UNATAKA KUJUA KUHUSU WOKOVU?


By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU 

■■Wokovu ni zawadi kutoka kwa YESU KRISTO.


 Tunaweza kupokea zawadi hii ya Wokovu tunapotubu dhambi zetu na YESU KRISTO anatupa msamaha wake.


Luka  1:77-79 " Uwajulishe watu wake WOKOVU, Katika kusamehewa dhambi zao.  Kwa njia ya rehema za MUNGU wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,  Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani."


 ●Kuwa na wokovu maana yake sisi si wenye dhambi tena waliokusudiwa laana ya milele.

 Adhabu ya dhambi zetu zilizofanywa inaondolewa kupitia toba katika Wokovu Wa KRISTO.  

Kwa hiyo badala ya kuhukumiwa kuwa wenye dhambi, baada ya kupokea zawadi hii kuu ya Wokovu, tunahesabiwa haki katika KRISTO. 


Warumi  10:10 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. "


  Kwa sababu KRISTO alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi, tunaweza kuondolewa dhambi zetu milele. 


■■Maana nyingine ya Wokovu ni Ukombozi kutoka nguvu ya adhabu ya dhambi tulizowahi kufanya tangu tunazaliwa.


Wokovu ndio Kuokoka,  hakikisha unaokoka rafiki yangu kwa kuupokea Wokovu wa Bwana YESU KRISTO. 

Kwa hiyo, wokovu ni ukombozi kutoka kwa nguvu na adhabu ya dhambi.


Waebrania  8:12 "Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. "


Kama hujaelewa kwamba ukimpokea YESU KRISTO kwa kuokoka unasamehewa dhambi zako zote na MUNGU hatazikumbuka ngoja nikupe andiko hilo kwa kiingeleza ambapo hiyo Waebrania 8:12 Biblia inasema hivi 

 "For I will be merciful to their unrighteousness, and their sins and their iniquities will I remember no more."


Ni hatari ukiukosa Wokovu Wa Bwana wetu YESU KRISTO. 

Mtu yeyote duniani hatakiwi kuukosa Wokovu Wa Bwana YESU KRISTO. 

Hakikisha uko wokovuni kuanzia leo.


Baadha ya hapo fanya hivi:

1. Ishindanie imani ya Wokovu wa KRISTO kwa kuhakikisha hakuna kitu au mtu yeyote anayekutoa ndani ya Wokovu. 


Yuda  1:3 Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. 



2. Anza kutangaza Wokovu wa KRISTO kwa watu wote wanaokuhusu.


1  Nyakati 16:23 Mwimbieni BWANA, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. 


 MUNGU akubariki na kukulinda.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika shamba la MUNGU Mwenyezi. 

+255714252292 (WhatsApp)

Ubarikiwe.





Comments