Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
Kama umewahi kushuhudia Injili mitaani utanielewa vizuri Zaidi juu ya watu kuchukia Neno la MUNGU.
Siku moja tulikuwa tunashuhudia mitani Injili ya KRISTO, mzee mmoja alitufukuza akionyesha chuki kama kwamba sisi ni watu wabaya sana na kumbe tunatangaza habari za Wokovu wa YESU tu.
Siku moja pia nikiwa Mkoa fulani tulikuwa tunashuhudia Injili nyumba kwa nyumba na tulipofika nyumba Fulani mzee mwenye nyumba alitoka kwa hasira sana akisema ‘’tokeni haraka kabla sijachukua hatua’’.
Sehemu nyingine tulifika na kuanza kuwaeleza kwa upole familia ile habari za YESU walikataa na ukitazama nyuso zao zimekunjamana kwa hasira kali kana kwamba wameudhiwa sana, wakawa wanatufukuza lakini tukasema kama wamemkataa YESU kwa Wokovu hamna tatizo ila YESU pia anaponya hivyo ambaye anaumwa ana vifungo vya giza tuko tayari kumuombea na Bwana YESU atamponya muda ule ule, wakajitokeza baadhi na tulipowaombea Bwana YESU aliwaponya ndipo hasira yao yote iikaisha. Nikawa najiuliza ‘’Kwanini watu wanachukia Neno la kweli la MUNGU?’’
Je ‘’Ni nini hasa wanakichukia katika Injili?’’
Inawezekana na wewe umewahi kupitia mambo kama haya.
Hapa chini nakuletea mambo matano hasa ambayo watu wa Mataifa huchukia katika Injili .
1. Wanachukia tukihubiri kwa jjina la YESU KRISTO.
Matendo 4:18 "Wakawaita, wakawaamuru WASISEME KABISA WALA KUFUNDISHA KWA JINA la YESU."
Unaona hapa Mitume wa Bwana YESU KRISTO wakikatazwa kufundisha kwa Jina la YESU KRISTO na wakikatazwa kusema kwa Jina la YESU KRISTO.
Hapo unagundua watu wa Mataifa huchukia Jina la YESU KRISTO lenye uzima wao.
✓✓Watu wengi sana na hasa wenye nguvu za giza ndani yao huchukia tukihubiri kkwa jina la YESU KRISTO.
Kama tungehubiri kwa jina la Mwanadamu au la Malaika wasingechukia lakini hakuna jina la Malaika wala la Mwanadamu yeyote tunaloweza kuhubiri kwalo ila tuna jina la YESU KRISTO hivyo hata kama watu hawalitaki jina la YESU hatutaacha kulihubiri maana hakuja jina lingine mbinguni na duniani litupasalo wanadamu wote kuokolewa kwako ila ni jina la YESU KRISTO.
Matendo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAPANA JINA JINGINE CHINI YA MBINGU WALILOPEWA WANADAMU litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
Ila ni Jina la YESU KRISTO tu.
Biblia inaonyesha maeneo kadhaa namna ambavyo watu wenye vifungo vya giza walivyokuwa hawataki kuhubiriwa kwa jina la YESU KRISTO.
Matendo 5:28-29 "akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi KWA NGUVU, MSIFUNDISHE KWA JINA HILI? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Petro na mitume wakajibu, wakisema, IMETUPASA KUMTII MUNGU KULIKO WANADAMU."
✓✓Lakini Wahubiri wa kweli miaka yote na hadi mwisho wa ulimwengu wanahubiri na watahubiri kwa jina la YESU KRISTO.
Hata Bwana YESU alilijua hili mapema kwamba Watumishi wake watachukiwa baadhi ya maeneo kwa sababu ya jina lake.
Luka 21:17-19" NANYI MTACHUKIWA NA WATU WOTE KWA AJILI YA JINA LANGU. Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu."
✓✓Kama wewe ni Mtumishi wa kweli wa MUNGU aliyeumba mbingu na dunia basi utaendelea kuhubiri kwa jina la YESU KRISTO maisha yako yote.
2. Wanatuchukia sisi Wahubiri kwa sababu tumelibeba jina la YESU KRISTO.
Mathayo 10:22 "NANYI MTAKUWA MKICHIKIWA NA WATU WOTE KWA AJILI YA JINA LANGU; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka."
✓✓Kama umelibeba jina la YESU KRISTO ni rahisi mno kuchukiwa na watu wa ulimwengu huu hasa walio na nguvu za giza ndani yao maana ndani yako umelibeba jina la YESU KRISTO.
Mathayo 24:9 "Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; NANYI MTAKUWA WATU WA KUCHUKIWA NA MATAIFA YOTE KWA AJILI YA JINA LANGU."
