MUNGU akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments