MAANA YA ULIMWENGU WA ROHO.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele 


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote. 
Rafiki yangu mmoja kutoka Kenya ameniuliza swali hili hapa chini.

Swali?

Mtumishi Mabula ,ninaomba kuelewa ni nini maana ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa giza?


Majibu ya Mtumishi Peter Mabula 


■Ulimwengu wa roho ni sehemu ya kiroho isiyoonekana ila inafanya kazi.

Ulimwengu wa roho unaofanya kazi uko wa aina 2.

1.  ■■Kwanza Ulimwengu wa roho wa Nuru ambao uko chini ya MUNGU na huko kwenye ulimwengu wa wa Nuru yuko MUNGU Baba, Bwana YESU KRISTO,  ROHO MTAKATIFU,  Malaika wa MUNGU na Wateule wa KRISTO waaminifu. 

Waefeso  1:3 "Atukuzwe MUNGU, Baba wa Bwana wetu YESU KRISTO, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake KRISTO; "

■Mwanadamu yeyote ukiokoka unaketishwa pamoja na KRISTO katika ulimwengu wa roho.  Anayekuketisha ni MUNGU Mwenyezi. 

Waefeso (Eph) 2:6-10 " Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika KRISTO YESU; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika KRISTO YESU.  Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU;  wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.  Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo. 

2. ●●Ulimwengu wa giza 

Wakolosai  1:13 "Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; "

Ulimwengu wa roho wa giza ni kinyume na Ulimwengu wa Nuru.

Ulimwengu wa roho wa giza yuko shetani,  Mnyama, Mizimu, Majini yote, wakuu wa giza, Wanadamu walio upande wa shetani na kila nguvu za giza.

Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. "

Nimetumia Neno "Mnyama" huyu ni msaidizi wa shetani ambaye dini zote zilizo nje na KRISTO humwabudu. Na kwa kumwabudu huyu Mnyama wanadamu husika moja kwa moja wanakuwa wanamwabudu shetani. 

Ufunuo  13:4 "Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? "

■Mambo yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yaani mambo yote tunayoyaona yakitendeka popote duniani na kwa yeyote chanzo cha hayo ni katika ulimwengu wa roho ama wa Nuru au wa giza.
Hakikisha wewe unakuwa upande wa ulimwengu wa roho wa Nuru.
Waefeso  3:10 "ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya MUNGU iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; "
MUNGU akubariki sana. 
By Mwl Peter Mabula. 
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele. 
+255714252292
Ubarikiwe 

Comments