Bwana YESU mwenye Wokovu wa milele kwa watu wote alilisema hili mapema sana ili Mtumishi wake ikitokea umechukiwa na watu kwa sababu ya jina la YESU KRISTO usiogope bali zidi sana kuwaeleza watu Wokovu wa thamani ulio katika jina la YESU KRISTO.
Matendo 5:40 "Wakakubali maneno yake; nao walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake YESU; kisha wakawaacha waende zao."
3. Watu wanachukia kuhubiriwa habari za ufufuo wa watu katika KRISTO.
Matendo 4:1-2 " Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, WAKIFADHAIKA SANA KWA SABABU WANAWAFUNDISHA WATU NA KUHUBIRI KATIKA YESU UFUFUO WA WAFU."
Watu wa dini zingine wanajisikia vibaya na wanakuwa wanyonge wanapoambiwa kwamba Wafu wote watafufuliwa kwa sababu na Bwana YESU KRISTO atakayehukumu wanadamu wote.
Mathayo 24:30-31 " ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu."
Unajisikiaje uko katika dini au dhehebu lakini hata ukiwauliza viongozi wako wa dini wanasema wanasubiri ujio wa YESU, yaani wanasubiri ujio wa YESU na sio yeyote kutoka katika dini yao.
Mathayo 25:31-32 " Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;"
Unajisikiaje una dini nzuri ila haihusiki na YESU lakini viongozi wa dini Yako wanakuambia siku ya mwisho YESU KRISTO ndiye atahukumu wanadamu wote.
Ukiamua kufuata ukweli lazima tu umfuate YESU KRISTO ila ukiamua kufuata dini Yako lazima umchukie YESU na uchukie ufufuo wa Wafu kama andiko hapo juu linavyoonyesha watu walichukia Kuhubiriwa ufufuo wa Wafu.
4. Watu wanatuchukia kwa sababu hatuabudu miungu yao.
Kumbu 6:14 "Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;"
Dini zote zilizo nje ya Wokovu wa KRISTO ni waabudu miungu au kwa jina lingine ni waabudu shetani hivyo lazima wawe kinyume na KRISTO kwa sababu wao wako upande wa miungu, wamedanganywa kwa mafundisho ya uongo na wakajiona wako upande wa MUNGU na kumbe sio kweli.
Mtu anayeabudu sanamu au mizimu ukimkemea kwa habari ya mizimu yake lazima aweke chuki kama hataki kuiacha hiyo miungu.
5. Ni kwa sababu watu wengi wa mataifa hamtambui Bwana YESU kwa usahihi
1 Yohana 3:1 "Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa BABA, kwamba tuitwe wana wa MUNGU; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, KWA KUWA HAUKUMTAMBUA YEYE."
Watu wengi wa mataifa hawamtambui Bwana YESU inavyowapasa kumtambua, inatupasa sisi Watumishi wa MUNGU kuwajulisha watu hao kuhusu YESU ili wamtambue.
Kuna watu akili zao kwa kufundishwa uongo zinaishia tu kumtambua YESU kama Nabii Issa, YESU KRISTO Wala sio Nabii Issa.
Kuna watu akili zao zinaishia kumtambua YESU kama Mtoto wa seremala.
Kuna watu akili zao zinaishia tu kumtambua YESU kama Mtume, YESU ndiye aliyetuma Mitume.
Kuna watu akili zao zinaishia tu kumtambua YESU KRISTO kama Mtu maarufu lakini YESU ni zaidi ya Mtu maarufu yeyote unayemfahamu.
Ni wajibu wetu kama Watumishi wa MUNGU kuwaeleza watu kuhusu YESU KRISTO Mwokozi kwa usahihi
YESU sio wa ulimwengu huu, tusimfananishe na wanadamu kadhaa waliowahi kuishi Duniani na kuanzisha dini za uongo.
Yohana 8:23-25 " Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu. Basi wakamwambia, U nani wewe? YESU akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia."
Asante rafiki yangu kwa kujifunza Neno hili la MUNGU leo.
Kabla sijahitimisha leo ninalo Neno la mwisho kwa ajili yako.
Je umeokoka?
Kama umeokoka endelea na Wokovu wa Bwana YESU KRISTO hadi mwisho wa maisha yako.
Na wewe ambaye hujaokoka nakuomba okoka leo maana tunaishi siku za Mwisho.
Ni YESU tu ndio anayeweza kuliandiika jina lako kwenye kitabu cha uzima hata upate Uzima wa milele, nakuomba sana mpokee YESU KRISTO leo kwa ajili ya Wokovu.
Huko huko uliko tafuta Kanisa la kiroho wanaohubiri Wokovu Wa KRISTO ukamweleze Mchungaji atakuongoza sala ya toba na utakuwa umeokoka.
Fanya hivyo kwa faida ya roho yako milele
MUNGU akubariki.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.
+255714252292(Sadaka ya kupeleka Injili, Maombi na ushauri)
Ubarikiwe sana
Comments