JINA LA YESU KRISTO LINAWEZA KUFUTA LAANA YAKO.

 

Na Mwl Peter Mabula,  Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele 

Bwana YESU KRISTO asifiwe rafiki yangu.

Karibu ujifunze kitu kupitia ujumbe huu mfupi ambao mimi Peter Mabula nimekuandalia.


✓✓Maana mojawapo ya Neno ''laana '' ni apizo atoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na mabaya.


✓✓Maana ya neno ''apizo'' ni dua ya kumuombea mtu laana.


Sijui kama ulishawahi kuomba maombi ya kufuta maapizo yote mabaya  yanayotengeneza mikosi, balaa na mambo  mabaya katika maisha yako!.


Laana ambazo zinawatesa wengi ziko katika makundi haya;


1. Laana zinazotokana na shetani.


✓Hizi laana zinampata mtu asiyeokoka au mtu ambaye sio mwaminifu kwa MUNGU yaani hana kitu Cha ki MUNGU kinachoweza kuzuia laana husika.


2. Laana zinazotokana uganga na uchawi.


✓Hizi laana zinawapata wasio na YESU KRISTO au wanaoishi maisha ya michanganyo hivyo hawana nguvu za MUNGU katika KRISTO YESU hata zisiwapate.


3. Laana zinazotokana na wazazi.


✓ Laana hii inaweza kumpata mtu yeyote kama kosa lake limetamkiwa laana na anastahili kulingana na mbingu.


4. Laana kama adhabu ya MUNGU.


✓Laana hii inampata mtu yeyote ambaye amefanya machukizo yaliyopelekea laana ya MUNGU.


✓✓Laana ya MUNGU kuifuta ni hadi toba ya kweli lakini hizo laana za shetani, wachawi, waganga au majini kwa maombi katika jina la YESU KRISTO unaweza kuzifuta na zinafutika.


✓✓Kuna baadhi ya watu  laana kwao  imeanzia tangu watu wakiwa tumboni mwa mama zao, kwa sababu ya wazazi kutegemea wanadamu na sio MUNGU.


Yeremia 17:5-6 ' 'BWANA  asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA. Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. ''


✓✓Kuna wazazi wamelaani watoto wao na kusababisha madhara makubwa sana baadae katika maisha ya mtoto husika.


✓✓Dawa ya laana zote ni maombi katika jina la YESU KRISTO na uiruhusu damu ya YESU KRISTO ifute laana zote kwako.


✓✓Hakuna laana isiyofutika katika damu ya YESU KRISTO.


Usifurahie tu mtu kukuambia kwamba ''utakufa masikini''


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba ''hutaolewa hata ufanyeje''


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba ndoa yako itakufa.


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba hutapona huo ugonjwa.


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba haitakuja kutokea amani katika familia yenu au ukoo.


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba hutafaulu mitihani hata kama utasoma vipi.


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba hutapata kazi.


Usifurahie tu mtu kukuapia kwamba hadi umnyenyekee yeye ndio utafanikiwa katika maisha yako.


Futa maapizo yote mabaya kwa jina la YESU KRISTO na anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO.

+255714252292.

Ubarikiwe.

Comments