NATAKA KUTUBU NA KUOKOKA

 


Mtu mmoja aliniandikia hivi 👇👇👇👇

Mtumishi Mabula nataka kutubu na nibadilike kabisa niwe Mtakatifu ninayeambatana na Yesu katika wokovu wake na utakatifu maana nilikuwa dini nyingine lakini moyoni mwangu nashuhudiwa Kila siku kwamba siwezi kupata uzima bila Yesu kristo, nitumie maandiko yanayohusu kutubu.

Majibu yangu yalikuwa haya👇👇👇👇👇👇
MUNGU akubariki sana.
Umechukua uamuzi mzuri kuliko maamuzi yote anayoweza kuyafanya mwanadamu yaani kumpokea Bwana YESU KRISTO awe Mwokozi wako na kutubu Kwa kumaanisha, Kwa uamuzi huo hutajuta milele.

Maandiko kuhusu kutubu Yako mengi sana lakini kama ulivyoomba baadhi ni haya
✓✓ Haya ni majira ya kutubu ili kuwa watakatifu katika KRISTO.

Mathayo 3:2 "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."

✓✓ Dhambi ni kikwazo Cha mambo mengi sana. mazuri kwa Mtu, hivyo ondoa Dhambi Kwa kutubu mbele za  MUNGU katika KRISTO YESU.

Isaya 59:1 "Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;  lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.  Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya."

✓✓Mahubiri ya mwanzoni ya Bwana YESU yalikuwa kuwaambia watu watu, hata Leo mtu anayetenda Dhambi na ambaye hajaokoka fundisho kuu la kumfundisha ni ili atubu.

Marko 1:15 " akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili."

✓✓Kuongozwa sala ya toba na kutubu katika KRISTO YESU ndio njia kuu ya kurudisha uhusiano kati Yako na MUNGU wa kweli.

Matendo ya Mitume 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; "

 ✓✓Wazazi wanaweza kumdanganya Mtoto wao na kumwelekeza dini za mashetani ambazo ni zile zote ambazo ziko kinyume na wokovu wa KRISTO Mwokozi, Ndugu unaweza hata kutubu Kwa ajili ya wazazi wako na Babu zako walio hai ili watoke kwenye ukengeufu wa kidini, waje Kwa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Yeremia 14:20 "Ee BWANA, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa baba zetu; maana tumekutenda dhambi. "

✓✓✓Ukweli mmoja ni huu hakuna Mwanadamu hata mmoja unayemfahamu au usiyemfahamu atakayeingia uzima wa milele kama hana YESU KRISTO kama Mwokozi wake.

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.  Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.  Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

Ubarikiwe sana.
Hata Kwa wewe ambaye unasoma ujumbe huu na hujaokoka, hujatubu na kuacha Dhambi nakuomba sana fanyia kazi ujumbe huu.
✓✓Hakikisha unampokea Bwana YESU KRISTO awe Mwokozi wako milele.

✓✓Hakikisha unakuwa na YESU KRISTO milele.

✓✓✓Jitenge na Dhambi, acha Dhambi, ukimbie Dhambi na usitende Dhambi Tena.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu Aliye hai milele.

Comments