Peter na Jemimah Mabula Watenda kazi katika Shamba la MUNGU |
Najua unafahamu lakini ngoja nikujuze kidogo.
Mathayo 21:7-10 " wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake. Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la BWANA; Hosana juu mbinguni. Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?"
✓Huyu punda kwa sababu alikuwa amembeba YESU KRISTO alikuwa anapita kwenye barabara nzuri iliyokuwa imejaa nguo za thamani huku yeye akizikanyaga hizo nguo bila hofu Wala wasiwasi.
✓Watu walitandaza matawi na punda akapita akikanyaga bila wasiwasi kwa sababu tu alikuwa amembeba YESU.
✓Watu walikuwa wamejaa pande zote za barabara wakishangilia na kupiga makofi mengi huku punda akipita katikakati yao kwa madawa.
✓Watu walikuwa na furaha mno na tabasamu nyingi huku punda akipita katikati yao kwa madoido.
Hayo yote yalifanyika kwa punda kwa sababu Moja tu, Punda alikuwa umembeba Bwana YESU.
Ulishawahi kujiuliza huyo punda angekuwa peke yake ingekuwaje?
Jibu ni kwamba asingeruhusiwa kukanyaga nguo za thamani, yale matawi aliyowekewa kwa heshima yangegeuka viboko vya kumchapa.
Asingeruhusiwa kupita katikati ya watu.
Punda huyu alipita hadi sehemu asiyotakiwa kwa sababu tu alikuwa amembeba YESU.
✓✓Wewe ukumbeba YESU KRISTO unaweza ukapita hata kwenye ngome za wachawi lakini hawatakufanya lolote kwa sababu tu umembeba YESU KRISTO asiyeshindwa.
1 Yohana 4:4 "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia."
✓✓Ndugu kama ukimbeba YESU KRISTO moyoni mwako unaweza kuishi hata sehemuu ambazo wengine wanasema mwanadamu Fulani hawezi kuishi kwa sababu eneo hilo ni mkao ya nguvu za giza.
✓✓Ndugu, mbebe YESU KRISTO utapita kila sehemu na nguvu za giza hazitakugusa.
✓Unambeba YESU KRISTO kwa namna gani?
✓✓✓Unambeba YESU KRISTO kwa njia ya kumpokea kwa Imani moyoni mwako kama Mwokozi wako.
Yohana 1:12" Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;"
Tendo hilo la kumpokea YESU KRISTO linaambatana na kuongozwa sala ya Toba Kisha ukatubia dhambi zako zote na kuziacha.
Mathayo 3:2 "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."
Ukifanya hivyo YESU anakuwa moyoni mwako hivyo unakuwa umembeba na baada ya hapo itakupasa kuukulia Wokovu wake kwa mafundisho ya Neno lake Kanisani.
✓✓Kumbeba YESU KRISTO ndio Kuokoka kwa Jina lingine.
Ndugu ukimbeba YESU KRISTO moyoni mwako utapata mambo haya mazuri sana.
1. MUNGU wa Mbinguni na YESU KRISTO watafanya makao kwako.
Yohana 14:23" YESU akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake."
2. Ufalme wa Mbinguni utakuwa ndani Yako maana una YESU KRISTO Mfalme wa ufalme wa Mbinguni.
Luka 17:21 "wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa MUNGU umo ndani yenu."
3. Roho Yako itakuwa hai kwa sababu ya haki.
Warumi 8:10 "Na KRISTO akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki."
4. ROHO MTAKATIFU ataanza kukaa ndani Yako.
1 Wakorintho 3:16 "Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la MUNGU, na ya kuwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu?"
5. ROHO MTAKATIFU ataanza kusema ndani Yako.
Mathayo 10:20 "Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni ROHO wa Baba yenu asemaye ndani yenu."
6. MUNGU wa Mbinguni ataanza kutenda kazi ndani Yako.
Wafilipi 2:13 ''Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.''
7. Jina la YESU KRISTO litatukuzwa ndani Yako.
2 Wathesalonike 1:12" jina la Bwana wetu YESU litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya MUNGU wetu na ya Bwana YESU KRISTO."
✓✓Ndugu yangu je unataka usizuilike na majini au mapepo au mizimu?
Basi mbebe Bwana wetu YESU KRISTO.
✓✓Je unataka wachawi na waganga na wasoma nyota na mawakala wa Shetani wasikuweze?
Basi mbebe YESU KRISTO.
✓✓Je unataka kushinda na zaidi ya kushinda?
Basi jibu ni Moja tu mpokee YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Warumi 8:37 "Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda."
Okoka ndugu, acha dhambi maovu na makosa.
Ishi Maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni.
+255714252292(Whatsapp, sadaka ya kupeleka Injili pamoja na ushauri wa kiroho)
Ubarikiwe
Comments